Hii kitu huwezi izuia ikiwa serikari ya aina hii ya kinyonyaji isiyo jali maslahi ya Wana nchi.
Chanzo Cha ukahaba ni uhaba wa Ajira na Elimu yenye manufaa kwa vijana na Jamii kwa ujumla.
Imagine mtoto anasoma miaka 12 (shule msingi mpaka secondary) na hapo anatoka secondary na miaka 17-20 akiwa hana Fani yeyote ile aliyo ipata kwenye hiyo miaka.
Na hapo kuna mawili ku'fail au kufaulu na akifaulu kuendelea ajira hamna. Na aki fail ndo ameishia hapo so mtoto anakosa direction Moja kwa Moja, ukichangia na Yale maneno unakuta anaambiwa pia wazazi unakuta hawana Options nyingne zaidi ya kukwambia alime au kuoa/kuolewa, hapo ndo unakuta watoto wengi wanakimbia makwao wanaingia mjini kutafuta kazi, wengi wanaishia Kuwa ma barmaid na wengine Madanga , vijana wa Kiume kujiingiza kwenye makundi mabaya kwa ajili ya kujipatia ridhiki.
Swali, Je! Serikari imejipangaje kuwa push au kiwainua au kuwawezesha wale walio fail masomo yao ya O 'level au S/msingi Ili wapate kujiajiri pamoja na kujiinua kiuchumi? Lakini pia hapo hapo serikari imejipangaje kupambana na wimbi la uhaba wa Ajira kwa vijana ambapo chanzo kikubwa Cha Madanga na bishara ya ukahaba?
Kuwakamata na kuwapiga faini nadhani siyo solution kwa sabab Bado Kuna vizazi vingine vinakuja so kutumia nguvu kubwa kupambana hawa badala yake tutengeneza tiba ya kudumu kwa kuboresha mitaala ya Elimu lakini pia kuwatengezea vijana mazingira wezeshi ya kulikomboa kiuchumi.
Mm Nafikiri Serikari ikitengeneza mazingira wezeshi hizo biashara zitapungua kama siyo kuisha kabsa.