International Schools zina nini cha zaidi?

Mfano international schools nyingi za hapa bongo zinafundisha biashara sana ndio maana wafanya biashara wengi wakubwaa wahindi, waarabu na wazungu watoto wao wapo huko
Shule za Tanzania haziwezi kufundisha BIASHARA?
 
Shule za Tanzania haziwezi kufundisha BIASHARA?
International business nasemea ..

Sisi hatuwezi bado utamfundisha mtoto international business wakati nchi ni third world country budget tu ya elimu almost 45 percent ni msaada..
 
International schools mtoto ana kuwa treated hadhi kubwa hata kama atakuwa kilaza kwenye curriculum anaweza kuwa bora kwenye extra curriculum ambazo ni tija kwake. Mfano arts and crafts, marital arts, foreign language nk
 
Zinafundisha Vingi sana Mtoto wa International School aliyemaliza Drs 7 ni sawa na Mtoto wa Secondary aliyemaliza Form four..
Ergo (Hence) Proved
International school zinakupa connection kitu cha mihimu katika zama hizi

Mtoto wako anasoma na watoto wakina gsm unafikiri atakua sawa na mtu aliyesoma kayumba
 
Unavosema ni kweli kutokana na fikra zako. Ila, umechanganya mafaili. Kuna shule za St. kayumba, English medium n international schools.
St kayumba ndio zimetapakaa, hizi sote tunazijua so hamna haja ya kuzitilia mkazo. English medium pia zina madaraja, la kawaida n la juu. Kawaida ni bora English inazungumzwa tu ila bora, wanazingatia mambo mengi nje ya kuongea English tu. Mfano, St marrys, kule bata na watoto wanalelewa kama kuku wa kizungu. Mtoto wa St marrys English kama lugha ya Mama tu, ila ukimpa swali lenye utatanishi, utaona anajing'atang'ata. Mfano wa shule bora ni ahmes, kule sio kingereza tu, mtoto anapelekwa mbio na analazimishwa kuzingatia kila jambo linalohusiana n malezi yake bora kielimu. Mwanafunzi wa ahmes ukimpeleka hizo st kayumba zenu au local English medium schools, anafundisha kwa utuo na wanafunzi watamuelewa.
Alafu kuna International schools. Hizi ni tofauti sana. Kwanza naomba nianzie kwenye usaili wa walimu wao. Mwalimu wa somo flani ni lazima awe alipiga A kwenye somo analofundisha, lafudhi yake iwe haijaathiriwa na lugha ya mama, sio kuongea tu, ila ni lazima awe na uwezo wa kuwasiliana kwa ufanisi wa hali ya juu.
Kuna kitu kinaitwa education systems, kwa tz ni lasaba, form 6 n chuo ni 3 yrs, so mfumo wetu wa elimu ni 7.6.3, Kenya ni la 8, form 4, chuo 4, hivyo ni 8.4.4, ambapo jumla hadi mwanafunzi kumaliza ni miaka 16. Ila kwa International schools, wale wanatumia mfumo tofauti kabisaaaaa. Kwanini, Mfano sisi 7.6.3, mtoto anafundishwa vitu vingi ambavyo havitomsaidia katika maisha yake, ni kama kunywa maji ya mto maana yanaonekana ni masafi. Ila kwa International schools, mtoto anafundishwa vitu vichache vya msingi tu. Juu ya yote, hadi kuitwa international, basi inamaanisha system/mfumo wake wa elimu ni wa kimataifa. Ninamaanisha, shule nyingi zinafundisha elimu ya nchi nyingine, haswa UK. Na kwa wastani, kati ya shule 100, 95 wanafundisha British system ambayo cjafuatilia ni miaka mingapi mtoto kumaliza shule, ila ninachojua mwanao akiwa 6, upande wa British system atakuwa anamalizia chuo.
So hizo ni shule zina walimu wazuri sana na waliobobea kwenye taaluma(sio failures)* kwanza nyingi zinanunua taaluma kutoka walimu wa nchi za nje, mazingira ya shule mazuri yenye kila kitendea kazi tena venye ubora na kila kitu chao ni bora.
Ndani ya maisha yangu, nimekutana na wanafunzi kutoka shule ya strathmore pale nairobery, kwenye hafla ya music festival. Wale wanafunzi ni bora ndugu zangu. Kichwani wapo vzuri kinoma, ukiwa karibu nao lazima ujishtukie. Ile shule ni ya boys, ila nilikutana n boys wanaimba soprano zaidi hata mabinti wa shule yangu. Mwalimu wao wa music alikuwa ni mmorocco, kila item either washike no 1 sisi no 2 au vice versa. Wanafunzi wa karura tulizoea kuwaonea wote tunaokutana nao ila sio wale binadamu. Aisee kwa experience nikiyoipata, inatosha kusema kati ya ndoto yangu kubwa zaidi ni mwanangu kuja kusomea strathmore kuanzia pri hadi seco. Tukiskia International school tuache fitna, tuzipe heshima zake. Zile ni shule na ni shule kweli kweli. Umasikini usitufanye kuvikebehi vitu bora kutokana hatuwezi kuviafford. Vijana tafuteni pesa watoto wetu waje kupata elimu bora, sio bora elimu. Ni fahari sana kwa mzazi kumuona mwanae akiwa bora upstairs. International schools sio 5 stars hotels, Zile ni shule n nusu.
 
Ada yake ni kiasi gani? Na vipi wanazuiaje mtoto wa kiume asije kuwa shoga?
 
Nazn unamaanisha international school
Mtaala wanaotumia ni international huo ni utofaut Tuu
(Big difference is sylubus)
 
nilikutana n boys wanaimba soprano zaidi hata mabinti wa shule yangu. Mwalimu wao wa music alikuwa ni mmorocco

Yaani kujifunza muziki tu mpaka ukasome INTERNATIONAL SCHOOL na ulipie milioni hamsini? Sijaona cha ajabu hapo, hizi ni delusions of grandeur tu.

Tukiskia International school tuache fitna, tuzipe heshima zake.

Kwamba tuzipe heshima hizo shule kwa KUZISIKIA tu?

Kindly avail us with some statistical data as to the quality of education.
 
International school zinakupa connection
Connection gani bana 🀣🀣🀣

Kama unaweza kulipa milioni hamsini kwa mwaka, unashindwa vipi kumpa mwanao connection mpaka umpeleke INTERNATIONAL SCHOOL?

Hilo ndilo lengo la hizo shule? Kugawa "connections"?

Mambo ya connections ni nadharia za watu masikini tu.

Ukiwa tajiri na unaweza kulipa ada ya milioni hamsini kwa mwaka, hauhitaji connection yoyote.

Achana na nadharia za makapuku.
 
Kumbe BICHWA KOMWE - ukitulia hua unatema madini hivi! hua nakusoma kwenye utani utani wako tu.

πŸ˜€ πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…