Sidhani kama issue ni Kodi,nadhani kuna shida mahali.
Me nnachoona hawa wafanyabiashara wamepata upenyo wa kutupiga kwakua iPhone hawana official store zao kwenye nchi yetu lakini kama zingekuepo bhas hizo Bei zisingekua mkasi hvyo.
Nakumbuka kipindi cha nyuma kidogo Simu za Xiaomi zilikua Bei mkasi kweli Bongo,unakuta Bei inazidi mpaka laki 3 ya Bei halisi ya Simu. Mfano Mimi nakumbuka niliagizaga Mi 9t Kwa laki 7 kama na Nusu hivi ,lakini Bongo Simu hyohyo ilikua inauzwa laki 9 mpaka milioni. Lakini baada ya Tigo na kampuni nyingine kuanza kuleta Simu za Xiaomi Bongo Bei hazitofautiani Sana na za mtandaoni.
Sasa kama iPhone unakuta pro Max ya 256gb huko mbele wanauziwa 3.5m huku Bongo unapigwa 4.8m-5m