Ipi tofauti ya Ibilisi, Mnyama na nabii wa uongo?

Ipi tofauti ya Ibilisi, Mnyama na nabii wa uongo?

Undava King

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2017
Posts
3,422
Reaction score
5,659
"Na yule ibilisi, mwenye kuwadanganya akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele" (Ufunuo wa Yohana 20:10)

Naamini JF siwezi kosa majibu ya maswali haya tafakarishi ninayojiuliza baada ya kukisoma kifungu hicho kutoka katika kitabu cha ufunuo wa yohana 20:10 sababu humu kuna watumishi,waamini, wanatheolojia, na wasomaji wazuri wa biblia wanaoweza kunipatia ufumbuzi wa kifungu hiki ambacho kina vitu vikuu vitatu ndani yake yaani IBILISI, MNYAMA na NABII WA UONGO.

1. Je, upi ni utofauti wa ibilisi, mnyama na nabii wa uongo?

2. Ikiwa ibilisi umaanisha shetani, je mnyama na nabii wa uongo ni akina nani hao kwa mujibu wa maandiko.

3. Je, binadamu anakabiliana na maadui wangapi hapo ni watatu au ni shetani tu?

4. Je, binadamu mwenye hatia atoangukia kwenye adhabu hii ya moto wa milele?Maana kulingana na kifungu hiki vinaonekana viumbe hivyo vitatu tu ndiyo vipo motoni.

5. Kwanini inaonekana kana kwamba mnyama na nabii wa uongo watamtangulia ibilisi kuingia motoni?
 
"Na yule ibilisi, mwenye kuwadanganya akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele" (Ufunuo wa Yohana 20:10)...
Kwa uelewa wangu hao ni viumbe watatu tofauti, lucifer aka Ibilisi aka Joka kuu ndio kiongozi wao. Ibilisi ndio kawapa nguvu na kuwatanguliza mnyama na nabii wa uongo kuandaa mazingira ya yeye kuja kwa ajiri ya vita kamili.

Ibilisi anatawala dunia kwa kupitia huyu mnyama ukisoma ukusima Daniel wale wanyama wanaoelezewa humo katika maumbo tofauti tofauti.

Pia inasemakana mnyama ndio huyu huyu antgod au antchrist na ndio maama mpinga kristo haonekaniki mwishoni akitupwa katika ziwa la moto.

Nabii wa uongo huyu ndiye yule ambaye atashusha moto toka mbinguni na kudanganya watu wa Mungu.

Siku za mwisho hao wote wataoneka wazi wazi kwa wale watakao bakia watawaona live.
 
Hawa wote wanaoperate under one umbrella

Maandiko yanasema "Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho" Efe 6:12

Kwa hiyo lucifer ana falme na mamlaka, wakuu wa giza, na jeshi lake la pepo wabaya ambayo hawa ndio binadamu anapambana nao, ukiwa wa kiroho hivi vita utavishuhudia jinsi mpambano ulivyo.
 
Unavyofikiri hili linaweza kuwa na uhusiano wa karibu na uwepo wa namba zenye tarakimu 3 yaani 666 kumwakilisha mnyama?
Hawa wote wanaoperate under one umbrella

Maandiko yanasema "Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho" Efe 6:12

Kwa hiyo lucifer ana falme na mamlaka, wakuu wa giza, na jeshi lake la pepo wabaya ambayo hawa ndio binadamu anapambana nao, ukiwa wa kiroho hivi vita utavishuhudia jinsi mpambano ulivyo.
 
Sasa huyo Mnyama ni nani au ni mnyama gani na huyo mpinga kristo ana wasifu gani na kwanini aje nyakati za mwisho tu
Kwa uelewa wangu hao ni viumbe watatu tofauti, lucifer aka Ibilisi aka Joka kuu ndio kiongozi wao. Ibilisi ndio kawapa nguvu na kuwatanguliza mnyama na nabii wa uongo kuandaa mazingira ya yeye kuja kwa ajiri ya vita kamili...
 
Hili jukwaa siku hizi limekuwa la makasuku na makondoo wa dini tu. Mtu mnajadili mada kama hii kwa kutumia reference za biblia tu bila references nyingine alafu mnasema ni Jamii Intelligence Forum[emoji57][emoji57][emoji57]

Sasa si ingepelekwa kwenye jukwaa la dini tu?
 
Kuwa mfano
 
Dini zinapoteza watu sana.
Mnaowalalamikia kua wanakuletea magonjwa na kila aina uchafu ndo hao hao mnaendelea kutukuza dini zao kwa kuumiza kichwa kwa vitu ambavyo havipo.
 
Dini zinapoteza watu sana.
Mnaowalalamikia kua wanakuletea magonjwa na kila aina uchafu ndo hao hao mnaendelea kutukuza dini zao kwa kuumiza kichwa kwa vitu ambavyo havipo.
Mbadala wa dini hizi tulizonazo kwa sasa wadhani ni nini
 
Ibilisi kazi yake kushawishi bindamu kitenda maovu...

Mnyama anaendeshwa hajui halitendalo...

Nabii wa uongo ni sumu ni hatari sana... sababu anajua anachofanya siyo ila bado anakifanya...
 
Mpaka sasa wote mnazingua. Maelezo yenu hayana mashiko.

Anayejua tueleweshe vizuri kwa reference ya kitabu chochote anachokijua yeye, (iwe cha dini au cha kidunia)
 
Sasa huyo Mnyama ni nani au ni mnyama gani na huyo mpinga kristo ana wasifu gani na kwanini aje nyakati za mwisho tu
Hawa wote ni malaika waasi kama Lucifer, kwa hiyo lucifer ndio joka kuu au ibilisi, na hao malaika wawili mmoja anaitwa mnyama, mwingine anaitwa nabii wa uongo, wanaitwa kwa titles zao na lucifer ndio kiongozi wao yeye ndio anawapa nguvu hawa ili kufanya maandalizi ya ujio wake siku za mwisho,

Siku za mwisho wa dunia hawa malaika waasi watakuja duniani na mamlaka zao walizopewa, na wanaonekana kwa macho ya nyama ya kibanadamu, kuja kuendelea kudanganya binadamu watakao kuwa wamebakia baada ya unyakuo.

Huyu mnyama ndio mpinga Mungu au baada kuja kwa Yesu kristo akawa ndio mpinga kristo,.na huyu mnyama ndio anasimama kama falme mbalimbali za hapa duniani, utaona kipindi cha Daniel aliitwa mfalme wa uajemi.
 
"Na yule ibilisi, mwenye kuwadanganya akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele" (Ufunuo wa Yohana 20:10)...

Ibilisi ni roho ,roho ya uasi na awe nyoka au mtu akiwa na roho hiyo unaweza kumhita tu ibilisi tupo naye kila sekunde ukiona kuna wazo au kitu rohoni kinakushawishi kufaya dhambi ndio roho hiyo ya shetani yenyewe ukiona mdada kabana makario makusudi ili kuwatamanisha ni roho yenyewe ya ibilisi, ukiona mali ya mtu ukasikia sauti moyoni hii ni fulsa hiyo ni roho ya ibilisi sauti nyingine acha hiyo roho ya Mungu

Kwa hiyo myama awe mpinga kristo ni viumbe tu ndani yake kuna roho ya shetani ni swala tu la position na wakati upi yupi anatumiwa kwa kazi zake

Mwisho
Roho za shetani na roho yaMungu zipo nasi full time 24/7/ inatengea sasa roho nafsi ya mtu itachagua kusikia sauti ipi ila tupo nazo zote
Shetani hana mwili mwili ni wewe
 
"Na yule ibilisi, mwenye kuwadanganya akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele" (Ufunuo wa Yohana 20:10)...
Kuna kitabu nimewahi kukisoma kinaitwa Mnyama, Joka na Mwanamke kama sijakosea. Ngoja nikitafute nikipandishe hapa. Kinaweza kuwa kinajibu maswali yako mengi.
 
Kuna kitabu nimewahi kukisoma kinaitwa Mnyama, Joka na Mwanamke kama sijakosea. Ngoja nikitafute nikipandishe hapa. Kinaweza kuwa kinajibu maswali yako mengi.
Jitahidi ufanye hivyo Mkuu
 
Tofauti ya Ibilisi, Mnyama na Nabii wa uongo kutokana na vyanzo mbalimbali;

Sehemu ya Kwanza:

IBILISI - katika kiebrania huitwa 'accuser' or 'adversary' mshitaki au mpinzani.
Rejea (waefeso 6:12, chronicles 21:1)

Katika ugiriki diabolos (devil- slanderer to hurl(verb)I.e accusations.
Rejea (Deuteronomy 13:13, 1 samuel 1:16;2, chronicles 13:7) kutoka katika vyanzo vya zamani "dead sea scrolls"
Haimjadili shetani kama muovu katika biblia ya kiebrania bali Belial na siyo shetani hivyo baadae ndipo uhusika wa shetani ulikuja kubatizwa na wayahudi na katika maandiko ya kikristo. Kwa mara ya kwanza neno shetani lilianza kutumika (2 Corinthians 6:15) pale Paulo alipoanza kutofautisha term hii alipokuwa akizungumzia habari za Yesu.

Rejelea (Yohana 12:13) mtawala wa dunia Yohana 8:44 baba wa uongo (2 wakorintho 4:4) mtawala wa nguvu ya upepo (Waefeso 2:2) na beelzebul, mtawala wa mapepo(mathayo 10:25); (Marko 3:22); (Luka 11:15) kwa mujibu wa Yesu (mathayo 12:29), (Marko 3:27),(Luka 11:21-22) 'mwenye nguvu' shetani lazima afungwe kuporwa nyumba yake ambayo ndo hazina(yaani wanadamu)

Je, uislamu unamzungumziaje MNYAMA -( DAJJAL au MPINGA KRISTO)?

Al masih Ad- Dajjah, ndiye mpinga kristo ambaye atajitokeza baada ya nyakati za mwisho za nabii wa Mungu, Muhammad, " Messiah wa uongo, ambaye kila Nabii ametuonya kumuhusu akiwemo Yesu ndiyo maana tunamwita Mpinga kristo."

Dajjal ni mtihani mkubwa aliopewa mwanadamu tokea adamu na hawa walipotua duniani, yeye ni binadamu ambaye atautawala ulimwengu wote, kwa kuwapumbaza wana wa adamu na hawa kuwa yeye ndiye messiah, isitoshe pia atadai kuwa ndiye Mungu.

Dajjali- umaanisha muongo, Mtume Muhammad anawaambia waamini kwamba "Allah ajafichwa hili msimuone, yeye (Allah) siyo JICHO MOJA na ajanyooshewa kidole kuelekea katika jicho lake, akaongezea Al masih mweupe. Ad Dajjal ni kipofu katika jicho lake la kulia na macho yake uonekana kama zabibu inayochomoza.
Neno Kafir( asiye amini) limeandikwa kati ya macho yake mawili(paji la uso).
Mfano ni uwepo wa alama ya jicho moja kwenye US dollar bill, ngazi 13 za pyramid, na neno" In God we trust" ufunguaji wa jicho la tatu nakadhalika.
Biblia inasema "huu ni wito wa hekima. Kila mwenye fahamu afanye mahesabu ya nambari ya mnyama, kwa sababu ni namba ya mwanadamu. Na hiyo namba ni 666. (Ufunuo 13:18)
Hivyo basi uonapo kiashiria chochote kwenye logo, michoro, brand,television, show nakadhalika yenye jicho moja, 666 na msalaba uliogeuzwa juu chini zote zinamwakilisha mpinga kristo " k.f.r"

Mtume Muhammad alitabiri juu ya uwepo wa illuminati ambao pia umwabudu ibilisi(Lucifer), na jini liitwalo Dajjal, "mwana wa ibilisi" na wanasubiria kuja kwake kama ulivyo ujio wa messiah Yesu utakavyokuwa.
 
Back
Top Bottom