"Na yule ibilisi, mwenye kuwadanganya akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele" (Ufunuo wa Yohana 20:10)
Naamini JF siwezi kosa majibu ya maswali haya tafakarishi ninayojiuliza baada ya kukisoma kifungu hicho kutoka katika kitabu cha ufunuo wa yohana 20:10 sababu humu kuna watumishi,waamini, wanatheolojia, na wasomaji wazuri wa biblia wanaoweza kunipatia ufumbuzi wa kifungu hiki ambacho kina vitu vikuu vitatu ndani yake yaani IBILISI, MNYAMA na NABII WA UONGO.
1. Je, upi ni utofauti wa ibilisi, mnyama na nabii wa uongo?
2. Ikiwa ibilisi umaanisha shetani, je mnyama na nabii wa uongo ni akina nani hao kwa mujibu wa maandiko.
3. Je, binadamu anakabiliana na maadui wangapi hapo ni watatu au ni shetani tu?
4. Je, binadamu mwenye hatia atoangukia kwenye adhabu hii ya moto wa milele?Maana kulingana na kifungu hiki vinaonekana viumbe hivyo vitatu tu ndiyo vipo motoni.
5. Kwanini inaonekana kana kwamba mnyama na nabii wa uongo watamtangulia ibilisi kuingia motoni?
Nitajibu maswali yako kwa ufupi (ukihitaji maandiko na rejea usisite kusema)
1.
-Ibilisi ni malaika kerubi aliyeasi kwa kutaka kuwa "Mungu"
-Mnyama ni mfumo wa utawala ambao mamlaka yake yanapewa nguvu na Ibilisi mwenyewe, kama ilivyokuwa Israel ya kale kuwa Mungu ndo mfalme wao basi na Mnyama ndiye vivo hivyo, na kiongozi wake kama ilivyo kwa Yesu Kristo ukuu wa Mungu unakaa ndani yake ndivyo hivyo Mpinga Kristo Ibilisi mwenyewe anakaa ndani yake.
-Nabii wa uongo ni mfumo wa dini utakaokuwa na muonekano wa kimungu ila matendo yake ni ya ibilisi mwenyewe yaani uongo mwingi wenye kuhadaa wote wasio na imani thabiti!
-Umesahau sanamu ya mnyama: kuna uwezekano mkubwa sanamu hii kuwa 'Artificial Intelligence' au akili mnemba. Itakapopewa nguvu ya 'uhai' na kuweza kufanya yale yote ayafanyayo mnyama au Beast! Kuwa macho katika tasnia hii kwani kama mwenye nymba angalijua siku ya kuja mwizi angalikesha na asingeliacha nyumba yake kuvunjwa!
2. Nadhani nimekujibu hapo juu
3. Shetani ndio kinara wa yote hayo. Inakupasa ufahamu kuwa kulikua kuna uasi mkuu mara 3 huko mbinguni. Uasi wa kwanza ni wa Shetani/Ibilisi/Joka na majina yake mengine, aliadhibiwa kwa kuondolewa mbinguni na kukaa duniani mpaka muda wake wa adhabu kufika. Uasi wa pili ulikuwa wa malaika waangalizi walioacha maeneo yao ya kutawala na kuzaa na wanadamu, watoto wao ndio walikuwa 'giants' waliofanya maasi makubwa dhidi ya binadamu. Baba zao yaani malaika waasi walifundisha binadamu maarifa mabaya yote unayoyajua kuanzia kufanya vita, uchawi na ukahaba!. Adhabu yao ilikua ni kufungwa gizani mpaka siku ya hukumu ambako wateule watawahukumu! Watoto wao yaani 'giants' waliadhibiwa katika gharika na baadaye Joshua aliwaondoa katika nchi, wachache waliobaki Daudi na wanajeshi wake waliwashughulikia. Kuna siri hapa!.
Uasi wa tatu ni ule wa malaika waliopewa kutawala kabila za binadamu walipoasi na kuzifanya kabila hizo kuwa waabudu sanamu nk. Kumbuka pale Babeli Mungu alichagua Israel kama taifa ambalo kupitia hilo angekuja kukomboa kabila zote zilizopotea. Uasi wa malaika hawa utatimilizwa siku ya hukumu.
Hivyo panabaki ibilisi ambaye ndiye mastermind wa mpango wake wa kupindua serikali ya Mungu. Mungu alimpa mwanadamu dunia aindeleze na kuitunza. Shetani hapendezwi na hili kwa hio ni adui namba moja wa mwanadamu. Hawezi kumdhuru Mungu moja kwa moja kwa hio anadhuru watoto wake! Jeshi la Ibilisi ni pamoja na makamanda wake alioasi nao pamoja na roho za giants ambazo ndizo pepo wabaya hao kwa pamoja na malaika waliopewa kabila za dunia huunda ufalme wa giza na kutenda yaliyo gizani.
4. Ndiyo binadamu mwenye hatia atakuwa na adhabu ya kutupwa ziwa la moto unaowaka moto wa kiberiti yaani sulphur. Ukijua sifa za sulphur utaelewa japo kwa wastani moto huo, harufu na mazingira yake yakoje. Yai viza lina harufu ya sulphur!
5. Lazima vijakazi waanze kupata adhabu kabla ya mkuu wao kuhitimisha.
Asante