iPhone ni kama gereza la kifahari. Ni kwajili ya fasheni tu, hutaweza kufanya vitu muhimu vifuatavyo...

Iooo namba 13 nielekeze mkuuu

Ni kama facebook vile, wote tunatumia facebook ila kila moja ana username yake na password.

Sasa hii uzuri wake ni kwamba unaweza kumwazima mtu simu yako aitumie hata siku nzima bila yeye kuchokonoa kitu chochote kwenye user unayotumia, Hata kwa watoto pia unaweza kumwazima alale nayo kabisa bila wewe kuhofia kwamba atavuruga chochote
 
kwahiyo unanifokea nakapenda kaiphone kangu hivhiv😂😂😂kina matundu matatu
 
Kule jukwaa la siasa naonaga wakikomenti hivi

"Tulia dawa ikuingie"😂
 
1. Hutaweza kusikiliza radio bila bando
Radio kwenye smartphone mambo ya kale.

3. Hakuna tundu la kuingiza earphone, hapa hadi ununue vifaa vya ziada, huku android ukinunua ear phonr unaitumia hapo hapo
Zungumzia akina Tecno. walishikilia mpini wa Android ndipo wanapoelekea uko. Wireless earphones. Na hili nalo unalalamika mambo ya kale 😀

3. Andaa laini moja tu, kuna matoleo machache sana yenye laini 2.
Mchina ndio kawazoesha kutumia laini 600 kwa simu moja. Hii sio feature ya android. Ilikuwepo kabla ya android kwenye miche ya sabuni za wachina ilokosa majina enzi izo.

4. Kudownload nyimbo hata humu jamiifroums ama mtandaoni ni ishu nzito
Hujui tu kudownload nyimbo kwa kutumia iphone. wenye kuijua iphone hilo ni jambo jepesi kwa kweli.

5. Kuhamisha vitu kutoka kwenye simu kwenda kwenye pc ni shughuli pevu
Vitu gani ivo? Kikubwa unahamisha picha na video. Na vyote rahisi sana, copy paste tu. Muhimu uwe na itunes software kwa ajili ya kudetect iphone.

7. Non restricted access ipo kwa android kwa sababu unaweza ku root ukafanya vingi vya ziada, Kwa iphone hapa ni mtihani inabidi uwe mvumilivu.
Ipo kwa iphone, inaitwa Jailbreak.

8. Kwenye android unaweza kutumia simu kama remote kwa vifaa kama samsung, lg ,n.k....huko kwa apple so rahisi labda kwa tv zao za apple tv
Ushamba tu. Remote ya TV nnayo tena nitumie simu niimalize chaji ya nini? Sio sifa ya kumshawishi mtu kutumia apple wala android kabisa!

10. Kwenye i phone ku customize vitu kuna vikwazo, mfano ringtone utachagua tu wanazotaka wao iphone na inakuwa sekunde 30 tu, huku android ringtone uutaweka hata ya kingwendu ni wewe
Mambo ya zamani haya kuweka ringtone miziki sijui mtoto anacheka. Lakini hata ivo, ukijailbreak tu, unaweza kufanya ivo.

11. kitaa cha notification hakipo kwenye iphone, mfani message ikiingia kama simu ipo silent huku android kataa kanawaka.
Hii nalo ni muhimu la kusifiwa? ukiamka asubuhi bila kutizama kama kuna kitaa kwenye android yako unakamata simu kutizama kuna nini. Huhitaji taa ya notification, automatic tu wewe mwenyewe tayari technology imeshakufanya uwe unacheki simu yako mara kwa mara.

12. hutaweza kuseti default app, utaweza kudownload app mbadala ya kufungua mafaili lakini hutaweza kuiseti iwe ya moja kwa moja, kika ukifungua faili litafunguliwa na app ya mwanzoni
hapa bado sijashawishika, As long as other options are available.

Hii hakuna kweli katika iphone. Your phone is your personal device. Unaficha nini kwa mtoto mdogo asieelewa kitu zaidi ya kutizama katuni 😀
Na kwa android, wala huhitaji kuwa na 2 users kuficha mambo yako. nafikiri kuna apps unaweka password tu kwa kila app. iphone lengo lake iwe yako tu, sio kushare share.

14. Huwezi kufanya vitu vingi kwa mpigo (multi tasking )kwenye iphone, Huku android unaweza ukawa unaandika post huku jamii forums ukarudi kwenye kubadili muziki na ukarudi jamiiforums bila kuanza upya
Hapa labda uzungumzia multi tasking ya ku run apps simultaneous, sio ivo ulivosema. Mana unaweza kuandika post ukaruka kuchange music na ukirudi basi unaendelea pale pale.

In short mambo yote uliyoyataja hapo hayana umuhimu
 
Povu la omo hili 😁😁

Umekuja kutetea iphone wakati hata huna, Au ili tu uonekane una uchungu nayo watu wajue unayo😁😁

Wenye i phone wamekaa kimya.
 
kumbe kusoma hujamaliza halafu unakimbilia kusema mtu katoa omo 😀

Namiliki simu gani basi?

By the way unajua Jailbreak lakini? maana kwa post yako ulichoandika, inaonekana hujui kitu kuhusu iphone.
 
Instagram kwenye ANDROID ina GB 23 au zaid kidogo. Ila kwenye mnyama IOS ina GB 99.

I love you my-
One plus 8 T pro
 
Mimi shazoea wereva yangu na Samsung hata Kama na hela ya iPhone
 
Misaada hiyo namba 13
Natumia Redmi note 8
 
Pamoja na mapungufu yote hayo zinashindana na android phones zote combined
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…