Ndugu zangu Watanzania,
Soma hapa 👉Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) na Chama cha Kamati za Olimpiki Afrika (ANOCA) zimetangaza kumtambua rasmi Antony Mtaka kuwa Rais mpya wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kufuatia uchaguzi uliofanyika Julai 05.2026, Peacock Hotel, Jijini Dar es Salaam, uchaguzi ambao uligubikwa na sekeseke na sintofahamu ya aina yake iliyozua mjadala mkali ndani na nje ya mipaka ya Tanzania
Barua ya pamoja iliyotolewa na IOC na ANOCA Julai 09.2026 kutoka Laussane, Uswisi, Vyombo hivyo vya Olimpiki vya Kimataifa vimeeleza kuwa vimepokea na kuridhia matokeo ya uchaguzi huo, ambapo kupitia taarifa hiyo vyombo hivyo vimeeleza kuwa Mtaka ambaye wengi hapa Nchini wanamfahamu kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe amepata kura 29 kati ya 36 hivyo kutuma salamu za pongezi kwake, pongezi zilizoelekezwa pia kwa Makamu wa Rais mpya wa TOC Nassra Juma Muhammed, pamoja na Wajumbe wapya wa Kamati ya Utendaji
Kupitia taarifa hiyo ya pamoja, IOC na ANOCA zimelaani vikali kile ilichokiita kuwa ni taarifa za jaribio la dakika za mwisho la Tume ya Uchaguzi ya TOC kudaiwa kutaka kupindisha matokeo ya nafasi ya Rais kwa kumtangaza mgombea ambaye hakuchaguliwa
Kufuatia sakata hilo, IOC na ANOCA vimeuagiza uongozi mpya wa TOC chini ya Rais mpya Antony Mtaka kuchunguza kwa kina sakata hilo, kuchukua hatua dhidi ya wote waliohusika, sambamba na kuhakikisha uongozi uliomaliza muda wake unakabidhi mali, nyaraka na account zote za TOC.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania Wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.