Inasemekana kuwa shetani alitupwa kuzimu, kulingana na maelezo yako inathibitisha kuwa duniani ndiyo kuzimu kwenyewe;
1. Kwanini Mungu mwenye upendo amuumbie binadamu kuzimu (mahali pa mateso/gereza) kuwa maskani yake?
NB: Kwahiyo kwa ufupi nilivyoelewa mimi kwa mujibu wa maelezo yako hapo; ibilisi= Malaika muasi au kiongozi wa waasi, Mnyama=Tawala za dunia, na Nabii wa uongo=dini.
2. Umeeleza kuhusu awamu tatu za maasi ambazo naweza kukubaliana nazo kwa kuwa ushahidi wake unaweza patikana katika maandiko lakini umeanza mambo ya ubashiri wa kisabato ya kuhusisha kila kitu na imani, nimeona umeanza kuzungumzia sijui AI na sanamu ya mnyama baadae ikija teknolojia nyingine pia utaendelea na utabiri wako ama?
3. Je, ukiwa kama mzazi mwenye akili timamu unaweza kumfungia adui yako aliyedhamiria kukuua chumbani anakolala mwanao?
Shetani hajatupwa kuzimu, kumbuka kuzimu nayo ni sehemu zinapokaa roho ambazo miili yao imekufa na mwisho wa siku vyote vitaharibiwa. Maana hakuna kufa tena wakati huo.
Ufunuo 20: 14 Mauti na
kuzimu vilitupwa kwenye ziwa la moto. Ziwa hili la moto ni mauti ya pili. 15 Na yeyote ambaye jina lake halikuonekana limeandikwa kwenye kitabu cha uzima alitupwa kwenye ziwa la moto.
1. Upendo ni nini? wewe unatafsiri vipi upendo? Je, baba mwenye mtoto anapomuona mtoto wake anakosea huwa anamchekea na kumkumbatia na kumuambia 'umefanya vizuri sana kijana?' endelea hivyo hivyo au je, sio kuwa anampa adhabu? Katika muktadha huo ndivyo Mungu mwenye upendo ana deal na watu pia.
Kumbuka, Mungu hakumuumba mwanadamu ili awe roboti wa kufata kila kitu (vivo hivyo malaika-ndo maana kuna walioasi) Mungu aliwapa viumbe vyake uwezo wa kuamua wenyewe wanataka nini, kumsikiliza au kutomsikiliza!
Maamuzi yote yana matokeo.
Adamu aliamua kwenda kinyume na matokeo yake ni kifo. Kifo cha kwanza kimwili na kifo cha pili ziwa la moto. Lakini kupitia mpango wa Mungu, sasa wewe na mimi tunaeza kupata uhai endapo tutamtii Mungu.
Ezekieli 18: 23
Je, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, nafurahia kufa kwake mtu mwovu? La hasha! Mimi napendelea aachane na njia zake mbaya apate kuishi.
Mungu hataki mtu ye yote aangamie. Anataka wote wafanye toba. Lakini Mungu anatambua kwamba si kila mtu atafanya toba. Ni dhahiri kwamba wengi wataangamia (Mathayo 7:13–14).
2 Petro 3:9, Mungu kuwachagua na kuwavuta baadhi kwa wokovu ni uthibitisho kwamba hakika hamtaki mtu ye yote aangamie. Kama si kwa uchaguzi na mwito wa Mungu, kila mtu angeangamia (Yohana 6:44; Warumi 8:29–30).
Kwahiyo kwa ufupi nilivyoelewa mimi kwa mujibu wa maelezo yako hapo; ibilisi= Malaika muasi au kiongozi wa waasi, Mnyama=Tawala za dunia, na Nabii wa uongo=dini.
Sikutaka uelewe hivyo: Ibilisi=malaika muasi, mnyama=tawala za dunia (sio tawala zote, bali ni zile ibilisi alizozichagua kuunda mfumo wake wa utawala) , nabii wa uongo =dini (manabii wa uongo wapo kila dini, lakini nabii huyu wa uongo atakuja wakati utawala huo wa mnyama utakapokuwa ukitawala, na hatakua katika dini zote, bali dini ambaye mnyama ataichagua kuwa dini ya ufalme wake!)
2. Yawezekana una 'ugomvi' au 'chuki' na dhehebu la kisabato ambalo mimi sio muumini wake na wala sijawahi kuwa muumini wake. Hivyo basi napinga kuwa hayo niliyoandika awali ni "
ubashiri wa kisabato". Nakataa!
Kuhusisha kwangu AI na mambo yaliyotabiriwa na manabii/mitume katika Biblia sio utabiri wangu bali ni katika kujaribu kungamua mambo haya. Pia sijasema AI ndiye sanamu ya mnyama, La hasha! bali ni mfano wake wa karibu.
Kama kitu kinatembea, kinatoa sauti na kina tabia za bata basi kwa asilimia kubwa ni bata huyo.
| Sifa | Sanamu ya Mnyama | Akili Bandia (AI) |
| Ujuzi wa kibinafsi | Hupewa fahamu na utambulisho | |
| Uwezo wa akili | Inamiliki ujanja na hekima ya kudanganya | Huonyesha uwezo wa ufumbuzi wa matatizo ya hali ya juu |
| Uwezo wa kuzungumza | Inaweza kuwapa pumzi na uhai sanamu ya mnyama wa kwanza, na hata kuzungumza na kuuwa wale ambao hawauabudu. | Inaweza kuzungumza na hata kutambua na kutekeleza amri zake,kama vile amri ya kumwua watu wasioabudu. |
| Uwezo wa kuwabaini watu wanaomfuata | Aliwalazimisha wote, watu watu wanaomfuata wadogo na wakubwa, matajiri na maskini, watu huru na watumwa, watiwe alama juu ya sura. mikono yao ya kulia au juu ya paji za nyuso zao. | Inaweza kutambua kwa kutumia alama za utambulisho kama vile alama za vidole na sura, au digital footprint! |
| Udhibiti wa biashara na shughuli za kiuchumi | Udhibiti wa biashara na shughuli za kiuchumi unamaanisha kwamba akili bandia inaweza kusimamia na kudhibiti shughuli za biashara na kiuchumi kwa kuhakikisha kwamba tu watu waliotiwa alama hiyo, yaani jina la yule mnyama au tarakimu ya jina hilo, ndio wanaoruhusiwa kununua au kuuza bidhaa au huduma. | Inaweza kusimamia na kudhibiti shughuli za biashara na kiuchumi kwa kutumia teknolojia ya blockchain au njia nyinginezo za dijitali. |
| | |
| | |
Teknolojia hii ya AI imeendelea kwa kiasi cha kufikia kuwa hatari sana kwa wanadamu. Hata mvumbuzi wake (sio kwa nia ya dini) anaonya juu ya madhara yake (
View: https://www.youtube.com/watch?v=FAbsoxQtUwM). Ukifatilia unaeza kuelewa au unaeza kumsoma Noah Harari na kitabu chake cha Homo Deus.
Ikitokea teknolojia ingine sitatabiri maana hata hapa sijatabiri bali nimejaribu kuonyesha mfanano wa AI na utabiri uliopo tayari!
3. Mfano wako haufanani na uhalisia!
Akili timamu ni zipi? Huyo unayemfungia na mtoto hata usipomfungia atawinda njiani na kufanya aliyodhamiria.
Binadamu 'hajafungiwa' chumbani na 'shetani'. Binadamu yuko huru duniani na yeye ndiye anayeamua afuate dhamira ipi, ya kimungu au kishetani. Shetani mwenyewe hajafungiwa kokote ndo maana tumepewa maelekezo haya 👉1 Petro 5: 8 Muwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye,
huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze.
Hiki sio kiumbe kilichofungiwa mahala. Zaidi ya yote hayo tunaaswa kuwa Wefeso 6: 10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. 12
Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. 14 Basi simameni, mkiwa mmejifunga
kweli viunoni, na kuvaa dirii ya
haki kifuani, 15 na kama viatu vilivyofungiwa miguuni mwenu muwe
tayari kutangaza Injili ya amani; 16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya
imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. 17 Tena ipokeeni chapeo ya
wokovu, na upanga wa Roho ambao ni
neno la Mungu; 18
kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote.
Hivyo basi hata kama 'ukifungiwa humo ndani' kama unavosema, bado umepewa uwezo kumshinda huyo adui. Japo narudia tena mfano wako haufanani na uhalisia wa mambo kwa ground!