Tabia hii Kwani Apple Hawana? Unakumbuka Kuhusu msimamo wa Apple na simu kubwa?
Na hili ni jambo la kupingwa na sio kuwa proud nalo, kwa jicho lolote ukiangalia loser ni mtumiaji.
mimi napenda kutumia iphone, na nilikuwa napenda Steve Jobs anapoipeleka iPhone, alikuwa anatizama zaidi usability kuliko trends. Iphone ilikuwa ni simu ya kutumia kwa mkono mmoja tu, ila saivi utumie yote miwili. Ila huyu Tim mapishi nimeona ni mtu ambae anataka kufuata trends lakini at the same time anataka kujitofautisha. Alipochukua nafasi yeye, nilijua tu kuwa jamaa ataingia kwenye screen kubwa. Halafu alipoanza kuja na variants of iphones ndio nikashindwa kumuelewa. STeve jobs katuzoesha simu moja kila mwaka, sio tatu mpaka nne kila mwaka.
Alivoleta design ya Notch, walipondwa sana tena, na mpaka Samsung akatoa ad kabisa. Mimi nilibaki nacheka tu, nikijua kwa 100% na wao watafuata tu. Si uongo, wakaja na za kwao, ila sasa mara zinaitwa tear drop instead of notch, mbaya zaidi practicality yake haieleweki. Kwa apple naweza kusema kuwa jamaa wametaka kulazimisha sensors za face id zikae mbele at the same time kupunguza bezels iliwalazimu wa sacrifice hio screen, sasa hawa akina Samsung/xiaomi na wengine wameweka nini wao zaidi ya camera?
Nafikiri i am safe nikisema kuwa Apple anawatia wenzake chaka na kudumaza creativity kwenye smartphones. Sasa ivi nothing is new or interesting kwenye smartphones, all come in same shape different sizes tu. Tunasifiwa benchmarks tu. kila keynote utasikia zinasifiwa internals tu. Zamani ukiflip motorola yako unajiona genius!
Wote watafuata hio trend ya kuuza simu bila charger kwa nyimbo ya kutunza mazingira, at the same time, hizo charge zinatengezwa na kuuzwa separately!