Ipi tofauti kati ya Mbunge wa Taifa na Mbunge wa Jimbo?

Ipi tofauti kati ya Mbunge wa Taifa na Mbunge wa Jimbo?

Richard

Platinum Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
16,890
Reaction score
26,440
Wakuu, nimeshtushwa kusikia hii statement leo kutoka kwa kiongozi wa nchi raisi Samia kwamba kuna mbunge wa Taifa na kuna mbunge wa Jimbo.

Mwezi October mwaka huu nchini Tanzania kutafanyika uchaguzi mkuu wa wabunge na pia raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo raisi wa sasa Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuidhinishwa kuwa raisi wa awamu wa 7.

Atakuwa ni raisi wa Awamu ya Saba kwasababu kwa sasa ni raisi wa Awamu ya Tano (kwasababu amalizia awamu hiyo) na pia ni raisi wa Awamu ya Sita kwa sababu yeye ni ana ajenda tofauti na yule raisi aliepita hivyo hawalingani sera zao.

Raisi Samia alipokea kiti cha uraisi baada ya aliekuwa raisi wa Awamu ya tano John Magufuli kufariki dunia mwezi march mwaka 2021.

Sasa raisi Samia yupo katika ziara ya kanda ya Ziwa na akiwa katika Jimbo la Kisesa alimsema Mbunge wa Jiimbo hilo mheshimiwa Luhaga Mpina kwamba asiombeombe pesa za miradi moja kwa moja kwa raisi kwenye mikutano na wananchi.

Katika hotuba yake ya akijibu maombi ya Mpina, raisi Samia amesema Mbunge huyo alipaswa kuwasilisha maombi yake kupitia TAMISEMI na sio katika mkutano huo na kwamba asitafute umaarufu kupitia mikutano ya raisi na wananchi.

Lakini la msingi katika mada hii ni kwamba raisi Samia akasema kwamba Mpina si mbunge wa Jimbo bali ni mbunge wa taifa akimaanisha (kwa uelewa wangu) kwamba Mpina alipaswa kuwasilisha maombi yake Bungeni ambako ni Dodoma makao makuu ya nchi.

Sasa, kwa maana hiyo ni kwamba Mbunge wa taifa ni yule ambae akiishachaguliwa na wananchi kwenye jimbo basi tiyari amepewa tiketi ya kwenda ziarani kwenye bunge la Taifa yaani Bungeni Dodoma akakaa huko weee, na kisha ukikaribia uchaguzi kama huu mbunge huyo hurudi Jimboni kuomba tena kura kwa wananchi na kuchungulia miradi ya hapa na pale.

Mbunge huyo wa Kisesa aonekana apendwa sana na wananchi wake maana hawakupiga makofi wala kushangilia pale raisi Samia alivyokuwa akimnanga mbunge huyo wa Jimbo la Kisesa jimboni kwake (kama tunavyoelewa Mpina ni Mbunge wa jimbo la Kisesa)

Lakini pia mheshimiwa Mpina huenda alikuwa akisisitiza kuhusu ombi hilo la kujengewa barabara ya lami katika jimbo hilo ambayo hata raisi Samia mwenyewe amepita katika barabara hizo na kuona vumbi lake.

Huenda vumbi hilo lilokuwa likitimka limesababisha ajali ya gari ambayo imeua watu 4 na wengine wengi zaidi ya 50 kujeruhiwa vibaya. Lakini kama kungekuwepo barabara safi ya lami na taa za barabarani, alama za waenda mguu na na taa za kuongozea magari ajali hiypo isingekuwepo.

Namalizia kwa kuuliza suali je, ipi tofauti kati ya mbunge wa Jimbo na Mbunge wa Taifa na je majukumu yao yatofautiana wapi katika utendaji wa shughuli zao iwe bungeni au jimboni?

Haya wakuu ,karibuni kwenye hii "brain storming".

Paschal Mayala, Nguruvi, Mwanakijiji wakongwe wenzangu na wengine karibu.
 
Slikuwa anamtafuyia yu sababu ya kumchafua Mpina. Uzuri wananchi wamemuonyesha Rais ni yupi wanamkubsli kati yao. Mpina slipata jrlele na change wakati Maza aliabulia vikofi vya wateule wake. Hii jeuri ya Viongozi wa CCM kuwachagulia watu viongozi nfiyo imesababisha Maza kiongea kitemi vile.

Ndiyo maana tunasema hii Reform inawahusu pia CCM. Kuna wengi Maza atawaondoa kwa vile hawapenfi. Kaanza na Gwajima, sasa Mpina ... list itaongezeka with time.
 
Kiukweli kupata rais wa kurithi urithi kutoka Kwa marehemu ni hasara kubwa sana Kwa taifa.aliongea ugoro mtupu na ujinga
 
Back
Top Bottom