Interview and employability; Usipozingatia haya, utaishia ku-apply kazi bila kuitwa kwenye interview

Interview and employability; Usipozingatia haya, utaishia ku-apply kazi bila kuitwa kwenye interview

USIPOZINGATIA HAYA, UTAISHIA KU-APPLY KAZI BILA KUITWA KWENYE INTERVIEW

Vijana wengi sana Wahitimu wa vyuo wamejikuta katika janga la kuishia ku-apply kazi bila kuitwa kwenye Interview. Kwa miaka kadhaa nimekuwa kwenye Managerial Level katika taasisi ninazofanyia kazi. Na katika recruitments kashaa nilizozifanya kuajiri, nimekutana na changamoto nyingi sana kwenye applications za kazi zinazowafanya watu wengi kutokuwa shortlisted kuitwa kwenye Interview.

Tuko katika ulimwengu wa Utandawazi ambapo mfumo wa kuomba kazi Serikalini, Taasisi mbalimbali, na Sekta binafsi ni kwa njia ya Online (Online Job Application). Nimebaini Graduates wengi hawana Job Application & Employability Skills kuwawezesha kuwa shortlisted tu. Na shida kuwa nadhani ipo kwenye mfumo wetu wa Elimu ambapo hauendani na mahitaji ya sasa, kumfanya mtu ahitimu masomo akiwa na uwezo na maarifa flani ya ziada ya kumsaidia.

Sasa Leo, nitagusia vituvichache tu ambavyo watu wengi wamekuwa hawavizingatii pindi wanapoomba kazi Online. Kazi yoyote ile ambayo Application yake ni Online (kama vile kutuma kwa njia ya barua pepe), Interview ya kazi inaanzia;

1. How you arranged your CV
2. How you drafted your Application/Cover Letter
3. How do you send your Application

1. Application Letter - Application yoyote ya kazi, Application /Cover Letter ni muhimu, hata usipoambiwa utume. Labda kama itakuwa imeelekezwa vingine.

2. Unapotuma Application kwa njia ya Email (barua pepe)
(a). Letter Heading - Kwenye barua lazima utaje exactly position unayoomba kama ilivyoelekezwa kwenye tangazo la kazi. Maana wakati mwingine Taasisi au kampuni hiyo wanaweza kuwa wametangaza nafasi za kazi za position tofauti tofauti.
(b). Kwenye Email Subject: You have to mention exactly the position unayoomba kama ilivyoelekezwa kwenye tangazo la kazi na inatakiwa kuandikwa kwa herufi KUBWA - APPLICATION FOR CALL CENTER AGENT.
(c). Documents zako (CV & Letter) attachment zinatakiwa kuwa na Majina yako - Kongwa Dodoma Tanzania
(d).Kwenye email body, lazima uandike chochote, not just sending it plain. Mfano:

Hi Sir/Madam;

As per the subject, Kindly receive the attached CV and application later for your perusal/reference.

Thank You.

3. Kwa ujumla, wengi wanakosa kazi kwa kutozingatia hivo vitu muhimusana. Yafuatayo ni moja ya hayo mambo yatakayokufanya application yako itupiliwe mbali, na hutakaa uje kuitwa kwenye interview kama hutoyazingatia.

(a). Kutuma Application kwa ku-forward email
(b). Kutoandika subject kwenye email yako
(c). Kusahau ku attach relevant documents kama ilivyoelekezwa kwenye tangazo la kazi
(d). Ku resend Email Application mbapo unakuta ulisahauku. Kama ulisahau ku attach documents, ni bora kutuma email mpya

NOTE: Kutokana na janga la ukosefu wa ajira, waajiri huwa wanapokea applications nyingi sana kiasi kwamba sio rahisi wakapitia applications zote katika zoezi la shortlisting. Hivyo, njia pekee wanayoitumia ni kutufa applications zote ambazo hazijazingatia professional application format na kubakiza zile ambazo ziko in good format, ndipo sasa waanze kuchambua nani ana sifa tunazozitaka.

Hivyo, unaweza kukuta una sifa zinazotakiwa, lakini kwakuwa hukufuata a professional appliaction format, application yako inatupiliwa mbali na unakosa kazi ambayo huenda wewe ndio ulikuwa candidate sahihi unayetakiwa.

Ni hayo tu kwa Leo. By professional I Am not an HR, hivyo I stand to be corrected na kuruhusu professionals wengine kuongeza mchango wako katika haya machache niliyoyagusia.

Asanteni sana.
ikitokea umeandika maelezo mengi bila kuwa straight to the point on "KWANINI WAKUAJIRI WEWE" utajikuta hauitwi na wenzako wanaitwa kwenye interview. Siku hizi kuna idadi kubwa sana ya wahitimu walio na vigezo kama vyako. Utofauti utakuja pale mwenzako atakavyoeleza namna ambavyo ukiachana na alichosomea yeye ana skills mbalimbali ambazo ataisaidia kampuni wakimpa nafasi.
 
Nimefaya yote uliyosema kwa usahihi. Nimetuma barua zaidi ya 500, feedback chache Ninazopata, paragraph ya pili inaanza na neno UNFORTUNATELY 😭
We regret to inform you that we will not advance with your application into next process. Keep your eye into our website...... kiufupi brother amegusa Engo muhimu but sisi watafuta kazi tume qualify vizuri tu. Kampuni nyingi zinafanya formality tu kwamba tuonekane tumetangaza as required by law and regulations of employment and labour laws but wengi sio wote wanakua tayari wana mtu anavolunteer ama yuko intern ama internal memo ila sio mbaya njia sahihi ya kupata kazi ni ku apply kazi pindi tangazo linapotoka megine tuwaachie wao waamue. OUTSIDE STRUGGLE IS VERY REAL. Tuendelee kupambana.
 
Huyu Sewando MP ndo yule wa kule Mzee wa Full mayoko Nachingwea au? [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
ikitokea umeandika maelezo mengi bila kuwa straight to the point on "KWANINI WAKUAJIRI WEWE" utajikuta hauitwi na wenzako wanaitwa kwenye interview. Siku hizi kuna idadi kubwa sana ya wahitimu walio na vigezo kama vyako. Utofauti utakuja pale mwenzako atakavyoeleza namna ambavyo ukiachana na alichosomea yeye ana skills mbalimbali ambazo ataisaidia kampuni wakimpa nafasi.
Nakubali Nakubali MC Shonde
 
Cover letter ndo application letter......hebu dondosha sample ya cover letter ya kada ya udereva.
 
Hapo kwenye ulazima wa kutuma BARUA hata kama wamesema tuma CV tu sidhani kama utakuwa sahihi?

Kuna wengine wanasema tuma CV, basi!!!

Halafu wewe uweke barua ni sahihi?
 
Kwa uzoefu wangu, kuweka picha sikushauri sana.
World CV hiyo mkuu.

Picha haina shida kama format inakubali weka.

Nishaitwa sehemu mbili kubwa kufanya interview na cv yangu ina picha.
 
Waambie watu ukweli, usiwadanganye kwamba shida ni CV.

Mtu anaambiwa haina shida we jumatano uripoti kazini usisahau kunitumia vyeti vyako kwenye email
 
Back
Top Bottom