Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata usione aibu mkuu, channel uzipendazo ziko bomba sana tu.Mmh huu Uzi naona wengi mpo duniani huko..naona hata aibu kuweka zangu[emoji23][emoji23]
Enwei...za kwangu
Obaapakua skinny(channel ya namna ya kutengeneza vipodozi na nimejifunza mengi mno..huyu mama angekua tz ningempelekea zawadi[emoji4])
Aroma talks(nayo Ni diy channel kwa ajili ya kutengeneza vipodozi vile wanasema organics)
Roberta gym(channel ya mazoezi ..na ukifuatilia mazoezi yao lazima upate matokeo chanya)
Chloe thing (sisi wenye vitambi anatusaudia sana)
Susana yabar (channel ya mazoezi)
Ivonmelda( kwenye hii channel kila siku Nina kipya najifunza..anadeal na utengenezaji wigs na ufungaji vilemba vya Nigeria)[emoji7]
Gemmakitchen (channel ya mama wa kizungu..anatengeneza keki za Aina zote.. ice cream vitu vitam tam vyote viko pale)
Holy Spirit connect( channel yenye kuelezea neno la Mungu na huwa nafuatilia maombi ..imenisaidia mno)
Pastor Rose shaboka jr (channel ya neno la Mungu..nayo kwangu ni msaada mkubwa sana
Rukias kitchen(channel ya mapishi..najifunzaga vingi wallah..)
Aroma of Zanzibar( channel ya mapishi)
Mapishi rahisi ( nayo ni channel ya mapishi[emoji39])
Natural herbs( channel yenye kuzungumzia Mambo ya Tiba asili..Yani namna ya kutumia spice kujitibu na magonjwa)
Rose Sharon (channel yenye kutoa mafunzo ya makeup na nimejifunza vitu vingi kwa huyu dada[emoji7] mkenya)
Kuti bari (channel ya kaka wa kihindi ..anafundisha namna ya kutengeneza vifaa ya kuwekea maua ya urembo na vifaa vya kupendezesha Nyumba)
Yudovh essential (channel ya wanadada yenye kufundisha namna ya kutengeneza furniture au urembo wa ndani kutumia malighafi rahisi.)
DIY CEMEnt (channel yenye kufundisha kutengeneza majiko yenye kutumia kuni au mkaa lakini yametengenezwa na cement..jiko langu lipo juani linamalizia ukaukaji[emoji3]
Nashukuru channel nyingi Kati ya hizo zimeniletea faida ..[emoji120]
Ngoja niishie hapa kwa leo
Wapo wengine Ophorotube na hata hawa shaster tv.Hivi kuna ma youtuber wakorofi kama hawa TOPNOTCH??😂😂
Hawa ni wa hapa hapa nyumbani sio?Wapo wengine Ophorotube na hata hawa shaster tv.
Ndio ni hapahapa Bongo.Hawa ni wa hapa hapa nyumbani sio?
Nataka nifungue channel ya YouTube ila sijui niweke content gani? Mnisaidie wandugu?
Huyu mwamba ni noma sana sema sijui kingereza ila maelekezo yake lazima utamuelewa sana mfano video ya Battle ya google pixel 6 na iPhone 13 pro..MKBHD
Kuelewa kingereza ni deal kubwa sana mkuu kwa sababu unapata connection nyingi zaidi mfano blogger anaefundisha kwa lugha ya kiswahili huwa anapata traffic (watembeleaji) wachache kuliko blogger anaetumia kingereza mtandaoni asilimia 10 ni kiswahili but 90% iliobaki ni lugha tamu ya kingereza..Marquees Brownie naona jamaa anaingizampunga sana kwenye channel yake. Muda mwingine anashirikiana na MrWhoseTheBowse kufanya review za simu. Mimi nampend zaidi MrWhoseTheBowse