Maendeleo ya kweli hupatikana kwa kuzalisha wenyewe na siyo kununua.
Kwa sababu ya umasikini wa fikra, tunazalisha wapigadomo wengi kuliko wataalamu.
Wanahitajika wataalamu wa ndani, makandarasi wa ndani, wenye ujuzi, teknolojia na uwezo wa kujenga miundo mbinu na viwanda vya uzalishaji ili tuendelee.
Kuwalipa wachina, wajapani, wazungu, waarabu,.... ili watujengee barabara, miradi, mitambo na viwanda siyo maendeleo ya kweli.
Hata hivyo, kwa sababu ya umasikini wa fikra, hayo ndiyo huitwa maendeleo na wapigadomo.