Haya mashule ya kata usiyabeze. Ni nafasi kubwa ya kila mwenye nia na uwezo wa kutoboa kupitia shule. Zamani kabla haya mashule hayajaja, Ndoto za wengi zilizimwa kutokana na kukosa nafasi za kuendelea na masomo baada ya Elowai. Japo walifaulu vizuri, lakini hawakwenda popote kutokana na nafasi kujaa mashuleni. Haya mashule ya kata yalikuja kufanya mapinduzi makubwa. Leo kuna madaktari, wahandisi, wahasibu, wanasheria wakubwa wametokea kwenye hayo hayo mashule. Usibeze ST. KAYUMBA zetu mzee, tunajua zilikotutoa hadi leo tupo hapa.
Nani huyo mwenye ufaulu mkubwa atakubali kudahiliwa ualimu ili aje alipwe laki3 kwa mwezi na manyanyaso kibao?
Yaani mwalimu ni mnyonge kwa kila mtu. wazazi, wanasiasa, mbaya zaidi hadi walimu wenzao wanawanyanyasa.
Imargine. Mratibu kata, Afisa elimu wanawanyanyasa walimu. Achilia mbali madiwani, watendaji wa vijiji/kata. Hapo hawajaja wakaguzi siju wa nini nini huko, hajaja mkurugenzi kuwatishia kumwaga unga, hajaja mkuu wa wilaya kuwacharaza bakora mbele ya wanafunzi. Nani huyo alofaulu vizuri atachagua kuwa mwalimu?!
Ipewe heshima taaluma ya ualimu. Ipewe maslahi mazuri kazi ya ualimu kisha wenye ufaulu mkubwa wataifuata wenyewe. Kitu ambacho pia hakiwezekani kutokana na idadi yao.
MWISHO, uwezo wa mtu kufanya vitu vikubwa hapa duniani, mfano, kuwa kiongozi mzuri, inovator, Fundi mzuri, mfanya biashara mzuri mwenye mafanikio..etc, ni uwezo wa kuzaliwa nao. Shule inakuongezea kitu kidogo sana.
Actually, shule ukishajua kusoma, kuhesabu, na kuandika what else do you need to fit in a sucessiful life?
Ubaya ni kwamba inafika pahala tunazama sana katika shule mpaka tunajikuta tunapoteza our natural abilities kwa kulishwa bookish concerpts ambazo kimsingi ni ideas za watu wengine. Tunakuwa wao, sisi tunajipoteza. School doent let you think oitside the box. Anyway. Ninamengi ya kuandika kuhusu shule lakini basi acha nirudi kwenye mada.....
Tunachagua kuwapeleka watoto kwenye shule za bei mbaya ili tu wawe na mazingira bora ya kusoma. Kufuata mkumbo wakati mwingi. Kutaka uonekane unahela wakati mwingine, kuwaridhisha watu flani wakati mwingine, kuhisi huko ndiko kunaelimu bora wakati mwingine. Yaani sababu ni mingi.