Kuna mambo ambayo wazazi na walimu huwa hawazingatii kutoka kwa watoto hasa katika mchakato mzima wa mtoto kupata elimu.
Pasipo kufahamu haya madogo ndio makubwa zaidi katika kumjenga mtoto kiuelewa ambapo itakuwa ni msaada mkubwa sana kwake katika maisha yake yote yaliyobaki kitaaluma, kazini na hata katika utu uzima wake baadae.
International schools ni zaidi ya english na masomo haya ya kawaida wanayosoma English Medium na kayumba.
Mambo madogo madogo ambayo hizi shule za kawaida hawazingatii kule international schools wanazingatia.
Katika kitu ambacho nili notice binafsi.
Uwezo tu wa kujiamini wa mtoto anayesoma International school ni next level, mtoto anafundishwa confidence ya hali ya juu anaweza kusimama mbele ya watu 1000 na akazungumza kwa kujiamini sana, na sio hawa watoto wa kayumba akiona mwalimu ni mbio na hajui hata anakimbia nini, ye anawaza fimbo tu, hio ni mbaya, mwalimu na mtoto ni maadui hapo saa 4 wapo wanapiga maembe na mawe kazi kweli kweli.
usizungumzie ubora wa elimu ya michezo na viwanja vya michezo, ubora wa maabara, computer room, maktaba hadi madarasa, vyakula n.k. plus watoto wanapewa care ya hali ya juu mfano uende 5 star hotel na kwa mama ntilie mtaani, mtoto anajiona special na wa thamani, haya ni mambo yanamjenga sana mtoto kisaikolojia.
Ukweli ni kwamba kila mmoja anatamani mwanae asome international ni ile tu uchumi hauruhusu.