Ipi ni tofauti ya mwili, nafsi na roho?

Mkuu ikikuoendeza sana naomba tufundishe mambo ya Astra projection,na pia hii mada ingia ndani sana ili wengine tufunguliwe macho.
 
Roho na nafsi ni viungo na dhana za kufikirika tu.

Havipo.
Wewe ni kichaa ...nafsi ni ufahamu wa kujitambua....roho ni spirit ndiyo energy kisayansi na mwili ni matter ambayo nayo ni energy tu hivyo Energy (roho) ni kila kitu mwili pia ni energy na nafsi ni energy pia hata mungu ni energy pasipo energy hakuna mungu wala chochote.
 
Mwili na nafsi vyote ni roho tumieni akili neno roho ni spirit ndiyo energy kisayansi....kwenye biblia mungu ana bainisha ukuu wa neno roho kwa kusema hata yeye ni roho na ufalme wake wote ni ufalme wa roho(energy) hivyo mwili na nafsi vyote ni roho
 
Mnachanganya mambo mwili na nafsi vyote ni roho (spirit) yaani energy.......Energy ndiyo mother nature ya vitu vyote hakuna kitu chochote kisicho energy
 
Hapo sasa ndiyo mkubaliane na mimi .....neno roho ni kiswahili kwa kingereza ni spirit na kisayansi ni Energy....hivyo ulimwengu wa roho ni kusema ULIMWENGU WA ENERGY ni sahihi kabisa maana ndiyo ilivyo
 
Wewe ni kichaa ..
Fala wewe.
Mwili upo una onekana.

Thibitisha una Roho acha Definition uchwara uchwara.
 
Naomba kujua utofauti na uhusiano wa Mwili, Nafsi na Roho.

Vipo wapi na vinatendaje kazi katika mwili wa mwanadamu.

Nawasilisha.
Mwili container/ kibebeo cha roho na nafsi. Roho ni uhai, ni kile kinachofanya mwili uwe hai kwa kusukuma damu ambayo ndiyo inapeleka chakula,maji na hewa sehemu zote za mwili. Nafsi inahusika zaidi na cognitive domain yaani mambo ya fahamu na maamuzi ambayo mtu anafikiria na kutenda, yaani hisia ya kiakili. Kuna wakati watu tunatumia maneno haya mawili yaani roho na nafsi interchangeably. Utasikia fulani ana roho mbaya. Hapa anakusudia kusema maamuzi ya mtu huyu hayampendelei yeye. Kwangu mimi nafsi ni kituo cha maamuzi katika mwili.
 
Mwili ni HALISI..... ni kila kitu ulichonacho na kinaonekana

Mwili na Roho SI HALISI...... ni vitu ambavyo vimebuniwa na kupewa majina ili kuelezea jinsi binadamu anavyo chakata maisha

Nafsi inaelezea kuhusu tabia na fikra za binadamu wakati Roho imekaa kiimani zaidi lakini mwili upo physically
 
Kwa hiyo inawezekana ikawa jukumu lako la kiroho ilikua uwe Daktari maisha yakakufundisha uwe askari kwa hiyo unakua umebeba nafsi mpya kinyume na roho yako sio yaani kuacha lile jukumu au lengo la msingi, NB:hili naona ni tatizo linalotusumbua wengi maishani kuwa na multiple self within one spirit then tunaondoka kwenye kusudi kuu lilotuleta ulimwenguni.
 
Nenda post #59 kuna video clip ina diagrams zinafafanuwa vizuri.
 
Hapa naona kuna mitazamo miwili; mtazamo wa kiimani na ule wa kisaikologia/ kibiolojia.Kiimani bado inabakia kuwa mwili ni chombo/ container ambamo ndani yake kuna roho na nafsi.Roho ni universal maana yake ni kuwa inamuunganisha mtu(mwili) na muumba wake kwa miili yote. Nafsi ni unique/hazifanani. Kila mwili una nafsi ya peke yake. Hakuna watu wawili wenye nafsi zinazofanana. Nafsi ni pamoja na mfumo wa kiakili, tabia za mtu kwa kadiri akili yake inavyomtuma, hisia za kupenda,kuchukia,kufurahi, huruma, ukatili nk.Ni vigumu wakati mwingine kutenga nafsi na roho.Hii ni kwa sababu vyote hivi ni vya kisaikologia zaidi kuliko kibiolojia. Hivyo ni rahisi kuvitumia kwa kuvipishanisha yaani interchangeably. Kwa hivyo hakuna mpaka mzuri wa kutenga roho na nafsi. Ni vigumu kusema kipi kinaongoza kingine.Hii ni sawa na mapacha wanaofanana, tofauti yao ni ndogo sana lakini ipo.
 
Tukienda kwenye biology mwili ni physical/tangible yaani unaonekana na unagusika. Roho ni kisaikolojia zaidi kuliko kibiolojia. Roho haigusiki, haionekani. Ni mental picture.Nafsi haionekani na haigusiki vilevile. Nafsi inajitokeza kwenye matendo ya mtu.Hapo tunajua tabia yake, anachopenda,asichopenda, ubunifu, ujinga wake yaani tunajua cognitive domain ya mtu huyo. Mtu anaweza kusema kuwa mtu anaweza kuitawala nafsi yake.Sitaki kuamini kuwa mtu anaweza kuitawala roho yake.Yaonekana kwangu kuwa roho inatawala nafsi. Yangu ni hayo tu kwa leo waungwana.
 
Umeeleza vzr sana. Kwa maneno mengine rahisi (tukianza na mwili) mwili ni hii body (housing) tunayoiona. Ambayo kiuhalisia imejaa sense organs na organs nyingine ndani kufanya mwili uwepo. (Kwenye mwili ulieleza vzr sana).

Soul ambayo ni roho, kiuhalisia ni Ile nishati iliyopo kwenye ubongo ambayo tunaita akili. Ule uwezo wa akili kuchakata taarifa na hisia zinazoletwa na mwili (sense organs) naweza kusema ndo roho. Akili iko kwenye ubongo, ubongo ni vimajimaji vyeupe vizito ambavyo ni ngumu kueleza vinafanyaje kazi.... kiufupi tafsiri ya akili ni ngumu kufafanua lkn Ile nishati iliyomo kwenye akili kupokea taarifa na hisia, kuchakata taarifa na hisia, na kuzitunza na nyingine kuzirudisha kwenye mwili naweza kusema hicho ndo kinaitwa ROHO.

Tukimalizia na nafsi, nafsi ni sehemu ndani ya akili ambapo mkusanyiko wa taarifa na hisia zilizotunzwa na ubongo toka kuumbwa zilipo. So nafsi ni zile taarifa na hisia zilizohifadhiwa na ile sehemu ambayo imezitunza hizo. Taarifa hizo na hisia hizo ndizo hutengeneza mitazamo na imani ya mtu. Ndo utu wa mtu mwenyewe. Ndo mtu huyo. Generally, scientifically roho na nafsi viko kwenye ubongo lkn havionekani ni energy, yaani nishati not physical. Nafsi kuna watu wanaiita subconscious mind.

Nafsi inatengenezwa au hutokana na roho (au ubongo). Wakati taarifa na hisia zinazochakatwa na roho hutoka kwenye mwili.

Dini (Ukristo na Uislamu) na wanadini wali- copy mawazo ya philosophers kuyahusianisha hayo na dini au Mungu
 
Naomba kujua utofauti na uhusiano wa Mwili, Nafsi na Roho.

Vipo wapi na vinatendaje kazi katika mwili wa mwanadamu.

Nawasilisha.
Kwanza kabisa tunapaswa kutambua kuwa Mungu ni Roho Yoh 4:24 na vinavyoweza (kuwa na mahusiano nae) ni viumbe vilivyo Rohoni (Spiritual realm) ndio maana tuna Roho Malaika na shetani rasilimali na Mungu (Ayu 1:6-8)

Turudi sasa kwa Mwanadam, Mwanadam/ mtu nikiumbe kilicho na vitu muhimu muhimu ni;-
  1. Roho
  2. Nafsi
  3. Mwili
Hivi ndivyo vinamuwezesha mtu kutoweza (Socialize) kwenye limwengu mbili tofauti huwenda kwa nyakati tofauti au kwa wakati mmoja kushiriana na limwengu zote mbili kwa pamoja.

Mtu ni ROHO anayo NAFSI na anaishi ndani ya mwili wa MWILI. Mwili ndio humsaidia mtu na yaliyomo katika ulimwengu wa mwili (physical realm)
Na ndio humsaidia mtu kusaidia/ Roho Mtakatifu na ulimwengu wa Roho ambao ndio MUNGU Mwenyezi na viumbe wengine kama malaika na shetani. Pia hii Roho ni imetoka kwa Mungu moja kwa moja yaani Roho ya mtu asili yake sio duniani Mwa 2:7 na ndio maana nafsi siku zote inashindana na roho katika utendaji kazi Gal 5:17 pia mtu anapokufa Roho yake humtoka na kuelekea mahali pa mangojeo ya kihama/ mwisho wa dahali. Hii pumzi ya uhai iliyozungumzwa kwenye Mwa 2:7 kwa lugha ya asili ya uyahudi huitwa Ruach kwa maana ya designated ghost.

Tuendelee...
Nafsi ya mtu iliumbwa pamoja na Roho ila haikuwa hai sababu ya nguvu inayoleta uhai nafsini haikuwepo ila mara baada ya pumzi (ruach)/ roho kuingia mwilini ndipo nafsi ikapata uhai Mwa 2:7.
Basi nafsi ni nini hasa?
. NAFSI ni kiunganishi kati ya roho (ulimwengu wa roho) na mwili (ulimwengu wa mwili) nafsi ndio huipa utashi/ ufahamu mwili wa mtu ambapo kazi ya nafsi ni kutafsiri yale yatokayo Rohoni ili yatendeke mwilini na yatokayo mwilini ili yaijaze/ kuishibisha Roho.
Nafsi hai ya mtu ndio humpa uwezo wa kuona, kuona, kuhisi, kugusa na kupambanua mambo kwa usahihi kwa wema au ubaya.
Nafsi hufa bali Roho hulala kungojea siku ya hukumu.


Prepared by
~Mwl. Eric Tonelo ~
0678 034 970
 
Hi mada inakuwaga ngumu sana maana inahusuana na kazi za Mungu

Mtu anaweza akandika maelezo mengi kama garazeti na mado usimuelewe

Kwa uelewa wangu Mimi Kwa kifupi

1) ROHO
Roho ndio msingi wa uhai wako roho ikitoka na wewe Kwisha habari yoko Ili nafsi na mwili vifanye kazi vinahitaji uwepo wa roho

2) NAFSI
Nafsi ndio ubinadamu wenyewe Yani mambo yote ya kibinadamu unayoyafanya unatumwa na nafsi yako uyafanye
Ubongo wako unakazi ya kuvisimamia vyote nafisi na akili
Ukitamani kumgonga demu Fulani hiyo nafsi yako ndio inataka ufanye hivyo akili yako nayo ikikubaliana na nafsi utaanza michakato ya kumfuatilia huyo demu

3) MWILI
Mwili ni jumba lenye viungo Ili kufanya mambo ambayo nafisi inataka yafanyike

Note
Roho kazi yake ni kuupa uhai mwili wako na nafsi yako na Kuna mda Huwa inatoa taarifa Kwa mwili wako na nafsi yako Kwa baadhi ya mambo ambayo yatatokea na kukugusa maana roho inauwwzo huo

Mfano
Unaweza ukaota msiba ambao utatokea katika familia yako hapa inaama roho yako imeshaona hivyo inaipa taarifa nafsi yako


Au unaweza ukajiona mkono wako wa kulia au kushoto unawasha sana hapa roho inaupa taarifa mwili wako kuwa utapokea au utatoa au utapoteza kitu unacho kipenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…