Ipi ni tofauti ya mwili, nafsi na roho?

Wote tulizaliwa na kufundishwa kuwa tumegawanyika mara tatu yaani mwili,nafsi na roho ila kiuhalisia tulikuwa tumegawanyika mara nne yaani mwili,nafsi,roho na moyo(sio unaopasuliwa india)

Mithali 4:23
Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

Mathayo 5:8
Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.

Roho ni copy ya mwonekano wako isiyooneka ila mnafanana kila kitu ndio ulikuwa mlango wa wachawi na falme na mamlaka kukufikia.Na roho ilikuwa ni kuugua tu

Warumi 8:23
Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu.

Ukiwa nafsi ilikuwa ni kubeba uchafu tu na kuwa mchafu

Ukiwa mwili manake ni adui na Muumba na huwezi kutii kanuni zake kamwe

Warumi 8:7-8
7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.
8 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.

Kusudi la Muumba ni wote tuwe moyo yaani mema na mazuri peke yake,sio roho,sio nafsi wala mwili.
 
Binadamu=Mwili+Moyo+Nafsi+Roho.

Mwili=Umbile la kifizikia(linaloshikika na kuonekana)

Moyo=Tabia/Haiba/utu/dhamira ya mahusiano ya mtu na wenzake au na Mungu.

Nafsi=Ufahamu/akili ya mwanadamu.

Roho= Nadharia ya kusadiki uwepo wa nguvu inayoendesha/kuathiri NAFSI zetu isiyoonekana/kuelezeka.

Mungu=Roho/Nguvu kuu isiyo na mipaka juu ya NAFSI na MWILI.

Shetani=Roho/Nguvu kuu hasi inayoathiri NAFSI.

Neno=Roho/Mungu.

Maji ya Uzima=Neno la Mungu.

Uzima wa milele=Roho isiyo na ukomo wa muda.

Kufanywa wana wa Mungu=Kubadilishwa kuwa Roho.

Wana wa nyoka/shetani=wenye MWILI kwa kuwa NAFSI zao uathiriwa na roho hasi.

Ubatizo=kukiri kwa NAFSI kupokea MAJI YA UZIMA.
 
Mwili ni nyama(kunusa,kuona,kuonja,kuhisi,kusikia)
Roho ni tabia za nafsi yako(uzinzi,wizi,kutokumwamini mungu n.k)

Nafsi ni mtu mwenyewe(wa Mungu ama wa ibilisi)
Naomba kujua utofauti na uhusiano wa Mwili, Nafsi na Roho.

Vipo wapi na vinatendaje kazi katika mwili wa mwanadamu.

Nawasilisha.
Wili
 
Ni kweli, Spirit ni Roho na sio nafsi. Mfano Holy spirit (Roho mtakatifu)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…