IOC na ANOCA Zamtambua Anthony Mtaka kama Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC)

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,776
Reaction score
42,933
Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) na Chama cha Kamati za Olimpiki Afrika (ANOCA) zimemtambua rasmi Anthony Mtaka kuwa Rais mpya wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), baada ya uchaguzi uliofanyika Julai 5, 2026 katika Hoteli ya Peacock, Dar es Salaam.

Katika barua yao ya Julai 9, 2026 kutoka Lausanne, Uswisi, IOC na ANOCA zimesema zimepokea na kuridhia matokeo ya uchaguzi huo, ambapo Mtaka alipata kura 29 kati ya 36. Pia zimempongeza Makamu wa Rais, Nassra Juma Muhammed, pamoja na wajumbe wapya wa Kamati ya Utendaji.

Hata hivyo, IOC na ANOCA zimelaani taarifa za jaribio la dakika za mwisho la Tume ya Uchaguzi ya TOC kudaiwa kutaka kupindisha matokeo ya nafasi ya Rais kwa kumtangaza mgombea ambaye hakuchaguliwa.

Zimeutaka uongozi mpya kuchunguza suala hilo na kuchukua hatua stahiki, ikiwemo adhabu kwa wahusika, ili kulinda heshima ya Olimpiki Tanzania. Pia zimeutaka uongozi uliopita kukabidhi mali, nyaraka na akaunti zote za TOC mara moja.

Soma Pia: Paul Christian, Makonda amesimamisha Uchaguzi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) na kuusimamisha Uongozi wa sasa wa Kamati hiyo

Wajumbe wapya wa Kamati ya Utendaji ya Kamati ya Olimpiki Tanzania ni Abdulrahman Said Simai, Makame Ally Machano, Thuwaiba Aboud Muhiddin, Mwatima Bakari Abdi, Noorain Gulam Hussein Shariff, Amina Mohamed Mfaume, Khalid Yahya Rushaka, Suma Steven Mwaitenda, Abdulkheir Ahmed Mohammed na Said Mohamed Abdullah.

Kwa mujibu wa barua hiyo, tukio la madai ya kupindisha matokeo lilikwenda kinyume na makubaliano kati ya IOC, TOC na mamlaka husika kuhakikisha uchaguzi huru, wa haki na wa kidemokrasia.

IOC na ANOCA zimeutaka uongozi mpya kuchunguza suala hilo, kuchukua hatua dhidi ya wahusika, na kuhakikisha uongozi uliopita unakabidhi mali, nyaraka na akaunti zote za TOC.
 
IOC imeutambua uongozi unaomwongoza Anthony Mtaka kama Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) baada ya kupitia mgogoro uliotokana na uchaguzi.

Taarifa ni kuwa IOC imekubali matokeo yanayompa Mtaka uhalali wa kuongoza TOC, tofauti na hali ya awali ambapo Leonard Thadeo alikuwa ametangazwa na kuapishwa huku suala hilo likiwa bado linachunguzwa

MY TAKE

Samia kafanya watu waone kuiba kura au kunyang'anya watu ushindi ni jambo la kawaida.

Samia kanajisi Tanzania..

Kwanini Mtaka alintang'anywa ushindi? Aibu kwa CCM

=====

The letter confirms that the IOC and ANOCA have accepted the election results from the TOC General Assembly held on July 5 at Peacock Hotel in Dar es Salaam, recognising Mtaka as president after receiving 29 of the 36 votes cast.

The international Olympic bodies also recognised Nassra Juma Muhammed as vice president together with the newly elected Executive Committee members, saying they look forward to working with the new leadership and resuming normal cooperation with the TOC for the benefit of athletes and the Olympic Movement in Tanzania
 
Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) na Chama cha Kamati za Olimpiki Afrika (ANOCA) zimemtambua rasmi Anthony Mtaka kuwa Rais mpya wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), baada ya uchaguzi uliofanyika Julai 5, 2026 katika Hoteli ya Peacock, Dar es Salaam.

Katika barua yao ya Julai 9, 2026 kutoka Lausanne, Uswisi, IOC na ANOCA zimesema zimepokea na kuridhia matokeo ya uchaguzi huo, ambapo Mtaka alipata kura 29 kati ya 36. Pia zimempongeza Makamu wa Rais, Nassra Juma Muhammed, pamoja na wajumbe wapya wa Kamati ya Utendaji.

Hata hivyo, IOC na ANOCA zimelaani taarifa za jaribio la dakika za mwisho la Tume ya Uchaguzi ya TOC kudaiwa kutaka kupindisha matokeo ya nafasi ya Rais kwa kumtangaza mgombea ambaye hakuchaguliwa.

Zimeutaka uongozi mpya kuchunguza suala hilo na kuchukua hatua stahiki, ikiwemo adhabu kwa wahusika, ili kulinda heshima ya Olimpiki Tanzania. Pia zimeutaka uongozi uliopita kukabidhi mali, nyaraka na akaunti zote za TOC mara moja.

Soma Pia: Paul Christian, Makonda amesimamisha Uchaguzi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) na kuusimamisha Uongozi wa sasa wa Kamati hiyo

Wajumbe wapya wa Kamati ya Utendaji ya Kamati ya Olimpiki Tanzania ni Abdulrahman Said Simai, Makame Ally Machano, Thuwaiba Aboud Muhiddin, Mwatima Bakari Abdi, Noorain Gulam Hussein Shariff, Amina Mohamed Mfaume, Khalid Yahya Rushaka, Suma Steven Mwaitenda, Abdulkheir Ahmed Mohammed na Said Mohamed Abdullah.

Kwa mujibu wa barua hiyo, tukio la madai ya kupindisha matokeo lilikwenda kinyume na makubaliano kati ya IOC, TOC na mamlaka husika kuhakikisha uchaguzi huru, wa haki na wa kidemokrasia.

IOC na ANOCA zimeutaka uongozi mpya kuchunguza suala hilo, kuchukua hatua dhidi ya wahusika, na kuhakikisha uongozi uliopita unakabidhi mali, nyaraka na akaunti zote za TOC.
Wajumbe kama wote ni wazanzibar
 
Amang'ana gasarikile
Ndugu yangu hawa watu wenye mahusiano na CCM kuiba au kufanya mizengwe ni jadi yao. Sasa fikiria wizara husika ni ya Habari yenye Waziri Bashite unategemea nini? huyo Bashite anahisi anaweza kufanya lolote nchi hii maana kuna XYZ ya mtu mashuhuri kesha ishusha mtamwambia nini?
Atahahakisha mtu makini yeyote anamshusha na kuwapandisha VILAZA wenzie.
Ngoja niishie hapo
 
Back
Top Bottom