Kumekuwa na mkanganyiko mkubwa kuhusu ukweli kuhusu Israel. Wengi wakidai waisrael wa leo siyo OG ni kikundi cha watu tu waliamua kuja kufanya makazi kwenye ardhi ya wa-Palestine kwa lazima.
Mwenye uelewa anieleweshe wa-Israel wa kwl ni wapi na ipi historia yao kabla ya mwaka 1947.
Changamoto kubwa kuhusu Wayahudi hapo Israel itakubidi kwanza uamue kujadili kwa mujibu wa iman au akili ya kuzaliwa nayo.
Kwanini nimekupa hizo option 2? Sababu iman unakupa kikomo cha kufikiri ila akili ya kuzaliwa nayo haitakupa kikomo cha kung'amua.
Wayahudi wasasa ni wahamiaji walionza kurejea Palestina mwaka 1917 toka Ulaya Mashariki, waliamua kuamza kurejea mara baada kunyanyaswa sana na jamii za wazungu huko Ulaya hasa mashariki.
Uingereza chini ya waziri wa mambo ya nje Sir Joseph Chamberlain aliahidi kuwapatia eneo wayahudi waliobaguliwa huko Urusi na Ulaya, alipendekeza kuwaleta Uganda 1903 ila Wayahudi walikataa na walianzisha harakati za kurudi Palestina.
Wakati huu Palestina ilikuwa chini utawala wa Otoman Empire ambapo ilikuwa ni moja ya dola yenye nguvu hapa Duniani. Uingereza alifanikiwa kuyarubuni mataifa kadhaa ya kiarabu kama Misri na Jordan kumpiga Otoman Empire kwenye vita ya 1 ya Dunia na hatimae wakamshinda na rasmi eneo la Palestina akapewa Uingereza kama mwanagalizi chini ya League of Nation's.
Uingereza alikuwa katika harakati pia za kuwatafutia eneo la kuishi Wayahudi na hii ilipata nguvu mara baada ya Uingereza kuitawala Palestina, mwaka 1917 Wayahudi walianza kurejea rasmi Palestina huku Uingereza ikipewa jukumu lasmi la kusimamia uundaji wa Taifa la Kiyahudi.
Hatimae mara baada ya Vita kuu ya pili ya Dunia nchi ya Israel iliundwa yaani 1948.
Nirudi kwenye swali lako mama, Je! Wayahudi hawa ndiyo wale wa kale? Jibu ni Hapana.
Inasemekena Wayahudi walitoka huko Palestina 1517 kukimbia manyanyaso ya utawala wa Otoman, na walianza kurejea mwaka 1917 yaani walikaa Ulaya zaidi ya miaka 400! Kiufupi tunaweza sema vilipita vizazi zaidi ya 5! Hapo katika vizazi 5 pamoja na kujamiina na jamii nyingine za Ulaya na Urusi bas ni wazi kuwa waliorejea kuanzisha nchi hawakuwa Wayahudi wale wa kale.
Hapa sijagusa ya utumwani Misri na ya Utawala wa Rumi.