Nchi ngumu sana hii. In general ulimwengu voice
Yaani ndugu hapo naweza kusema kwamba serikali imetengeneza mianya ya rushwa kwa wasaili dhidi ya wasailiwa,
Pia imetengeneza matumizi mabaya ya fedha dhidi ya watafuta ridhiki Bora hata awali mtu alikuwa akituma maombi anabaki kusuburiyaani anaumizwa na pesa ya kwenda kutuma maombi kule steshenari na siyo huu mfumo wa usahili, Kuna watu wataishiaga kufanya usaili mara 50 bila kupata ajira,
Hivi kama siyo complications ni Nini imagine mtu amesoma chuo kipo chini ya udhibiti wa serikali, kapewa cheti na wataaalamu wa serikali yenyewe, Bado serikali hiyo hiyo inahitaji certification ya cheti hichohicho kwa mwanasheria, maanayake ni kwamba wanasheria hapo wametengenezewa mazingira ya kula, baaado mtu huyo huyo ataambiwa Hana vigezo vya kupata kazi husika alafu cheti anacho kama final qualification ya taaluma yake na cheti hicho alipewa na nani na alikipataje??...
Hivi kweli ndugu zangu mnaotuwekea mifumo hii nyie mliwekewa vizuizi hivi??
Vijana Wala hatujachoka kupambana,
Tuonee huruma vijana wa kitanzania ambao tulishapigwa na maisha, vijana ambao tulisomeshwa kwa kuuzwa Mali zote za familia tegemeo likiwa baada ya kusoma zitarejeshwa Mali zote lakini Leo hii wazazi na walezi mpaka nao wanakufa kwa njaa, wanakufa kwa presha, wanakufa kwa shida vijana wao hatuwasaidiii, ila Bado vigogo hamuoni, Wala hamjali, daah! Leo hii Kuna vijana wamejitolea zaidi ya miaka mitatu na Bado hamuoni
Yaani taasisi mbalimbali zimejaa graduates wanalipambania taifa lakini Bado vigogo hamuoni
Ikifika applications wanachomekwa wahuni eti nawao walikua wanajitolea ndo wanapita alafu wale wahusika wa kujitolea hakuna anaye waona, hivi mfumo wa serikali haujawahi kujua Wala kuliona hili? Wazalendo Hawa hamuwaoni kweli yaani mnahisi mzalendo ni mwanajeshitu?
Motisha yetu vijana ni Ipi sasa?
Siku tukiwa viongozi itakuaje sasa??
Twambieni bas sisi vijana pengine kama tunawakosea au tuliwakosea.
Au nyie wabunge mnaosema tujiajiri mtwambie labda wazazi wetu, walezi wetu maskini waliwakosea,,
Kwakweli vijana wa kitanzania wasomi wanatia huruma Sana wengi washapauka, washakata tamaa, wanaumwa preshaa, Wana madonda ya tumbo na siyo mfano wa kuigwa kwa wadogo zao mpaka hata kwenye jamiii, ndo maana vijana wengi kwa Sasa hawataki shule serikali imebaki kuitumia nguvu kulazimisha watoto kwenda shule kumbe shule ishapoteza mvuto na madhara yake hayawezi onekana Leo Ipo siku yataonekana
#Tanzania nchi yangu nakupenda kwa dhati Sana ilatu Kuna jinamizi anatugombanisha Mimi na wewe