Ipi gari ya kuchukua? Toyota RunX / Allex, IST, Spacio, Raum,Carina

CARINA TI aiseee.nlinunua kwa mtu mwaka 2011 namba A hadi leo inadunda balaa..haina tatizo lolote na moshi arusha ninaenda kila napojisikia
 
Carina Ti utapakiza watu 5 na mzigo wa kutosha na ina cc 1500.
IST utapakiza watu 4 na mzigo kiasi cc 1300.
Spacio inabeba watu 5 kwa kujibana na mzigo mkubwa kiasi kuliko IST ila engine size 1800cc.
Runx/Allex ina inabeba watu 5 kwa kujibana, mzigo kiasi kama ist na cc1500.
Raum watu 4 mzigo mkubwa kiasi kama spacio na cc 1500.

Hapo piga mahesabu yako crossmultiplication upate gari unayoitaka. Zote gari nzuri.
Kwa ushauri wangu carina Ti is the car to go with kama una familia na utaifanyia baishara ya teksi ikiwa utapata gari nyingine badala ya kuiuza.
 
Mkuu kwenye spacio hapo sio kweli kwa spacio new model zinabeba watu saba tena sio kwa kujibana na zipo za cc1490 to cc1500 na izo za cc1780 to cc1800
 
Jamani kuna mtu ashawahi kuagiza gari kupitia hawa jamaa wa CARJUNCTION?
 
Angekuwa anataka gari ya kubeba abiria wengi angesema na angekuwa anataka gari ya kubeba mizigo angesema,hiyo Carina ti sio gari nzuri haukai comfortable unakuwa kama umechuchumaa,na hapo uliposema spacio zina cc 1800 umeteleza spacio nyingi zinatumia 1NZ-FE engine chache sana zinazotumia 1ZZ-FE lete visingizio vingine
 
Duuuu list yako ndefu, bora utoe aina mbili
Anyway kura nyingi zimekwenda kwa Carina Ti
 
Aisee i beg you nina experience na hii gari usichukue but take carina ti angalia hata comments za watu wengi hapo juu waliyoyasema ni sahihi kabisa
Vvti imetulia sana katika mafuta, wengi wakisikia Gx 100 wanawaza 1g ambayo ni kweli inakunywa, ninazo zote mbili gx na Carina na sioni utofauti katika wese.
 
mkuu kwa umeshauri runx na sio allex?
 
Nimecheka saana. Teh teh teh teh teh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…