Ipi tofauti ya Ibilisi, Mnyama na nabii wa uongo?

Ipi tofauti ya Ibilisi, Mnyama na nabii wa uongo?

Msaada jamani kwa mwenye uzoefu ama ufahamu wa kutosha naomba nisaidie kujibu hili swali.

Je nitamjuaje nabii wa uongo?

Natanguliza shukrani.
Nabii wa uwongo ni yule anaye toa unabii wa uwongo simple as that
 
Tafakari yafuatayo kumtambua
1. JE, anakuombea upate kile ambacho yeye anachangiwa pesa akipate?
2. je, anaponya wachache? je anaweza kwenda pale hospital na wote wakapona?
3. Je amewah ponya mlemavu wa kuzaliwa? Yaan kiwete toka azaliwe, je anaponya?
4. Je, anaweza kufufua?
5.
6.
7.
8. Usidanganyike
manabii wa ukweli ni wale waliolisha chakula watu wengi na wakashiba, inje ya hapo hamna nabii ila ni viinimacho
 
Biblia Imeandika Haya yote vizuri mno.

UKITAKA kujua ni kusoma Tena vitabu viwili tu.

DANIEL.

UFUNUO WA YOHANA.

HATA SIO MAMBO YA KUUMIZA KICHWA AU MAGUMU. UKISOMA LAZIMA UTAELEWA TU .

TATIZO ndio hivyo hamtaki kusoma
 
Ibilisi ni sheytwan/lucifer, mnyama ni ukatoliki na nabii wa uongo ni Muhamad
Una ushahidi gani wakujustify kauli yako au jaribu kufafanua tafadhali.

Pili kuna utofauti gani kati ya mohamedanism na popery?
 
Biblia Imeandika Haya yote vizuri mno.

UKITAKA kujua ni kusoma Tena vitabu viwili tu.

DANIEL.

UFUNUO WA YOHANA.

HATA SIO MAMBO YA KUUMIZA KICHWA AU MAGUMU. UKISOMA LAZIMA UTAELEWA TU .

TATIZO ndio hivyo hamtaki kusoma

Kwa kuwa unajua unaonaje ukitutegulia kitendawili cha uzi wetu juu ya nani hasa ni walengwa wa majina haya kama biblia ilivyowapa uhusika wa mnyama, nyoka na nabii wa uongo?
 
Ibilisi ni Shetani.

Mnyama ni UTAWALA WA kiselikali, UFALME.

NABII WA UONGO ni MWAMED.
Hapo kwa ibilisi na mnyama kulingana na sources kadhaa inaonekana ni kweli, ila hapo kwa Muhammed bado sikubaliani napo kwanini yeye na si Yesu?
 
no Alie mwongo, huongopa. sio ya kidunia.. Ipo hivi, wa Mungu atakuelekeza kwa Mungu bali wa uongo atakudanganya ili akupeleke kwa shetani
Swali ni kuwa unawatambua vipi ikiwa wote wanapayuka kwa jina la Yesu na wanaonesha kwa dhati kuwa wanaifuata njia iliyo ya haki?
 
Akianza kuuza mafuta na maji na vinginevyo,akianza kuambatanisha maombi na sadaka kwa maandiko ya agano la kale yale ya zamani ku justify utoaji wa sasa!

Akianza kukuambia toa sadaka KWA kuvunja agano tena anasema kabisa roho wa Mungu kasema utoe sh. Kadhaa kwa AJILI ya HILI na lile huyo ni mchungaji,nabii,mtume,shemasi vyovyote vile wa uongo!!!

Hata kama ni huyu mwalimu mashuhuri akisema ambatanisha maombi na sadaka huo ni wizi!


Yesu hakuponya KWA kuambatanisha na sadaka bali walitoa baada ya kuponywa ndio wakaleta shukrani na sio KABLA ya uponyaji kufanyika!!

Paulo anaandika hivi"NIFUATENI MIMI KAMA JINSI NINAVOMFUATA KRISTO!

YESU HAKUWAAMBIA SADAKA KABLA YA KUTATUA MATATIZO YAO WALA HAKUWAAMBIA ETI WAAMBATANISHE SADAKA KATIKA MAOMBI BALI KILA MTU ATOE KWA SHUKRANI KAMA ALIVOBARIKIWA TENA KAMA DESTURI YA WANA WA MUNGU!!!!

HAKUNA KUAMBATANISHA MAOMBI NA SADAKA BALI SHUKRANI KWA JINSI ULIVOGUSWA!!!

KATIKA ULIMWENGU WA AGANO JIPYA NA UKRISTO HAKUNA SADAKA ZA KUAMBATANISHA ILI MUNGU AKUJIBU BALI NI HAPO KALE!

MAHUBIRI YA KUAMBATANISHA SADAKA NI WIZI ULIOHALALISHWA KWA MAANDIKO YA GANO LA KALE ILI KUFUMBA MACHO WAJIBU WA AGANO JIPYA!!!

HIVYO TU YAANI!!!

Kwani neno "Nabii" lina maana gani?

Je, Yesu alijitambulisha kama nani kati ya majina haya; Mchungaji, mtume, nabii au mwalimu?
 
Utamtambua kupitia matunda yake. Je baada ya kuhubiri matunda yake ni yapi? Ni uzima au ni mauti.

Nabii wa kweli huongea neema na uzima kwa wana wa Mungu kwa imani ya Kristo.
Nabii wa uongo huongea habari za hukumu na mauti.

Karibu kwa swali lolote

Kwahiyo wale wanaotuhubiria kuwa tukitenda dhambi tutaishia kwenye hukumu ya moto ndiyo manabii wa uongo?
 
Back
Top Bottom