International Schools zina nini cha zaidi?

Umeongea nini sasa shule za International huzitaki za kata pia huzitaki kwaiyo watoto wasisome
 
Kudahili walimu wenye ufaulu wa juu sio tija kwasababu swala la kumfundisha mtu akakuelewa halihitaji ufaulu mzuri ila mbinu madhubuti, mfumo wa kama unaotumiwa na wanafunzi wa Masters na PHD kwa Tanzania ni mzuri ukitumiwa kuanzia kidato cha kwanza.
 
bado mnachanganya kati ya English Medium Schools na Internationa schools. hata huko Uganda na Kenya kuna International schools ila hakuna English Medium Schools maana huko lugha ya kufundishia ni English.
 
Hujanielewa public speaking ni suala la kisaikolojia,tafuta six fears that face human beings. Na ilo la kuongea limo nadhani ni namba mbili Kama sio tatu.
Kujua na kutenda vitu viwili tofauti uelewe
kama ni swala la kisaikolojia huko IS wanafunzwa ndio maana watoto wa IS wanauwezo mkubwa wa kujieleza kwakua wameshajengwa kisaikolojia kwahyo hayo maswala ya sikisi fears tupa kule
 
Maskini mmeshaaza nongwa,

Hapo umeshakula zako kipolo Cha wali na chai ya mdalasin na sigara pembeni
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
I really trust desire of someone to reach the highest of his performance at his personal journey.
kama ni swala la kisaikolojia huko IS wanafunzwa ndio maana watoto wa IS wanauwezo mkubwa wa kujieleza kwakua wameshajengwa kisaikolojia kwahyo hayo maswala ya sikisi fears tupa kule
Hebu tuangalie big innovators na suala la shule walizosomea.
Am sure that going outside and buying expensive cigarettes won't make you rich.
Siamini kuwa kuwa shuleni Fulani inampatia mtu akili. Kila mtu ana uwezo wake na ishu kubwa ni desire ya mtu binafsi ku achieve maximum
 
Binafsi naheshimu sana kitu maarifa maana katika dunia ya sasa kinachotafutwa ni wewe una nini cha kutoa utatuzi wa changamoto zinazoikabili dunia.

Katika elimu yetu hii ya kidumu na mfagio inayomkaririsha mtoto majibu ya maswali ya mtihani badala ya kumfundisha kuwa na fikira tunduizi(critical thinking) na mdadisi huwezi kulinganisha na wenzetu wa mitaala ya kimataifa au hata baadhi ya English Medium kuanzia mazingira ya kujifunzia, nyenzo/vifaa hadi mfumo wa ufundishaji.

Tukubali tu kuwa ni umasikini ndio kikwazo lakini hakuna urithi bora kama elimu bora kwa mwanao.
 
Zama zimebadirika sana....
Sasa hivi baba, mama wote watafutaji. Na malezi ya watoto yameachwa kwa mtu wa tatu, msichana wa kazi, ndugu wa karibu, wa mbali jirani nk nk.
Yale masaa nane mtoto anayotumia akiwa shule, ni vyema mazingira ya shule yakawa salama kwao kiafya, kiakili, kimwili na imani pia.

Hapa ndipo umuhimu wa hizi shule unapo kuja, zina viwango vya kimataifa:
Yale matoto yenu yanayoshinda kwenye vibanda umiza kuangali video, chafu.
Yale matoto yenye kushinda kwenye ngoma na mikesha ya singeli,
Yale yale matoto yenye kushinda kwenye ku-bett,
yenye kujifunza misamiati na matusi mapya kila leo.

vyema yakasomea huukoo KATA

HATUTAKI HIYO MITOTO IJE IHARIBU WATOTO WETU!
ACHA WAO WASOME HUKO HUKO KATA, KWENYE SHULE ZA HADHI YAO.
 
Tuliosoma shule za kata ndio leo tunafanya mambo makubwa kwenye nchi
 
Watu wamekariri kwamba shule zote za magari ya njano ni international jambo ambao si kweli international school means mtaala wa elimu ni wa first nje hata baadhi ya waalimu ni wa nchi za nje ,let's say UK ,USA, na wana exposure na mambo mbalimbali unakuta eti mwalimu anajiita mwalimu wa international kisha tu sababu anafundisha watoto wa magari ya njano , huyo huyo mwalimu akiwa anatazama CNN news anatoka kapa hajui nini kinazungumzwa. International means international that's is not child play ,that's where children are taught how to interact with the world.
 
St.Jude hiyo,bonge la shule kuzidi hata baadhi ya vyuo vikukuu hapa Bongoland.
Kumbe wewe ni wa "kule"😀


Nilikwepa kuitaja jina lakini kumbe umeshainyaka.

Nilikuwepo siku mkurugenzi wa hiyo shule alipotangaza kusitihwa kwa mchakato wa St. Jude kutumia mitaala ya Cambridge kwa sababu walimu wake hawajui Kizungu cha Kimataifa😢😢😢
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…