Ipi tofauti ya Ibilisi, Mnyama na nabii wa uongo?

1 siyo mwili unao kaidi ni nafsi inavutwa na tamaa za mwili hadi kutiishwa na mwili

2) mwili uliumbwa vyema tu ila kudanganywa na ibilisi ndiyo kuliuponza mwili na nafsi...ndipo neno dhambi likazaliwa.
3)Ufahamu ni nafsi

4) neno roho ni spirit ambalo kisayansi ni energy vitu vyote ni roho mwili na nafsi ni roho ndiyo maana vinaweza kurejeshwa hata baada ya kuoza au kuungua kuwa majivu ...kumbuka kuwa energy haiwezi kuangamia ila inabadilika tu kutoka umbo moja na kuwa umbo jingine

Maelezo yako yana-prove wazi kuwa umeanza kuchanganya mafaili:-
1. Umesema kuwa nafsi ni uelewa sasa iweje mwili ambao ni kama vazi tu la uelewa lilete majaribu wakati mwili uongozwa kutenda kupitia ufahamu?

2. Kwahiyo mwili kumbe uweza kujiamulia kutenda pasipo akili (nafsi) kwa maana unasema walidanganywa wote na ibilisi yaani mwili na nafsi?

3. Umejibu kitu ambacho ujaulizwa kukwepa swali kwa nadharia za kisayansi na kibudha, nimekuuliza swali la Mungu wa kwenye maandiko; je ana mwili au hana.
 
Nitajibu maswali yako kwa ufupi (ukihitaji maandiko na rejea usisite kusema)
1.
-Ibilisi ni malaika kerubi aliyeasi kwa kutaka kuwa "Mungu"
-Mnyama ni mfumo wa utawala ambao mamlaka yake yanapewa nguvu na Ibilisi mwenyewe, kama ilivyokuwa Israel ya kale kuwa Mungu ndo mfalme wao basi na Mnyama ndiye vivo hivyo, na kiongozi wake kama ilivyo kwa Yesu Kristo ukuu wa Mungu unakaa ndani yake ndivyo hivyo Mpinga Kristo Ibilisi mwenyewe anakaa ndani yake.
-Nabii wa uongo ni mfumo wa dini utakaokuwa na muonekano wa kimungu ila matendo yake ni ya ibilisi mwenyewe yaani uongo mwingi wenye kuhadaa wote wasio na imani thabiti!
-Umesahau sanamu ya mnyama: kuna uwezekano mkubwa sanamu hii kuwa 'Artificial Intelligence' au akili mnemba. Itakapopewa nguvu ya 'uhai' na kuweza kufanya yale yote ayafanyayo mnyama au Beast! Kuwa macho katika tasnia hii kwani kama mwenye nymba angalijua siku ya kuja mwizi angalikesha na asingeliacha nyumba yake kuvunjwa!

2. Nadhani nimekujibu hapo juu

3. Shetani ndio kinara wa yote hayo. Inakupasa ufahamu kuwa kulikua kuna uasi mkuu mara 3 huko mbinguni. Uasi wa kwanza ni wa Shetani/Ibilisi/Joka na majina yake mengine, aliadhibiwa kwa kuondolewa mbinguni na kukaa duniani mpaka muda wake wa adhabu kufika. Uasi wa pili ulikuwa wa malaika waangalizi walioacha maeneo yao ya kutawala na kuzaa na wanadamu, watoto wao ndio walikuwa 'giants' waliofanya maasi makubwa dhidi ya binadamu. Baba zao yaani malaika waasi walifundisha binadamu maarifa mabaya yote unayoyajua kuanzia kufanya vita, uchawi na ukahaba!. Adhabu yao ilikua ni kufungwa gizani mpaka siku ya hukumu ambako wateule watawahukumu! Watoto wao yaani 'giants' waliadhibiwa katika gharika na baadaye Joshua aliwaondoa katika nchi, wachache waliobaki Daudi na wanajeshi wake waliwashughulikia. Kuna siri hapa!.
Uasi wa tatu ni ule wa malaika waliopewa kutawala kabila za binadamu walipoasi na kuzifanya kabila hizo kuwa waabudu sanamu nk. Kumbuka pale Babeli Mungu alichagua Israel kama taifa ambalo kupitia hilo angekuja kukomboa kabila zote zilizopotea. Uasi wa malaika hawa utatimilizwa siku ya hukumu.
Hivyo panabaki ibilisi ambaye ndiye mastermind wa mpango wake wa kupindua serikali ya Mungu. Mungu alimpa mwanadamu dunia aindeleze na kuitunza. Shetani hapendezwi na hili kwa hio ni adui namba moja wa mwanadamu. Hawezi kumdhuru Mungu moja kwa moja kwa hio anadhuru watoto wake! Jeshi la Ibilisi ni pamoja na makamanda wake alioasi nao pamoja na roho za giants ambazo ndizo pepo wabaya hao kwa pamoja na malaika waliopewa kabila za dunia huunda ufalme wa giza na kutenda yaliyo gizani.

4. Ndiyo binadamu mwenye hatia atakuwa na adhabu ya kutupwa ziwa la moto unaowaka moto wa kiberiti yaani sulphur. Ukijua sifa za sulphur utaelewa japo kwa wastani moto huo, harufu na mazingira yake yakoje. Yai viza lina harufu ya sulphur!

5. Lazima vijakazi waanze kupata adhabu kabla ya mkuu wao kuhitimisha.

Asante

Inasemekana kuwa shetani alitupwa kuzimu, kulingana na maelezo yako inathibitisha kuwa duniani ndiyo kuzimu kwenyewe;

1. Kwanini Mungu mwenye upendo amuumbie binadamu kuzimu (mahali pa mateso/gereza) kuwa maskani yake?

NB: Kwahiyo kwa ufupi nilivyoelewa mimi kwa mujibu wa maelezo yako hapo; ibilisi= Malaika muasi au kiongozi wa waasi, Mnyama=Tawala za dunia, na Nabii wa uongo=dini.

2. Umeeleza kuhusu awamu tatu za maasi ambazo naweza kukubaliana nazo kwa kuwa ushahidi wake unaweza patikana katika maandiko lakini umeanza mambo ya ubashiri wa kisabato ya kuhusisha kila kitu na imani, nimeona umeanza kuzungumzia sijui AI na sanamu ya mnyama baadae ikija teknolojia nyingine pia utaendelea na utabiri wako ama?

3. Je, ukiwa kama mzazi mwenye akili timamu unaweza kumfungia adui yako aliyedhamiria kukuua chumbani anakolala mwanao?
 
Muumba hakuumba kuzimu wala jehanam wala ujinini hizo zote zimeundwa na mvamizi (ufunuo,nyoka,vita)
 
Maelezo yako yana-prove wazi kuwa umeanza kuchanganya mafaili:-
1. Umesema kuwa nafsi ni uelewa sasa iweje mwili ambao ni kama vazi tu la uelewa lilete majaribu wakati mwili uongozwa kutenda kupitia ufahamu?

2. Kwahiyo mwili kumbe uweza kujiamulia kutenda pasipo akili (nafsi) kwa maana unasema walidanganywa wote na ibilisi yaani mwili na nafsi?

3. Umejibu kitu ambacho ujaulizwa kukwepa swali kwa nadharia za kisayansi na kibudha, nimekuuliza swali la Mungu wa kwenye maandiko; je ana mwili au hana.
Sikusema walidanganya wote mwili na nafsi nimesema imeuponza mwili na nafsi
...kuhusu mungu kuwa na mwili au la jibu ni kuwa mungu kiasili hana mwili ila anaweza kujifanya kuwa na mwili.tena nataka kukujuza kuwa miili ni kitu feki tu hata sisi binadamu siyo miili ni nafsi hivyo hatujawai kujiona tulivyo bali tunachokiona ni mwili ambao siyo sisi.
 
Muumba hakuumba kuzimu wala jehanam wala ujinini hizo zote zimeundwa na mvamizi (ufunuo,nyoka,vita)
Nachukua maneno yako mawili tu ya mwanzo "Muumba hakuumba.."

..kumbe Shetani naye ni muumba?
 
Sikusema walidanganya wote mwili na nafsi nimesema imeuponza mwili na nafsi
...kuhusu mungu kuwa na mwili au la jibu ni kuwa mungu kiasili hana mwili ila anaweza kujifanya kuwa na mwili.tena nataka kukujuza kuwa miili ni kitu feki tu hata sisi binadamu siyo miili ni nafsi hivyo hatujawai kujiona tulivyo bali tunachokiona ni mwili ambao siyo sisi.
Umesema kiasili Mungu hana mwili? Na je wale waliotuumba sisi kwa mfano wao ni hakina nani? (Mwanzo 1:26)

Hata yule aliyemwonesha Musa mgongo wake naye alikuwa ni nani (Kutoka 33 mstari wa 17:23)

Umesema kile alichokiumba Mungu na kukibariki ikiwemo kukipulizia pumzi yake (yeye Mungu) kuwa ni feki?

Ikiwa nafsi (roho) zinaukamilifu kama inavyonadiwa kwanini zihitaji kujidhihirisha ndani ya miili ambavyo si vitu halisia?

Katika adhabu ya moto wa milele kwa wadhambi kitakacho unguzwa ni kipi kati ya nafsi au mwili?
 
Mbona nimesema kuwa hata sisi siyo mwili japo tunayo migongo tumia akili mungu alipo sema tumfanye mtu kwa mfano wetu wewe unajua alimaanisha nini ? Kwanini unadhani alikuwa anaongelea mwili na si muundo wa nafsi huru yenye akili na utashi na matamanio ...kwanini wewe ukadhani ni mwili na kama ni mwili mbona binadamu tumetofautiana mambo mengi wengine weupe wengine weusi wengine wa fupi wengine warefu sasa huo mfano wa mungu ni umbo gani na sura kama ya nani maana hata sura zetu zipo tofauti..
Kuhusu kuunguzwa ni vyote ila nafsi ndiyo itakayo teseka lengo ni kuitesa nafsi

Kuhusu ufeki mbona hata yesu mwenyewe kasema kuwa nafsi ndiyo uzima mwili haufai kitu ....pia nimegundua ujui maana ya kupuliziwa pumzi ....maana ya pumzi hapo ni kutiwa nafsi nikama kwenye kompyuta kutia Windows (operating systems) =nafsi
 
Ama hakika unazidi kuchanganyikiwa ndugu yangu kwa kumix theories mbalimbali na maandiko ya biblia.

Naona umekazania nadharia za energy na mambo ya vibration, na law of nature unayamix na maandiko kitu ambacho ni bias, unapopokea maarifa mapya unatakiwa ujue wapi pa kuya-apply, ukiwa ni msomaji wa kitabu cha biblia basi rejea ya vifungu itumike siyo tu kujitungia vitu kichwani na kuungaunga idea.

Mungu alituumba kwa mfano wa umbile lake inamaana hata yeye anafanana na binadamu. "...Yesu akawaambia mtu akiniona mimi amemwona Baba" (Yohana 14:8-12)

Unadai mwili ni kitu feki, je Mungu alipoteza muda kufanya arts yake ya kuufinyanga mwili unaofanana na umbo lake kwa udongo kabla ya kuupulizia pumzi ya uhai (nafsi)?

Hapo mwanzo mwili ulipoumbwa Mungu hakuwa na mpango wa kuufanya mwili kuwa kitu temporary na chenye kuoza isipokuwa tu baada ya hukumu ya kifo ndipo mwili ulipoitajika kuwa na ukomo na nafsi pia. (Mwanzo 2:17)

Nafsi ni kitendo cha kupumua kama ulikuwa hujui, na ukifa maandiko yanasema nafsi imeondoka na kumrejelea Bwana aliyeitoa. (Mwanzo 2:7)

Naona unamlisha mpaka Yesu maneno ambayo hakuyaongea, hakuwahi kunukuliwa akidai nafsi ndiyo uzima na mwili haufai kitu.."

Yohana 6:63 ROHO ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu, "MANENO" hayo niliyowaambia ni ROHO, tena ni UZIMA.

NB: Neno la Mungu=Uzima=Roho
 
Wewe ujui unacho sema kuhusu yesu umekosea logic yesu alisema atakufa na siku ya 3 atafufuka ila alipokuwa msalabani anasema leo hii utakuwa pamoja nami pema peponi ...sasa yesu anapesema mwana umaanisha mwili na anaposema baba umaanisha nafsi yake ambayo ndiyo mungu ...hivyo yesu kufasiku 3 ni mwili wake ndiyo uliokufa ila nafsi yake ni mungu hivyo mungu hawezi kufa hata sekunde moja ndiyo maana msalabani anasema leo hii utakuwa pamoja nami pema peponi.

Pia yesu aliulizwa nawanafunzi wake kuhusu kiama kitakuwa lini yeye akasema mwana hajui ila baba kwa kusema hivyo ilimaanisha anajua siku ya kiama maana mwana ni mwili na baba ni nafsi yake....maana yake mwili haujui ila nafsi yakeinajua....ndiyo maana yesu akawaambia anionaye mimi amemwona baba maana hata mimi na wewe hatujawai kujiona nafsi zetu ila tunajiona miili tu hivyo mwili wa kristo ulibeba nafsi ya mungu hivyo ni kweliamwonaye kristo kamwona baba...nakama unabishakwanini yesu asiseme ukijiona wewe mwenyewe umemwona baba? Kwanini aseme ukimwona yeye kwanini siyo binadamu yoyote tumia akili.
 
Aisee huko mweupe sana katika maandiko hivyo haina haja ya kuendelea kubishana kwa kukwepa maswali yangu na kuongeza mambo mengine ambayo ni nje ya mada.

Nilikwambia Nafsi ni nini?

Na Je, nilisemaje kuhusu pumzi hiyo baada ya mwisho wa uhai wa mtu kuwa inarudi wapi?

Kwahiyo unadhani Yesu alikosea nini aliposema kuwa nafsi yake itakuwa peponi (kwa Mungu).

Yesu aliposema atakufa physical siku 3 alimaanisha ni siku tatu kweli na siyo hizo nadharia zako za kuungaunga. Nakusihi tena usiendelee kuunganisha mafunzo ya biblia na mafunzo ya new world.

Yesu anaposema katika Yohana kuwa yeye na baba ni wamoja ajiongelei yeye kama mwanadamu bali analizungumzia NENO LA MUNGU (ROHO)

Anaposema sisi tu miungu na tukimfuata (tukilitimiza kusudio la Neno la Mungu) atatufanya wanawe, hamaanishi tumwabudu yeye (kama tulivyopotoshwa na ulimwengu wa dini za dunia) bali tulifuate Neno la Mungu ndiyo uzima wenyewe au Roho wa Mungu anayeishi nasi (Emmanueli)

Hivyo Yesu ni binadamu aliyetumiwa na Mungu kama chombo kuifikisha sauti yake kwa wanadamu (wana wa Mungu na huyo Yesu akiwa mmoja wao) na wala Yesu si mkamilifu hata aabudiwe isipokuwa anayepaswa kufanyiwa hivyo ni Baba peke yake (Roho mtakatifu). Kiufupi mafundisho ya utatu mtakatifu ni upotoshaji na ni mafundisho ya new world.
 
Shetani sio muumba ni muundaji kinyume.

Tofautisha kuumba na kuunda
Siku nyingine usimpe shetani sifa zisizo zake; aliyeumba ulimwengu kwa ujumla wake na kila kilichomo iwe ni dunia, mbingu, kuzimu, binadamu, majini, uzuri, ubaya, uovu n.k ni huyo huyo Alfa na Omega na kamwe hakitokei kitu pasipo rhuksa yake.

Yaani katika mlinganyo rahisi ni hivi:-

MUNGU= Roho Mtakatifu (Mungu Baba) + Roho Mwovu (Shetani)

NB: Binadamu= alipaswa kuishi upande mmoja wa Roho mtakatifu pindi alipoumbwa ila akachagua kuwa Mungu.

Hivyo Binadamu naye akaingia katika kundi moja la miungu isipokuwa yeye aliwekewa ukomo ambao ni KIFO ili asitaabike milele dhambini kama zilivyo roho zilizochagua upande wa maasi zaidi mf shetani, mapepo n.k

Vita anavyopigana Mungu ni vita vya nafsi (kiroho) na ni dhidi yake yeye mwenyewe, akitaka upande mmoja wa mema utende zaidi ya ule wa maovu. Na hapendi kiumbe chochote alichokiumba kiishi kwa mateso kama aliyonayo yeye (kuwa na mawazo kinzani)

Sasa sisi binadamu tuna afadhali ya laana ya kufa ila kabla ya kufa tuna-option ya kujiunga na Roho Mtakatifu ambayo ndiyo asili yetu (upande mzuri/wa mema ya Mungu) kuliko wale waishio daima wakiteseka katika maovu ambao utamani tuwe kama wao wakitufundisha masomo ya kula tunda la mti wa kati wa mema na mabaya kwa kuvunja codes tukidhania kuwa tunapendwa kumbe ni mtego wa kufanywa kuwa nafsi isiyoonja mauti ambayo uishi daima ikitamani kifo lakini hakitokei.

Rejea: Kitabu cha Mwanzo.
 
Ngoja nikutafsirie ndugu,Muumba aliyekuwepo kabla ya chochote aliumba mbingu na nchi, baada ya moyo wa mwanzo kutekwa na uumbaji ukawa umetekwa ikabadilishwa kuwa dunia na ulimwengu.

Ila Muumba hajaumba dunia na ulimwengu ni walioteka nyara kubadilisha badala ya kuwa mbingu na nchi (nuru) ikawa dunia na ulimwengu (giza)

Nguvu zote za giza zinatokana na kuibiwa kwa nguvu za Muumba alizoweka ndani ya kila mmoja hasa mitume na manabii walioongoza vizazi na majira kuzibadili (kuunda ndo huko) kuwa nguvu za giza.

Hata Mungu mwenye mwanzo na mwisho nae pia aliumbwa, ndo maana ikaandikwa katika 1korintho 15:24-28 mwisho atamkabidhi Muumba kila kitu maana sharti amiliki yeye.
 
Aisee mambo unayoeleza kiujumla hayapo kwenye maandiko zaidi ya stori za kahawa.

1. Baada ya moyo wa mwanzo kutekwa...
(A) Moyo upi huo wa mwanzo?
(B) Liko wapi andiko kuhusu huo moyo wa mwanzo?
(C) Ulitekwa na nani?
(D) Ni andiko gani lina-support hoja yako kuhusu tafsiri ya tofauti kati ya mbingu na nchi kuwa nuru na ile ya dunia na ulimwengu kumaanisha giza?

2. (A) Mungu mwenye uwezo wote kumbe anaibiwa nguvu zake na zinatumiwa bila ridhaa yake?
(B) Kwahiyo muumba ni dhaifu kiasi cha kumwachia majukumu yake Yesu ndiyo apambane na maadui zake ili mwishoni amrudishie crown yake aliyopokonywa?

Ama hakika ukisoma maandiko kama riwaya lazima uangukie pua.

Eti hadi Alfa na Omega naye aliumbwa..! Au mimi ndiyo sijakuelewa?

Mwisho una-quote mistari ya 1Wakorintho 15:24-28 kwanini usisome kifungu chote kuanzia 15 mpaka 28 uelewe vizuri kabla ya kuja hapa kuanika... Anyway kifungu hiki kinazungumzia process ambazo hazipingani na zile zilizoko katika kitabu cha ufunuo juu ya Mungu kumwandaa mwanae wa pekee kama mrithi halali wa kiti cha enzi, hivyo katika 1wakorintho15:24-28 tunapata ufafanuzi wa kina juu ya kile kitakachotokea kabla ya kutawazwa kwake.

Kutakuwa na zoezi la Mwenyezi Mungu kuangamiza maadui wote (rejea kitabu cha ufunuo) na kuweka kila kitu chini ya himaya yake au chini ya miguu yake "hili mwana atukuzwe katika Baba na Baba katika Mwana" ili mwisho lipate kutimia Neno la Bwana kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Yohana.
 
Ukisoma mwanzo 1:1 yule ndio moyo wa mwanzo aliyepewa kusimamia uumbaji au wengi wanamuita mungu ambaye ndie alikuwa alfa na omega yaani mwanzo na mwisho.

Ukatokea utekaji wa uumbaji ndo maana daniel 7:21 akasema hakuna mtakatifu aliyeshinda.

Sababu kulikuwa na wavamizi ufunuo 12:1-9(ufunuo,nyoka na vita) waliokuwa wako juu ya watakatifu wote including Yesu. Ndo maana Yesu akamwambia baba yake katika mathayo 24:22 siku zisipofupishwa zilizoandikwa (ufunuo 20:6) hatapona hata mmoja.

Wengi walikuwa wanaabudu wasichokijua bila kujua (yohana 4:22a) na dunia ilikuwa inaficha kweli isijulikane.

Muumba sio dhaifu, alikuwa mahali pake hakuna anayepajua akisubiri majira na wakati wake ufike aje kutukomboa.

Ndo maana akasema katika (mika 1:2-6) atakuja akitoka mahali pake kuja kuyeyusha vilima na milima (fahamu kinyume zilizotangulia)
 
Wengi tulizaliwa tukifundishwa kuwa tumegawanyika mara tatu yaani (Roho,nafsi na mwili).Habari za moyo zikafichwa zikawa hazifundishwi sana

Ndo maana ikaandikwa katika

2korintho 7:1
Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu.

Lakini hakuna aliyeweza kujitakasa akawa msafi.

Muumba wetu yeye ni Moyo Halisi sio roho, sio nafsi wala mwili.

Moyo maana yake mema na mazuri peke yake.sio moyo huu unaopelekwa India kupasuliwa.

Ndo maana ikaandikwa katika

Mathayo 5:8
Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.

Mithali 4:23
Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
 
Inasemekana kuwa shetani alitupwa kuzimu, kulingana na maelezo yako inathibitisha kuwa duniani ndiyo kuzimu kwenyewe;

1. Kwanini Mungu mwenye upendo amuumbie binadamu kuzimu (mahali pa mateso/gereza) kuwa maskani yake?

NB: Kwahiyo kwa ufupi nilivyoelewa mimi kwa mujibu wa maelezo yako hapo; ibilisi= Malaika muasi au kiongozi wa waasi, Mnyama=Tawala za dunia, na Nabii wa uongo=dini.

2. Umeeleza kuhusu awamu tatu za maasi ambazo naweza kukubaliana nazo kwa kuwa ushahidi wake unaweza patikana katika maandiko lakini umeanza mambo ya ubashiri wa kisabato ya kuhusisha kila kitu na imani, nimeona umeanza kuzungumzia sijui AI na sanamu ya mnyama baadae ikija teknolojia nyingine pia utaendelea na utabiri wako ama?

3. Je, ukiwa kama mzazi mwenye akili timamu unaweza kumfungia adui yako aliyedhamiria kukuua chumbani anakolala mwanao?
Shetani hajatupwa kuzimu, kumbuka kuzimu nayo ni sehemu zinapokaa roho ambazo miili yao imekufa na mwisho wa siku vyote vitaharibiwa. Maana hakuna kufa tena wakati huo.

Ufunuo 20: 14 Mauti na kuzimu vilitupwa kwenye ziwa la moto. Ziwa hili la moto ni mauti ya pili. 15 Na yeyote ambaye jina lake halikuonekana limeandikwa kwenye kitabu cha uzima alitupwa kwenye ziwa la moto.

1. Upendo ni nini? wewe unatafsiri vipi upendo? Je, baba mwenye mtoto anapomuona mtoto wake anakosea huwa anamchekea na kumkumbatia na kumuambia 'umefanya vizuri sana kijana?' endelea hivyo hivyo au je, sio kuwa anampa adhabu? Katika muktadha huo ndivyo Mungu mwenye upendo ana deal na watu pia.

Kumbuka, Mungu hakumuumba mwanadamu ili awe roboti wa kufata kila kitu (vivo hivyo malaika-ndo maana kuna walioasi) Mungu aliwapa viumbe vyake uwezo wa kuamua wenyewe wanataka nini, kumsikiliza au kutomsikiliza!
Maamuzi yote yana matokeo.

Adamu aliamua kwenda kinyume na matokeo yake ni kifo. Kifo cha kwanza kimwili na kifo cha pili ziwa la moto. Lakini kupitia mpango wa Mungu, sasa wewe na mimi tunaeza kupata uhai endapo tutamtii Mungu.

Ezekieli 18: 23 Je, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, nafurahia kufa kwake mtu mwovu? La hasha! Mimi napendelea aachane na njia zake mbaya apate kuishi.

Mungu hataki mtu ye yote aangamie. Anataka wote wafanye toba. Lakini Mungu anatambua kwamba si kila mtu atafanya toba. Ni dhahiri kwamba wengi wataangamia (Mathayo 7:13–14).

2 Petro 3:9, Mungu kuwachagua na kuwavuta baadhi kwa wokovu ni uthibitisho kwamba hakika hamtaki mtu ye yote aangamie. Kama si kwa uchaguzi na mwito wa Mungu, kila mtu angeangamia (Yohana 6:44; Warumi 8:29–30).

Kwahiyo kwa ufupi nilivyoelewa mimi kwa mujibu wa maelezo yako hapo; ibilisi= Malaika muasi au kiongozi wa waasi, Mnyama=Tawala za dunia, na Nabii wa uongo=dini.
Sikutaka uelewe hivyo: Ibilisi=malaika muasi, mnyama=tawala za dunia (sio tawala zote, bali ni zile ibilisi alizozichagua kuunda mfumo wake wa utawala) , nabii wa uongo =dini (manabii wa uongo wapo kila dini, lakini nabii huyu wa uongo atakuja wakati utawala huo wa mnyama utakapokuwa ukitawala, na hatakua katika dini zote, bali dini ambaye mnyama ataichagua kuwa dini ya ufalme wake!)

2. Yawezekana una 'ugomvi' au 'chuki' na dhehebu la kisabato ambalo mimi sio muumini wake na wala sijawahi kuwa muumini wake. Hivyo basi napinga kuwa hayo niliyoandika awali ni "ubashiri wa kisabato". Nakataa!

Kuhusisha kwangu AI na mambo yaliyotabiriwa na manabii/mitume katika Biblia sio utabiri wangu bali ni katika kujaribu kungamua mambo haya. Pia sijasema AI ndiye sanamu ya mnyama, La hasha! bali ni mfano wake wa karibu.

Kama kitu kinatembea, kinatoa sauti na kina tabia za bata basi kwa asilimia kubwa ni bata huyo.
SifaSanamu ya MnyamaAkili Bandia (AI)
Ujuzi wa kibinafsiHupewa fahamu na utambulisho
Uwezo wa akili Inamiliki ujanja na hekima ya kudanganyaHuonyesha uwezo wa ufumbuzi wa matatizo ya hali ya juu
Uwezo wa kuzungumzaInaweza kuwapa pumzi na uhai sanamu ya mnyama wa kwanza, na hata kuzungumza na kuuwa wale ambao hawauabudu.Inaweza kuzungumza na hata kutambua na kutekeleza amri zake,kama vile amri ya kumwua watu wasioabudu.
Uwezo wa kuwabaini watu wanaomfuataAliwalazimisha wote, watu watu wanaomfuata wadogo na wakubwa, matajiri na maskini, watu huru na watumwa, watiwe alama juu ya sura. mikono yao ya kulia au juu ya paji za nyuso zao. Inaweza kutambua kwa kutumia alama za utambulisho kama vile alama za vidole na sura, au digital footprint!
Udhibiti wa biashara na shughuli za kiuchumiUdhibiti wa biashara na shughuli za kiuchumi unamaanisha kwamba akili bandia inaweza kusimamia na kudhibiti shughuli za biashara na kiuchumi kwa kuhakikisha kwamba tu watu waliotiwa alama hiyo, yaani jina la yule mnyama au tarakimu ya jina hilo, ndio wanaoruhusiwa kununua au kuuza bidhaa au huduma.Inaweza kusimamia na kudhibiti shughuli za biashara na kiuchumi kwa kutumia teknolojia ya blockchain au njia nyinginezo za dijitali.

Teknolojia hii ya AI imeendelea kwa kiasi cha kufikia kuwa hatari sana kwa wanadamu. Hata mvumbuzi wake (sio kwa nia ya dini) anaonya juu ya madhara yake (
View: https://www.youtube.com/watch?v=FAbsoxQtUwM). Ukifatilia unaeza kuelewa au unaeza kumsoma Noah Harari na kitabu chake cha Homo Deus.

Ikitokea teknolojia ingine sitatabiri maana hata hapa sijatabiri bali nimejaribu kuonyesha mfanano wa AI na utabiri uliopo tayari!

3. Mfano wako haufanani na uhalisia!
Akili timamu ni zipi? Huyo unayemfungia na mtoto hata usipomfungia atawinda njiani na kufanya aliyodhamiria.

Binadamu 'hajafungiwa' chumbani na 'shetani'. Binadamu yuko huru duniani na yeye ndiye anayeamua afuate dhamira ipi, ya kimungu au kishetani. Shetani mwenyewe hajafungiwa kokote ndo maana tumepewa maelekezo haya 👉1 Petro 5: 8 Muwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze.

Hiki sio kiumbe kilichofungiwa mahala. Zaidi ya yote hayo tunaaswa kuwa Wefeso 6: 10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. 12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. 14 Basi simameni, mkiwa mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, 15 na kama viatu vilivyofungiwa miguuni mwenu muwe tayari kutangaza Injili ya amani; 16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. 17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; 18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote.

Hivyo basi hata kama 'ukifungiwa humo ndani' kama unavosema, bado umepewa uwezo kumshinda huyo adui. Japo narudia tena mfano wako haufanani na uhalisia wa mambo kwa ground!
 
Back
Top Bottom