International Schools zina nini cha zaidi?

International Schools zina nini cha zaidi?

ANAANDIKA BICHWA KOMWE:-

Hizi shule zinazoitwa "international schools" zinafundisha nini cha ziada sana ambacho hakimo penginepo?

Ni kweli, shule zina mazingira mazuri na yanayofurahisha, lakini je, kile wanachofundishwa wale watoto kina hadhi gani ya kulipiwa mamilioni?

Hapa ieleweke vema kwamba siungi mkono mashule ya kata ambayo kimsingi ni mashule butu yasiyo na sifa wala vigezo vya kuwa shule. Mashule ya kata ni maeneo maalumu ambayo watoto wanaenda kujazwa ujinga na kupoteza wakati.

Hizi international schools pia ni kama mashule ya kata yaliyochangamka tu isipokuwa pale unaenda kununua KIINGEREZA kwa milioni hamsini kwa mwaka.

Zaidi sana mtoto atapewa midoli ya kuchezea na mabembea ya kuning'inia. Of course bila kusahau CHETI CHA KIINGEREZA.

Linapokuja swala la maarifa ni kitu kingine kabisa. Hawa watoto ni makanjanja tu kama watoto wengine wanaosoma kwenye mashule ya kata.

Mpaka sasa sijaona ni kwanini mtoto akanunue Kiingereza kwa shilingi milioni hamsini wakati mtu anaweza kujifunza Kiingereza hata chini ya mti na akabukua vema tu kama makanjanja wengine akina Dayamondi waliojifunza Vingereza magetoni.

Tukiwawezesha hawa walimu wetu uchwara wa shule za Kata wataweza kufundisha kizungu vizuri tu.

Tuanze kudahili walimu ambao wana ufaulu mkubwa badala ya kudahili vilaza wenye MADIVISHENI FOO ati ndio wakawe walimu!

Hili lizingatiwe sana.
ukiwa maskini automatikali akili yako inajidifensi kuona hizo shule hazina kitu ila ungekua na pesa nadhani ungeelewa zaidi maana akili i gekua inaona mazuri zaidi kuliko mabaya
 
Huna hela ndio maana unauliza maswali ya ajabu ajabu ungekuwa na hela ungempeleka mtoto wako huko we unategemea watoto wa akina Mwigulu wasome kwenye hiyo mishule yenu.Tuseme tu ukweli mitoto inayosoma kayumba ni.mishenzi mishenzi.Huku kwetu vibao vya mitaa vyote vomeshaharibiwa na hii mitoto mishenzi mishenzi ya Kayumba.Watoto wanaosoma shule za maana huwa wanakuwa wastaarabu mno tofauti na hii mitoto ya Kayumba
 
This is really myopic. Extremely myopic!

Kumbe lengo la kusoma INTERNATIONAL SCHOOL ni kwenda uRaya kufanya interviews na wazungu?

Na kwanini wasome mtaala wa wazungu? ili iweje? wakawe vijakazi wa uRaya?
Mkuu....shida ya mitaala yetu.
  • Nadharia nyingi kuliko vitendo
  • Bado inatupa elimu ya kikoloni ya kuwa vijakazi
  • Haijui hata lugha ipi ni bora kwa ajili kufundishia
  • Unafunzwa vitu vya miaka 40 hadi 50 hamsini nyuma
  • Hata hizo maabala ni za enzi hizo za akina Newton
  • Mwanafunzi anabeba begi kubwa kama anaenda Panda milima
  • Inajikita kwa mwanafunzi kumeza kuliko kuelewa
  • Mwalimu anafundisha masomo yote
Nenda vyuoni sasa
  • Kuna vyuo vya Uhandisi watu tuliosoma hadi masomo 15 kwa semister,,,
  • Watu wa arts walichaguliwa fani za Uhandisi na hadi sasa wapo mtaani
  • Watu wanakopi na kupaste research na wahadhiri hawana hata mda.
  • Maabala hazifanyi kazi
Njoo mtaani
  • Kuna watu wamehitimu lakini tuliosoma nao mpaka tunacheka kama mjaamaa anaenda mtibu mtu
  • Sasa tafuta watu waliogusa hata degree moja huko Ulaya au America uone walivyo moto...
  • Mfano mzuri mtaalam mwenyewe Chenge the Don,kila skendo ya wizi yupo ila hakuna wa kumgusa, uone elimu ya Havard inavyofanya kazi.
 
ANAANDIKA BICHWA KOMWE:-

Hizi shule zinazoitwa "international schools" zinafundisha nini cha ziada sana ambacho hakimo penginepo?

Ni kweli, shule zina mazingira mazuri na yanayofurahisha, lakini je, kile wanachofundishwa wale watoto kina hadhi gani ya kulipiwa mamilioni?

Hapa ieleweke vema kwamba siungi mkono mashule ya kata ambayo kimsingi ni mashule butu yasiyo na sifa wala vigezo vya kuwa shule. Mashule ya kata ni maeneo maalumu ambayo watoto wanaenda kujazwa ujinga na kupoteza wakati.

Hizi international schools pia ni kama mashule ya kata yaliyochangamka tu isipokuwa pale unaenda kununua KIINGEREZA kwa milioni hamsini kwa mwaka.

Zaidi sana mtoto atapewa midoli ya kuchezea na mabembea ya kuning'inia. Of course bila kusahau CHETI CHA KIINGEREZA.

Linapokuja swala la maarifa ni kitu kingine kabisa. Hawa watoto ni makanjanja tu kama watoto wengine wanaosoma kwenye mashule ya kata.

Mpaka sasa sijaona ni kwanini mtoto akanunue Kiingereza kwa shilingi milioni hamsini wakati mtu anaweza kujifunza Kiingereza hata chini ya mti na akabukua vema tu kama makanjanja wengine akina Dayamondi waliojifunza Vingereza magetoni.

Tukiwawezesha hawa walimu wetu uchwara wa shule za Kata wataweza kufundisha kizungu vizuri tu.

Tuanze kudahili walimu ambao wana ufaulu mkubwa badala ya kudahili vilaza wenye MADIVISHENI FOO ati ndio wakawe walimu!

Hili lizingatiwe sana.
Tuliza komwe lako kabla hujapost,.........
 
Unavosema ni kweli kutokana na fikra zako. Ila, umechanganya mafaili. Kuna shule za St. kayumba, English medium n international schools.
St kayumba ndio zimetapakaa, hizi sote tunazijua so hamna haja ya kuzitilia mkazo. English medium pia zina madaraja, la kawaida n la juu. Kawaida ni bora English inazungumzwa tu ila bora, wanazingatia mambo mengi nje ya kuongea English tu. Mfano, St marrys, kule bata na watoto wanalelewa kama kuku wa kienyeji. Mtoto wa St marrys English kama lugha ya Mama tu, ila ukimpa swali lenye utatanishi, utaona anajing'atang'ata. Mfano wa shule bora ni ahmes, kule sio kingereza tu, mtoto anapelekwa mbio na analazimishwa kuzingatia kila jambo linalohusiana n malezi yake bora kielimu. Mwanafunzi wa ahmes ukimpeleka hizo st kayumba zenu au local English medium schools, anafundisha kwa utuo na wanafunzi watamuelewa.
Alafu kuna International schools. Hizi ni tofauti sana. Kwanza naomba nianzie kwenye usaili wa walimu wao. Mwalimu wa somo flani ni lazima awe alipiga A kwenye somo analofundisha, lafudhi yake iwe haijaathiriwa na lugha ya mama, sio kuongea tu, ila ni lazima awe na uwezo wa kuwasiliana kwa ufanisi wa hali ya juu.
Kuna kitu kinaitwa education systems, kwa tz ni lasaba, form 6 n chuo ni 3 yrs, so mfumo wetu wa elimu ni 7.6.3, Kenya ni la 8, form 4, chuo 4, hivyo ni 8.4.4, ambapo jumla hadi mwanafunzi kumaliza ni miaka 16. Ila kwa International schools, wale wanatumia mfumo tofauti kabisaaaaa. Kwanini, Mfano sisi 7.6.3, mtoto anafundishwa vitu vingi ambavyo havitomsaidia katika maisha yake, ni kama kunywa maji ya mto maana yanaonekana ni masafi. Ila kwa International schools, mtoto anafundishwa vitu vichache vya msingi tu. Juu ya yote, hadi kuitwa international, basi inamaanisha system/mfumo wake wa elimu ni wa kimataifa. Ninamaanisha, shule nyingi zinafundisha elimu ya nchi nyingine, haswa UK. Na kwa wastani, kati ya shule 100, 95 wanafundisha British system ambayo cjafuatilia ni miaka mingapi mtoto kumaliza shule, ila ninachojua mwanao akiwa 6, upande wa British system atakuwa anamalizia chuo.
So hizo ni shule zina walimu wazuri sana na waliobobea kwenye taaluma(sio failures)* kwanza nyingi zinanunua taaluma kutoka walimu wa nchi za nje, mazingira ya shule mazuri yenye kila kitendea kazi tena venye ubora na kila kitu chao ni bora.
Ndani ya maisha yangu, nimekutana na wanafunzi kutoka shule ya strathmore pale nairobery, kwenye hafla ya music festival. Wale wanafunzi ni bora ndugu zangu. Kichwani wapo vzuri kinoma, ukiwa karibu nao lazima ujishtukie. Ile shule ni ya boys, ila nilikutana n boys wanaimba soprano zaidi hata mabinti wa shule yangu. Mwalimu wao wa music alikuwa ni mmorocco, kila item either washike no 1 sisi no 2 au vice versa. Wanafunzi wa karura tulizoea kuwaonea wote tunaokutana nao ila sio wale binadamu. Aisee kwa experience nikiyoipata, inatosha kusema kati ya ndoto yangu kubwa zaidi ni mwanangu kuja kusomea strathmore kuanzia pri hadi seco. Tukiskia International school tuache fitna, tuzipe heshima zake. Zile ni shule na ni shule kweli kweli. Umasikini usitufanye kuvikebehi vitu bora kutokana hatuwezi kuviafford. Vijana tafuteni pesa watoto wetu waje kupata elimu bora, sio bora elimu. Ni fahari sana kwa mzazi kumuona mwanae akiwa bora upstairs. International schools sio 5 stars hotels, Zile ni shule n nusu.
Hiyo shule ipo Kenya tu?
 
Unajua oysterbay na masaki mipaka inazingua,nami nimeishi huko kabla ya oysterbay hospital,,sitaki kufungua code kuhusu mtaa coz huenda nikatambulika
Barabara ya Msasani Road ndiyo mpaka wa Masaki na Oysterbay...
Pale Haile Selassie road kwenye kile kimteremko ndipo kuna bara inaunda junction ya kwenda Beach....
Sisi home kulikuwa na Ramani za mitaa za kata ya Msasani yote...
 
Asante kwa kunifahamisha,,kile kimteremko kilikuwa kinaitwa kilima nyege coz kinashuka ghafla bin vuu 😂😂
 
Back
Top Bottom