Interview ya Ommy Dimpoz: Bifu lake na Diamond, hastahili lawama

Interview ya Ommy Dimpoz: Bifu lake na Diamond, hastahili lawama

Ulisikia ile kashfa ya gazetini kwamba jamaa anamlala mama yake kila jumatano ili asishuke kimziki?kashfa kubwa sana kwa D
Hadi kuna wimbo kaimbiwa unaitwa Bongo flavour tafuta mtu anaaitwa Kapuku digital instagram utaupata wimbo unaozungumzia hiyo kashfa
 
Hilo Ni bifu jipya mujini waache waendelee tutajua baadae nani mgomvi.
 
D kaulizwa na ndio maana akawa anawaelekeza so hajalalamika n akiwajibu maswali yalokua vichwan mwa watu.
 
Nimesikiliza vizuri interview ya Ommy...swala ni kwamba yeye alimchukulia Diamond kama mshikaji na akataka kila anachofanya Dee na yeye akijue au ashirikishwe, jambo ambalo Dee hakulitaka. Dee aliona kama Ommy anataka sana kujua kazi yake so akawa kama anamkwepa na hivi ashakua msanii mkubwa..kwahyo na kiburi kikaongezeka!
Ommy alichoongea kiko vizuri kabisa.. Riziki anatoa Mungu na yeye hashindani na Dee kabisaa...sema Dee anaonekana hapendi mtu yoyote ampite kwa chochote..na ana tamaa! Kila kizuri anataka kiwe chake..

Ommy kasema Kiba alikua mshikaji wake tangu mwanzo...na sio kwamba kisa haongei na Dee ndo amekua upande wa Kiba! Na kasema akikaaga na Kiba hizo habari za Dee hawaongei kabisaa...maana hata Kiba mwenyewe sio mzungumzaji kabisaa..

Anachoshangaa zaidi ni vile watu wanavyomuona Dee kama mungu mtu, kwamba yeye Ommy ndo ajishushe yaishee..badala waseme au wapange wakutanishwe wote sehemu ( kasema hata kwa AY) waongee yaishe! Yeye kasema hana shida..ana love ya kutosha kwa Dee na anaheshimu mchango wake!

Sehemu iliyonigusa...ni vile Ommy alivyosema..hadi siku Dee ananunua pikipiki yake ya kwanza ( kipindi huko Dee ndo anatoka kimziki) ..wanapakizana wote, wakifika sehemu za makorongo anashuka..then mshikaji chombo... Af leo huyo mtu anakwambia unapumuliwa!!! Ila Dee uswahili umemzidi..anatakiwa abadilike!! Yote mapito tu...walikuwepo akina R.Kelly enzi hizooo...leo kimyaaaa, haya maisha tu!
 
Mie ningekuwa naendesha talk show kwa Tv au radio hizi beef za Diamond na Kiba/Ommy/Jide na Ruge ningezitumia kutengeneza pesa na brand kubwa sana.You know smart people use fool people to make money.
 
kumbe ommy ana akili zake timamu nadhani sababu ya kukaa na watu wenye busara na maono ya mbali kama AY,sasa huyu ndugu yetu anashinda na kaka zake raisi wa manzese wao wanawaza majungu tu ndomana kuna show walipigwa makopo..!!kinacho mwangusha bwana D ni ile crew ya mameneja ilio mzunguka
HASA SALLAM
 
Ommy Dimpoz alianza kuwa mbali na Diamond baada ya kuamua kuwa karibu sana na Ali Kiba.

Kuna uwezekano akapotea kabisa katika game kutokana na kujiingiza katika upande wa teams.

Mtu mwingine ambaye yupo katika hati hati ni Baraka da Prince.

Ngoja tuone
Ommy yuko close na Ally kitambo tangu colabo ya Nainai aliyomshirikisha Ali.
Tena anakuambia kipindi anafatilia hiyo nyimbo alikua hana usafiri diamond akawa anampeleka studio kwa gari yake kufatilia hiyo nyimbo.
 
Sure. Ameongea safi sn, ila kma ni kweli anayoyaongea, kwa sababu tumesikia upande mmoja wa story, basi Diamond atakuw na matatizo. I'm not judging, thats why nasema "kama ni kweli".
Dmomd si ndio alianza jana? Katoa povu hadi la Omy kumuomba amle nyuma yeye Dmond akagoma
 
Sikuwahi kumfikiria km anaweza kujieleza kuufasaha namna hii kweli Ommy umetulia km ni kweli unayoyasema mm nakutakia mafanikio mema Mungu akupe moyo huohuo wa uvumilivu Maana Rizki haizimwi ila inacheleweshwa tu!
 
Sallam hapa kamuingiza chaka, halafu Sall anaonekana ana akili za kitoto sana. Sja jua kina mkubwa fella wako wapi sku hizi.

Cloudz nao wamenunua hii bifu kwa manufaa yao, na wamemuingiza chaka diamond naye kaingia mzima mzima.

Cloudz ni washenzi kweli!!!
mmmmhhhh!Leo ....!!
 
Omi anatafta ngazi ya kuvukia. Na source ya yote ni blouz fm wao wasingemuuliza hayo maswali sidhan km mondi angejibu. Simpendi mtu mnafki kama omi.
Btw miss you
Ommy leo amewaweza mmebaki kimya.
Mbaya zaidi interview ya leo imesikilizwa na watu wengi zaidi hadi Magufuli nimemuona kavaa earphones anamsikiliza kijana mwenye busara pozi kwa pozi.
 
Nimejikuta tu inabidi nichangie hii thread hata kama sina cha kuandika, naona yote wadau wamemaliza.

Tatizo Bongo wasanii ni wachache, vituo vya redio na TV ni vile vile, utakuta kila mnapoenda mnakutana ovyo.

Kunatakiwa kuibuke kundi lingine au makundi zaidi ya management kuhakikisha kwamba kina D wanakuwa na ushindani kikazi, management hiyo iwe inaweza fitna za ndani, iwe na connections za nje etc.

D simlaumu sana, ila ninaamini kama yeye alivyo-struggle kujulikana nje na wengine nao wafanye hivyo ila wasilalamike eti jamaa kakataa kuwashika mkono.
 
Back
Top Bottom