Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi unajua wafunzi wengi wanaotoka hizo shule za international wanaenda kusoma vyuo vikubwa duniani kamaANAANDIKA BICHWA KOMWE:-
Hizi shule zinazoitwa "international schools" zinafundisha nini cha ziada sana ambacho hakimo penginepo?
Ni kweli, shule zina mazingira mazuri na yanayofurahisha, lakini je, kile wanachofundishwa wale watoto kina hadhi gani ya kulipiwa mamilioni?
Hapa ieleweke vema kwamba siungi mkono mashule ya kata ambayo kimsingi ni mashule butu yasiyo na sifa wala vigezo vya kuwa shule. Mashule ya kata ni maeneo maalumu ambayo watoto wanaenda kujazwa ujinga na kupoteza wakati.
Hizi international schools pia ni kama mashule ya kata yaliyochangamka tu isipokuwa pale unaenda kununua KIINGEREZA kwa milioni hamsini kwa mwaka.
Zaidi sana mtoto atapewa midoli ya kuchezea na mabembea ya kuning'inia. Of course bila kusahau CHETI CHA KIINGEREZA.
Linapokuja swala la maarifa ni kitu kingine kabisa. Hawa watoto ni makanjanja tu kama watoto wengine wanaosoma kwenye mashule ya kata.
Mpaka sasa sijaona ni kwanini mtoto akanunue Kiingereza kwa shilingi milioni hamsini wakati mtu anaweza kujifunza Kiingereza hata chini ya mti na akabukua vema tu kama makanjanja wengine akina Dayamondi waliojifunza Vingereza magetoni.
Tukiwawezesha hawa walimu wetu uchwara wa shule za Kata wataweza kufundisha kizungu vizuri tu.
Tuanze kudahili walimu ambao wana ufaulu mkubwa badala ya kudahili vilaza wenye MADIVISHENI FOO ati ndio wakawe walimu!
Hili lizingatiwe sana.
Bila shaka anazungumzia Internatinal school as international school. Sio EM. Ndio maana kwenye ada kataja 50MKuna international school na kuna English medium hizo international school achana nazo hizo zina watu na hadhi zao.
Halafu hizi English medium nadhani ndio unaziongelea wewe of which una point nzuri.
Nimeipenda hiiElimu ni gharama ,asije kukudanganya mtu uwekezaji thabiti kwenye elimu ndio ukombozi wa nchi
Hujiulizi kama ada ya 50M mwalimu anayefundisha hao wanafunzi , nyenzo za kisasa za kujifunzia na viwango vya kimataifa vya mitihani wanaofanya hao wanafunzi.
Maslahi ya mwalimu kuanzia mshahara , malazi , usafiri , chakula na kadhalika mwalimu lazima atakua focused kwa kiasi kikubwa kuendana na viwango vya kimataifa vya hizi shule maana mwisho wa siku anafanyiwa tathmini kwa alichokifanya.
Serikalini huko CCM inawalipa walimu mishahara kiduchu na kuwakamua kwenye vyama visivyo na msaada kutetea maslahi yao ni miaka mingi sana walimu wamekuwa "laughing stock" kwa mishahara na hadhi wanayopewa ilhali hawa ndio watu waliomuandaa kila mmoja wetu hadi kufika hapa tulipo .
Pia mitaala ya hizo shule inaanza kumuandaa mwanafunzi kuwa mtu fulani moja kwa moja na mwisho inawajengea "exposure" kwa safari za mataifa tofauti tofauti ili kuwakutanisha na wenzao wa mataifa tofauti wangali wadogo.
Mtoto akitoka hapo lazima awe wa tofauti sana huwezi kulinganisha na elimu ya anayepata huyo wa elimu bure isiyo na kiwango.
Najua watu watasema mbona nchi zingine wanasoma bure , ndio ni bure ila bure yenye kiwango cha hali ya juu kodi ya mwananchi inatumika 100% kweli na inaonekana kuitoa elimu bure ndio maana hata mataifa hayo ya elimu bure wengi husoma shule za umma kuliko hata za private maana ni bure na ni bure yenye kiwango cha hali ya juu.
mambo baby 😂😂😂😂😂😂Bichwaaaa
Hasara sana 😂😂Watakwambia una wivu. Tafuta hela.
Kimsingi wanachoweza ni kuongea kingereza tu.
Maana wengine hata kufua nguo zao na chupi zao hawawezi.
Tupe madini love zina nini haswa
Haya mashule ya kata usiyabeze. Ni nafasi kubwa ya kila mwenye nia na uwezo wa kutoboa kupitia shule. Zamani kabla haya mashule hayajaja, Ndoto za wengi zilizimwa kutokana na kukosa nafasi za kuendelea na masomo baada ya Elowai. Japo walifaulu vizuri, lakini hawakwenda popote kutokana na nafasi kujaa mashuleni. Haya mashule ya kata yalikuja kufanya mapinduzi makubwa. Leo kuna madaktari, wahandisi, wahasibu, wanasheria wakubwa wametokea kwenye hayo hayo mashule. Usibeze ST. KAYUMBA zetu mzee, tunajua zilikotutoa hadi leo tupo hapa.Hapa ieleweke vema kwamba siungi mkono mashule ya kata ambayo kimsingi ni mashule butu yasiyo na sifa wala vigezo vya kuwa shule. Mashule ya kata ni maeneo maalumu ambayo watoto wanaenda kujazwa ujinga na kupoteza wakati.
Nani huyo mwenye ufaulu mkubwa atakubali kudahiliwa ualimu ili aje alipwe laki3 kwa mwezi na manyanyaso kibao?Tuanze kudahili walimu ambao wana ufaulu mkubwa badala ya kudahili vilaza wenye MADIVISHENI FOO ati ndio wakawe walimu!
Umeshawahi kujiuliza kwa nini Mwalimu wa English Medium anaweza asiwe na vigezo vya kukidhi kumfundisha International School?ANAANDIKA BICHWA KOMWE:-
Hizi shule zinazoitwa "international schools" zinafundisha nini cha ziada sana ambacho hakimo penginepo?
Ni kweli, shule zina mazingira mazuri na yanayofurahisha, lakini je, kile wanachofundishwa wale watoto kina hadhi gani ya kulipiwa mamilioni?
Hapa ieleweke vema kwamba siungi mkono mashule ya kata ambayo kimsingi ni mashule butu yasiyo na sifa wala vigezo vya kuwa shule. Mashule ya kata ni maeneo maalumu ambayo watoto wanaenda kujazwa ujinga na kupoteza wakati.
Hizi international schools pia ni kama mashule ya kata yaliyochangamka tu isipokuwa pale unaenda kununua KIINGEREZA kwa milioni hamsini kwa mwaka.
Zaidi sana mtoto atapewa midoli ya kuchezea na mabembea ya kuning'inia. Of course bila kusahau CHETI CHA KIINGEREZA.
Linapokuja swala la maarifa ni kitu kingine kabisa. Hawa watoto ni makanjanja tu kama watoto wengine wanaosoma kwenye mashule ya kata.
Mpaka sasa sijaona ni kwanini mtoto akanunue Kiingereza kwa shilingi milioni hamsini wakati mtu anaweza kujifunza Kiingereza hata chini ya mti na akabukua vema tu kama makanjanja wengine akina Dayamondi waliojifunza Vingereza magetoni.
Tukiwawezesha hawa walimu wetu uchwara wa shule za Kata wataweza kufundisha kizungu vizuri tu.
Tuanze kudahili walimu ambao wana ufaulu mkubwa badala ya kudahili vilaza wenye MADIVISHENI FOO ati ndio wakawe walimu!
Hili lizingatiwe sana.
Kama jina lilivyo walimu wake ni international,mazingira ya shule ni bora kuanzia (madarasa,hostel,vyakula ni kama wako hotelini),wanafunzi wanahudumiwa kwa ukarimu/hospitable,facilities zote za kusomea zinapatikana kuanzia vitabu hadi computers,walimu wanalipwa vizuri kwa hiyo wanajituma sana kufanya kazi yao kiufasaha tofauti na kwenye shule za serikali walimu wanafundisha huku wakiwa na stress kwa hiyo wanalipua kazi yao bora liende,mtoto akielewa somo ni sawa na asipoelewa pia nu sawa potelea mbali hawana hasara.Hiyo international school ina kitu gani cha tofauti sana?
Sasa kufua nguo zako ni taaluma ya kukuletea mlo mezani....🤣🤣🤣Watakwambia una wivu. Tafuta hela.
Kimsingi wanachoweza ni kuongea kingereza tu.
Maana wengine hata kufua nguo zao na chupi zao hawawezi.
HahahaaSasa kufua nguo zako ni taaluma ya kukuletea mlo mezani....🤣🤣🤣
Pata hela umtoe mwanao kwenye mateso mkuu....🤣🤣🤣mtoa mada azingatiwe hizi shule ukiacha ada kubwa na kiingireza basi hakuna cha ziada.
Inawezekana UDSM ikawa ndiyo Chuo Kikuu bora kabisa duniani! Kwani kuna kinachoshindikana Tanzania?Ipo siku mtakuja sema
Vyuo kama Havard na Oxford havina vya kuvizidi vyuo vya Bongo....nyie endeleeni tu.
Je,hapa tunaongea na GoldDhahabu Mdogo au mtu mzima...kwanza tujuze tusije ua Mende kwa nyundo.Inawezekana UDSM Ika wa ndiyo Chuo Kikuu Bora duniani! Nini kinashindikana Tanzania?
Nilipokuwa "mdogo", nilimsikia:
1. JWTZ ndilo Jeshi bora duniani
2. Tanzania inashika nafasi ya pili duniani kwa ukachero.
Lakini baada ya kuwa mtu mzima, ingawa ninaviamini vyombo vyetu vya dola, hasa JWTZ, nimebaini mengine "nilidanganywa"