Yani nieleweshwe kuhusu roho wakati mnadai kila mtu ana roho ,utanieleweshaje kwa kitu ambacho tayari ninacho , huo ni mwanzo wa utapeli sasa[emoji848][emoji848][emoji848]
Naomba pia maelezo ya utofauti wa ulimwengu wa roho na telepath. Naitaji kufahamu hili, maana wanasema ulimwengu wa roho ndo umebeba kila kitu kinachoonekana mwilini.
Naomba pia maelezo ya utofauti wa ulimwengu wa roho na telepath. Naitaji kufahamu hili, maana wanasema ulimwengu wa roho ndo umebeba kila kitu kinachoonekana mwilini.
Telepath ni kumanipulate energy ili kuweza kuendana na You energy capability na kusend frequency kuweza kuisoma hiyo energy kwa level fulani..
Unajua In the universe we are all connected..
Kwa mfano unaweza kutumia Telapathic ability kumcontrol mtu matendo yake na vitu vyake na kujua hata mambo yake yote lakini bila kuingia Spiritual realm...
Kuna watu wana Ability Ambazo tunaziita Clairs..
Au Another Beyond senses..
kuna mtu anaweza kujua feelings za mtu na akakuambia huyu mtu ana matatizo kwenye familia na Ana shida maybe kazini na akakuambia mpaka sehemu anayoishi hii inaitwa Clairsentience...
na kuna.
Clairvoyance: Clear seeing, the ability to gain information about an object, location, or event beyond normal human perception.
Clairaudience: Clear hearing, the ability to perceive sounds or information beyond the scope of ordinary hearing.
Claircognizance: Clear knowing, the ability to know things without having direct or obvious access to that knowledge.
Na zote hizi ni just Energy and Frequency manipulation na sio lazma uingie kwenye Spiritual Realm..
Japo kuna baadhi ya Information lazma uingie spiritual realm kama Past details na future details
Swali zuri hili na mara nyingi tunakuwa hatuwezi kuuliza maswali kama haya kwa sababu tunajifanya tunajua kwa hio tukiuliza maswali kama haya tunajiona wajinga,kwa hio tunabakia hatuulizi ili tuwe miongoni mwa wanaojua.
Roho, nafsi na mwili ni vitu tafauti na kila kimoja kina kazi yake ili kumtimiza mwanadamu awe kamili,ukikosa kimoja kama ya hivyo vitatu, uwawadamu wako utakuwa mashakani.
Tuanze na mwili
Mwili asili yake ni hapa duniani au kwenye dimension hii au realm hii ya dunia au existence, hapa ndio pahala pekee mwili unapoweza ku-exist
Kazi ya mwili kubwa ni ku-host nafsi,yaani nafsi inauvaa mwili na kuishi kwenye mwili, yaani kama vile unapokumbwa na shetani, Anakuwa ameuvaa mwili na anajitambulisha kama yeye na sio wewe tena. Na nafsi inafanya hivyo in a permanent basis yaani kwa namna ya kudumu.
Na mwili ni kama mashine inayomfanya kazi kwa ajili ya nafsi kuweza kuishi kwenye dunia hii,realm au dimension hii.
Mwili kazi yake ni kukusanya information kupitia hisia zake kuu tano,kuona,kusikia,kuonja,kuhisi,kunusa
Sasa twende kwenye roho au kwa kiingereza soul
Soul ni kiunganishi baina ya nafsi na mwili, soul au roho ndio muezeshaji mkubwa wa nafsi, soul ndio mkalimani anaetafsiri kwa nafsi kila kitu kinachofanywa na mwili hapa duniani,
Ndani ya soul kuna emotions,intellect and will, sijui kwa Kiswahili nisemeje hapa,mi sijui tunaitaje emotions kwa Kiswahili
Mwili kupitia hisia zake kuu tano unakusanya information na kupeleka kwenye soul kwa njia ya intellect(akili)
Akili inaweza kufanya kazi upitia hisia za mwli tu bila ya hisia za mwili akili haina uwezo wa kufanya kazi,macho yakiona kitu akili ina-process na kutafsiri ni nini macho yameona kupitia kumbukumbu za akili.
Maskio yakisikia kitu akili ina-process kisha inatafsiri nini maskio yamesikia
Na hisia nyengine kazi ndio hio hio
Sasa tuingie kwenye nafsi au sprit
Sprit ndio uhai wenyewe,yaani sprit ndio mtu mwenyewe naejelewa au kujitambua,utambulisho wa mtu hautokani na mwili wala roho wala akili
Utambulisho wa mtu mimi ni nani unatokana na nafsi au sprit
Kwenye sprit au nafsi kuna mambo matatu makuu
Kuna intuition,consciousness na submission to the source au God
Intuition ni uwezo wa kujua kitu bila ya kujua umejuaje, inatokea unajua tu bila kuambiwa ua kufundishwa
Consciousness ndio uhai wenyewe na kujitambua
Na submission to the source ni kusalimu amri kwenye chanzo cha sprit au nafsi na hiki tunakiita mungu au God
Vitu hivi vyote vipo kwenye nafsi au sprit
Nafsi au sprit haiwezi kuishi hapa duniani bila ya mwili na soul(roho) ndio mana mtu akiwa mzee na mwili umechoka nafsi inaondoka na mwili unaparalaiz na haujiwezi tena na hicho ndio kifo.
Pia mwli ukipata majanga makubwa kama ajali na ukawa hauwezi tena kui-support nafsi dakika hio hio nafsi inaruka permanently na kuondoka na hicho ndio kifo
Kifo ni kufariki
Fariki maana yake ni kutenga,au tunasema kufarakana maana ni kutengana
Kwa hio maana yake ni nafsi inafarakana na mwili hio ndio kufariki au kufa
Mi nadhani niishie hapa kama kunakuwa na Shaka tutaulizana
Mada hii nlielezea kwa kina kidogo kwenye uzi huu hapa chini wa kiingereza
What is spiritual awakening? Spiritual Awakening means that you have realized that you are an Immortal and Eternal Spiritual Being, not a Mortal Human Body. Where do we come from? God, or Divine Intelligence, is not a Person but a Neutral Power with the Potential for Unlimited Creation. God...
Nikiri kwamba nimesoma bandiko lako...
Na umeelezea Vizuri sana..
I think Uko sahihi sana kama nilivyosema Mwanzoni..Ntaendelea kusema hivyo pia..
NaQuotes Baadhi ya Comments yako..
-Sprit has three parts, consciousness,intuition and submission to the source(God)
-soul has three parts, emotions,intellect/mind and will(I will do/ I will not do)
-body have all the senses, smell,hear, see, touch,feel,etc
The way it is, is that spirit is the godly part in human and the soul is the connection between spirit and body, the soul function is to make sense to the spirit all things the body does
Na kwa hayo uliyoandika Sina shaka na wewe kabisa..
Ila shida Ni Tafsiri yako ya Kiswahili..
Roho ni spirit..
Nafsi ni Soul
Body ni Mwili..
Hata binadamu Hakuumbwa Akiwa Nafsi "Yaani akiwa Soul"
Ilibidi Apewe the connection Between These Two realm (Body and soul) na That Connection its Called Spirit au Roho..
Na ndo maana maandiko ya Kikristo,Kiyahudu na Kiislam yanasema..
"Mungu akampulizia Adam (Body /Udongo) Pumzi ya uhai (The Spirit/Rua'ch/Ruuhu/Pneumo/Roho)
Na akawa Nafsi hai (Soul/Nefesh/Nafsi)
Kwahyo between Nafsi (Soul) and Body Sit the Spirit..
Swali zuri mkuu, manake hapa ndio tunapochanganywa ili tusielewane tunapojadiliana kuhusu uhalisi wetu binadamu.
Maana ya nafs ni self au awareness of self au conscious of one’s self, haya yote kwa ukamilifu wake ya I namaanisha spirit
Na maana ya soul ni ruh kiarabu au roho kiswahili
Na ukitazama maana ya spirit utakuta pia maana yake ni ruh kwa kiarabu na kwa Kiswahili ni roho, huu ni mkanganjiko
Sisi binadamu katika mafunzo yetu tunakuwa hatufundishwi kuhusu spirit kwa undani, mara zote huwa inatajwa tu, na ikitajwa huwa inaunganishwa na soul ili tufahamu kuwa spirit ni soul au binadamu ndio soul
Ngoja nifafanue hapa kidogo kwanini hatufundishwi hivi vitu
Kama nlivyosema katika hizo mada za awali kuwa mwanadamu ana sehemu tatu
Spirit,soul and body
Spirit ni sehemu ya ndani zaidi,soul ni sehemu ya kati na body ni sehemu ya nje
Spirit inapata informatin from the source (god) through intuition,spirit haiwezi kufundishwa kitu kutoka hapa duniani,inajua inchojuwa kwa kujua tu na sio kwa kufundishwa
Soul ipo kati ya body and spirit na ina uwezo wa kupata information kutoka kwenye sprit au body inategemea na Kipi kimewezeshwa mwanzoni, kwa mfano ulipozaliwa tu ni Kipi kimewezeshwa kwanza, soul kupitia intellect inaweza ku-adapt na mfumo wa mwanzo, ama mfumo utakuwa kutoka sehemu ya ndani au spirit au wa nje ambao ni body.
Katika mifumo yetu ya maisha spirit imeachwa na kufungiwa kabisa,mtu akizaliwa tu zinatumika hisia zake za mwili( maskio,macho,hisia,ku-taste na kunusa) ili kuingiza infomation akilini info ambayo ndio ina control mwanadamu kwenye maisha yake yote, na kama info hii sio sahihi au sio kweli inakuwa haiendani na spirit na kama haiendani na spirit mwanadamu anakuwa gerezani muda wote wa maisha, anakuwa hajui kitu chochote kwenye uhalisi wake anajua alivyofundiahwa tu.
Kwa ufupi spiritual knowledge inatoa uhuru na kumuwezesha mwanadamu na mafunzo yalotokana na body kama sio kweli ya a uwezo wa kumjandamiza mwanadamu
Safi sana Faiza leo umejadili mada kwa utamu wake nimependa..
Japo mama yangu Nafsi Sio Psychology kwa kingereza ni Soul (Nafsi=Soul)
na ni kweli Katika Dini tulipewa Elimu chache sana kuhusu Roho,Mwili na nafsi..
Surah Ban-ilsrail aya ya 85-87...
(Quran 17:85-87)
"...Na wakikuuliza khabari za Roho (Spirit). Sema: Roho (Spirit) ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi. Nanyi hamkupewa katika ilimu ya Roho (Spirituality) ila kidogo tu. Na tungeli penda tungeli yaondoa tuliyo kufunulia. Kisha usingeli pata mwakilishi wa kukupigania kwetu kwa haya. Isipo kuwa iwe rehema itokayo kwa Mola wako MIezi. Hakika fadhila yake kwako ni kubwa.....
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.