Nimejikuta tu inabidi nichangie hii thread hata kama sina cha kuandika, naona yote wadau wamemaliza.
Tatizo Bongo wasanii ni wachache, vituo vya redio na TV ni vile vile, utakuta kila mnapoenda mnakutana ovyo.
Kunatakiwa kuibuke kundi lingine au makundi zaidi ya management kuhakikisha kwamba kina D wanakuwa na ushindani kikazi, management hiyo iwe inaweza fitna za ndani, iwe na connections za nje etc.
D simlaumu sana, ila ninaamini kama yeye alivyo-struggle kujulikana nje na wengine nao wafanye hivyo ila wasilalamike eti jamaa kakataa kuwashika mkono.