Uwe unasoma nakuelewa basi, Nilisema huku android kampuni nyingi za simu kuanzia flagship hadi za chini zinatumia os ya android kutengeneza simu zao na hii inaleta ushindani kwamba moja akiringa kutunyima kitu flani basi wateja tunahama, mfano samsung akibana tundu la earphone tunaweza kwenda kwa sony, nokia, huawei, motorola, n.k. Huko ios ni apple tu anaetengeneza simu, Mkibanwa kitu flani inabidi mufyate tu mkia hakuna namna, mfano laini 2 apple kaanza kuweka majuzi tu hapo, kabla ya hapo ailimlazimu mmiliki wa i phone kuwa na simu ya ziada.
Mkuu unavyosema ki Tecno utadhani una hela wakati ulianzisha threas humu kulalamika umeombwa buku ya luku na nyingine eti ukipata hela utawakomoa maninti [emoji16][emoji16].
Tafuta pesa mkuu hizo simu za i Phone zimekaa kwa status zaidi kuliko feautures, Ni kama pamba za Gucci kule hata pochi milioni 10 zipo na watu wananunua kwasababu Gucci imekaa kwa status ya kitajiri flani ivi.
Nachokushauri nunua hicho ki Tecno ulichosema uza iPhone maana tabia ya kutuanzishia nyuzi humu za kulalamika kuombwa buku ni vibaya.