Interpol: Mwenyekiti IEBC alihongwa $3M

Interpol: Mwenyekiti IEBC alihongwa $3M

Jameni haya mavitu mnayatoa wapi, licha ya kwamba sikumpigia Ruto kura na simpendi, ila mpaka sijaona sababu zozote zenye mantiki za kumkatalia urais, vyombo vyote hadi vya habari vina matokeo ya kila kituo, mbona wasijumuishe huko watuambie hii issue imekaa vipi.
Kama Wakenya wengi wamemchagua yeye, atunukiwe urais tusonge mbele na mengine, hii nchi ni yetu sote, waliomchagua na ambao hatukumchagua.

Huu ndio ukweli Ruto kampiga Raila ground, Ruto aapishwe maisha yaendelee kama kawaida maana tume ilikua wazi kiasi hata kipofu hawezi kusema chochote na wanataka kutia doa uchaguzi uliokua wa mfano Afrika nzima, na upande wa Raila wangejua wanaharibu sifa nzuri ambayo kila mtu kaiona kwa macho yake juu ya Kenya ya katiba mpya
 
Ili kampuni iamue kutoa rushwa ya pesa yote hiyo kwani gharama ya kuprint hizo ballot papers ni kiasi gani? Hii ni taarifa ya kumchafua Chibukati, waoneshe hiyo taarifa ya Interpol siyo gazeti liisemee.
Hapo sio kuuliza gharama ziko zaidi ya fedha Iyo na faida yake juu

Uchaguzi huwa unakula fedha mingi sana mkuu
 
Huu ndio ukweli Ruto kampiga Raila ground, Ruto aapishwe maisha yaendelee kama kawaida maana tume ilikua wazi kiasi hata kipofu hawezi kusema chochote na wanataka kutia doa uchaguzi uliokua wa mfano Afrika nzima, na upande wa Raila wangejua wanaharibu sifa nzuri ambayo kila mtu kaiona kwa macho yake juu ya Kenya ya katiba mpya
Mkuu kumbuka maafisa wa 4 kati ya 7 wanasema tume haikuwa wazi

Alafu wanabaki wa 3 ndo hao waliogawana fedha za rushwa inayosemwa na interlpool
 
Kwani karatasi zilifika lini mpaka hao Interpol watoe Taarifa leo baada ya Matokeo?
 
Haihusiani kivipi inaonekana hana msimamo sasa kama alichukua hela hyo atashindwa kuchukua na kwingine kama ni kweli itamletea shida
Itamletea shida kwenye mambo ya maadili lakini haitakua sababu ya kupinga matokeo ya Urais
 
Na watengezaji wa hizo hoax news ni wabongo hasa yale machawi ya CCM ili ku justify unyani wao wanaofanya hapa. CCM roho inawauma sana kwa yaliyotokea Kenya maana wamedhihirika wao ni Nyani kwa hii NEC yao.
Ndio akili na mawazo yako yalipoishia GT wa JF

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Shirika la Polisi wa Kimataifa Interpol limetoa taarifa inayomuanika Mwenyekiti wa Tume Huru na Mipaka ya Uchaguzi Kenya (IEBC) Bwana Wafula Chebukati na makamishna wawili wa tume hiyo kuwa walipokea rushwa ya Dola Milioni Tatu za Kimarrekani ili kuidhinisha kampuni iyakayochapisha karatasi za kupigia kura kwenye Uchaguzi mkuu wa Kenya.

Uchaguzi huo umekamilika baada ya Mwenyekiti wa atume kumtangaza Mshindi huku kukiwa na mgawanyiko baina ya makamishna wa Tume hiyo ambapo Naibu Mwenyekiti na wajumbe wengine 3 wamegima kuyatambua matokeo yaliyotangazwa na Mwenyekiti Chebukati.

Naibu Rais, Mheshimiwa William Ruto alitangazwa Rais Mteule na tume hiyo ya UchaguziView attachment 2325908
Fake news, hili gazeti la kutengenezwa kama wanavyofanya kutengeneza gazeti fake la mwananchi

Nilishasema wafuasi wa Magufuli vichwa maji sana
 
Marekani wLikuwa wanataka Raila ashinde sasa hii ya interpol ni sehemu ya mikakati hiyo sio coincidence. Tutasikia mengi ili mradi mtu wao ameshindwa uchaguzi. Hao intepol tangu lini wamekuwa wakitoa taarifa za rushwa zinazohusu viongozi? Mbona huku Tanzania ambako rushwa inaliwa waziwazi lakini gawajahi kutoa taarifa kuhusu vigogo wa rushwa wa miktaba na manunuzi makubwa.
Hilo gazeti la The Star wamekanusha hiyo sio habari yao, ni wahuni wametengeneza gazeti fake
 
Fake news, hili gazeti la kutengenezwa kama wanavyofanya kutengeneza gazeti fake la mwananchi

Nilishasema wafuasi wa Magufuli vichwa maji sana
Marehemu anakukosesha usingizi.
Bado kuokota makopo tu sasa
 
Watu wengine kumbe hawafuatilii mambo.Hiyo kampuni inayolalamikiwa Inahusishwa na Moja ya watu walioko kwenye Azimio la Kenya kwanza,Akina Raila walishalalamika sana juu ya Hilo wakamtaka mwenyekiti wa tume ajiuzuru akagoma na Moja ya watu walikuwa wakimkingia kifua ni Ruto.Kimsingi Kuna mengi sana nyuma pazia.Sisi watanzania ni watazamaji tu.Mwisho tutampokea yeyeto atakaye kubaliwa.
 
We akili zako zimeishia wapi? Usikute umeamini hilo gazeti ukamsimulia na baba yako....
NI mara.chache sana kuamini yanayoandikwa humu JF, nitachangia lakini mwisho ya yote nayaacha humu humu kisa cha kisutwa.maana chai ni nyingi kuliko uhalisia
 
Hizo $ ni mali ya USA na wahongaji ni USA wenyewe, kwa nini hawajakamatwa?

Babu Trump alilalamika pia ila mlipotezea, interpol ya sasa ni vishoia wa viwango vya juu kabisa 😂
 
Back
Top Bottom