Interview za afya na haki

Interview za afya na haki

lyajody

Senior Member
Joined
Aug 16, 2024
Posts
145
Reaction score
196
Kwanza niipongeze wizara husika Kwa hatua iliyochukuliwa ya kuwafanyisha usaili ..maana italeta haki Kwa watoto wasiokuwa na watu au connection za kuwaingiza kwenye system Yani ufaulu wako ndo utakaokusaidia
 
Watu wazito bado wapo na wanafanya connection hasa kwenye taasisi zenye maokoto ya maana.

Pia watu wazito washaacha kuwatafutia watoto wao kazi, hizo ni zilipendwa. Watu wazito wanawatafutia watoto wao nafasi nzito za kisiasa au kwenye Taasisi zenye pesa au wanawapa mtaji mkubwa(50m-1B+) wanafanya biashara za pesa ndefu.

Ndio maana siku hizi ni vigumu kuona mtoto wa mkubwa Anatafuta kazi. Ila inakuwa kinyume chake, kazi inamtafuta yeye.
 
Jidanganye!
Siku ukijua hapa duniani hakuna haki ndipo utakapo elewa ulichelewa sana
 
Siku zote Tamisemi connection na utumishi connection ni wachache sana wengi walioajiriwa Tamisemi ilikuwaga ni bahati tu maana wale jamaa walikuwa hawana vigezo Bali inategemea wameamka vipi siku hiyo, unaweza Kuta boss anakuambia safar hii tuchukue wa mwaka flani tu
 
Kwel kabisa mkuu, bora sasa hv kuna usaili kwa watu wote
 
Kwel kabisa mkuu, bora sasa hv kuna usaili kwa watu wote
Wanasema et connection haziwezi kukosekana ..et wengine tyr wameshapangiwa had vituo interview kama geresha tu bajeti ipitishwe watu wapate per Dm
 
Kwanza niipongeze wizara husika Kwa hatua iliyochukuliwa ya kuwafanyisha usaili ..maana italeta haki Kwa watoto wasiokuwa na watu au connection za kuwaingiza kwenye system Yani ufaulu wako ndo utakaokusaidia
Hapo rushwa Zitasikika kwelikweli, kama usaili wa watendaji wa vijiji watu hutoa rushwa je hii vipi? Serikali imejipanga? # Technical know whom and not technical know how.

Pili binafsi mim naona ni kuwaharibia nauli vijana jobless maana mtu anaenda kwenye usaili kajichanga kwelikweli anarudi hawezi kulipa madeni na pia kazi hapati

Maskini anaendelea kunyanganywa hata kile kidogo alichonacho, Wala hakuna anae jali

Mwenye kisu kikali ndiye atakae kula nyama
 
Umelala wapi wewe? Tanzania au Marekani, Sweden? Norway? Maana unayoyaandika ni kama hukai hapa? Haki itoke wa[pi? Au nawe ni mnufaika wa rushwa za interview
 
Umelala wapi wewe? Tanzania au Marekani, Sweden? Norway? Maana unayoyaandika ni kama hukai hapa? Haki itoke wa[pi? Au nawe ni mnufaika wa rushwa za interview
Nimeomba mara nyingi sana tamisemi sijawahi pata ndo natarajia kufanya interview nasikiaga utumishi hakuna rushwa mkuu
 
Haki,

1000012500.gif
 
Hapo rushwa Zitasikika kwelikweli, kama usaili wa watendaji wa vijiji watu hutoa rushwa je hii vipi? Serikali imejipanga? # Technical know whom and not technical know how.

Pili binafsi mim naona ni kuwaharibia nauli vijana jobless maana mtu anaenda kwenye usaili kajichanga kwelikweli anarudi hawezi kulipa madeni na pia kazi hapati

Maskini anaendelea kunyanganywa hata kile kidogo alichonacho, Wala hakuna anae jali

Mwenye kisu kikali ndiye atakae kula nyama
Nchi ngumu sana hii. In general ulimwengu voice
 
Nchi ngumu sana hii. In general ulimwengu voice
Yaani ndugu hapo naweza kusema kwamba serikali imetengeneza mianya ya rushwa kwa wasaili dhidi ya wasailiwa,

Pia imetengeneza matumizi mabaya ya fedha dhidi ya watafuta ridhiki Bora hata awali mtu alikuwa akituma maombi anabaki kusuburiyaani anaumizwa na pesa ya kwenda kutuma maombi kule steshenari na siyo huu mfumo wa usahili, Kuna watu wataishiaga kufanya usaili mara 50 bila kupata ajira,

Hivi kama siyo complications ni Nini imagine mtu amesoma chuo kipo chini ya udhibiti wa serikali, kapewa cheti na wataaalamu wa serikali yenyewe, Bado serikali hiyo hiyo inahitaji certification ya cheti hichohicho kwa mwanasheria, maanayake ni kwamba wanasheria hapo wametengenezewa mazingira ya kula, baaado mtu huyo huyo ataambiwa Hana vigezo vya kupata kazi husika alafu cheti anacho kama final qualification ya taaluma yake na cheti hicho alipewa na nani na alikipataje??...

Hivi kweli ndugu zangu mnaotuwekea mifumo hii nyie mliwekewa vizuizi hivi??

Vijana Wala hatujachoka kupambana,

Tuonee huruma vijana wa kitanzania ambao tulishapigwa na maisha, vijana ambao tulisomeshwa kwa kuuzwa Mali zote za familia tegemeo likiwa baada ya kusoma zitarejeshwa Mali zote lakini Leo hii wazazi na walezi mpaka nao wanakufa kwa njaa, wanakufa kwa presha, wanakufa kwa shida vijana wao hatuwasaidiii, ila Bado vigogo hamuoni, Wala hamjali, daah! Leo hii Kuna vijana wamejitolea zaidi ya miaka mitatu na Bado hamuoni
Yaani taasisi mbalimbali zimejaa graduates wanalipambania taifa lakini Bado vigogo hamuoni
Ikifika applications wanachomekwa wahuni eti nawao walikua wanajitolea ndo wanapita alafu wale wahusika wa kujitolea hakuna anaye waona, hivi mfumo wa serikali haujawahi kujua Wala kuliona hili? Wazalendo Hawa hamuwaoni kweli yaani mnahisi mzalendo ni mwanajeshitu?
Motisha yetu vijana ni Ipi sasa?

Siku tukiwa viongozi itakuaje sasa??

Twambieni bas sisi vijana pengine kama tunawakosea au tuliwakosea.

Au nyie wabunge mnaosema tujiajiri mtwambie labda wazazi wetu, walezi wetu maskini waliwakosea,,
Kwakweli vijana wa kitanzania wasomi wanatia huruma Sana wengi washapauka, washakata tamaa, wanaumwa preshaa, Wana madonda ya tumbo na siyo mfano wa kuigwa kwa wadogo zao mpaka hata kwenye jamiii, ndo maana vijana wengi kwa Sasa hawataki shule serikali imebaki kuitumia nguvu kulazimisha watoto kwenda shule kumbe shule ishapoteza mvuto na madhara yake hayawezi onekana Leo Ipo siku yataonekana

#Tanzania nchi yangu nakupenda kwa dhati Sana ilatu Kuna jinamizi anatugombanisha Mimi na wewe
 
Back
Top Bottom