Ipi tofauti ya Ibilisi, Mnyama na nabii wa uongo?

Ipi tofauti ya Ibilisi, Mnyama na nabii wa uongo?

Hawa wote ni malaika waasi kama Lucifer, kwa hiyo lucifer ndio joka kuu au ibilisi, na hao malaika wawili mmoja anaitwa mnyama, mwingine anaitwa nabii wa uongo, wanaitwa kwa titles zao na lucifer ndio kiongozi wao yeye ndio anawapa nguvu hawa ili kufanya maandalizi ya ujio wake siku za mwisho,

Siku za mwisho wa dunia hawa malaika waasi watakuja duniani na mamlaka zao walizopewa, na wanaonekana kwa macho ya nyama ya kibanadamu, kuja kuendelea kudanganya binadamu watakao kuwa wamebakia baada ya unyakuo.

Huyu mnyama ndio mpinga Mungu au baada kuja kwa Yesu kristo akawa ndio mpinga kristo,.na huyu mnyama ndio anasimama kama falme mbalimbali za hapa duniani, utaona kipindi cha Daniel aliitwa mfalme wa uajemi.
Acha urongo. Reference ipo wapi ya kusapoti hoja zako??

Alafu lucifer sio ibilisi. Usitupange..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tofauti ya Ibilisi, Mnyama na Nabii wa uongo kutokana na vyanzo mbalimbali;

Sehemu ya Kwanza:

IBILISI - katika kiebrania huitwa 'accuser' or 'adversary' mshitaki au mpinzani.
Rejea (waefeso 6:12, chronicles 21:1)

Katika ugiriki diabolos (devil- slanderer to hurl(verb)I.e accusations.
Rejea (Deuteronomy 13:13, 1 samuel 1:16;2, chronicles 13:7) kutoka katika vyanzo vya zamani "dead sea scrolls"
Haimjadili shetani kama muovu katika biblia ya kiebrania bali Belial na siyo shetani hivyo baadae ndipo uhusika wa shetani ulikuja kubatizwa na wayahudi na katika maandiko ya kikristo. Kwa mara ya kwanza neno shetani lilianza kutumika (2 Corinthians 6:15) pale Paulo alipoanza kutofautisha term hii alipokuwa akizungumzia habari za Yesu.

Rejelea (Yohana 12:13) mtawala wa dunia Yohana 8:44 baba wa uongo (2 wakorintho 4:4) mtawala wa nguvu ya upepo (Waefeso 2:2) na beelzebul, mtawala wa mapepo(mathayo 10:25); (Marko 3:22); (Luka 11:15) kwa mujibu wa Yesu (mathayo 12:29), (Marko 3:27),(Luka 11:21-22) 'mwenye nguvu' shetani lazima afungwe kuporwa nyumba yake ambayo ndo hazina(yaani wanadamu)

Je, uislamu unamzungumziaje MNYAMA -( DAJJAL au MPINGA KRISTO)?

Al masih Ad- Dajjah, ndiye mpinga kristo ambaye atajitokeza baada ya nyakati za mwisho za nabii wa Mungu, Muhammad, " Messiah wa uongo, ambaye kila Nabii ametuonya kumuhusu akiwemo Yesu ndiyo maana tunamwita Mpinga kristo."

Dajjal ni mtihani mkubwa aliopewa mwanadamu tokea adamu na hawa walipotua duniani, yeye ni binadamu ambaye atautawala ulimwengu wote, kwa kuwapumbaza wana wa adamu na hawa kuwa yeye ndiye messiah, isitoshe pia atadai kuwa ndiye Mungu.

Dajjali- umaanisha muongo, Mtume Muhammad anawaambia waamini kwamba "Allah ajafichwa hili msimuone, yeye (Allah) siyo JICHO MOJA na ajanyooshewa kidole kuelekea katika jicho lake, akaongezea Al masih mweupe. Ad Dajjal ni kipofu katika jicho lake la kulia na macho yake uonekana kama zabibu inayochomoza.
Neno Kafir( asiye amini) limeandikwa kati ya macho yake mawili(paji la uso).
Mfano ni uwepo wa alama ya jicho moja kwenye US dollar bill, ngazi 13 za pyramid, na neno" In God we trust" ufunguaji wa jicho la tatu nakadhalika.
Biblia inasema "huu ni wito wa hekima. Kila mwenye fahamu afanye mahesabu ya nambari ya mnyama, kwa sababu ni namba ya mwanadamu. Na hiyo namba ni 666. (Ufunuo 13:18)
Hivyo basi uonapo kiashiria chochote kwenye logo, michoro, brand,television, show nakadhalika yenye jicho moja, 666 na msalaba uliogeuzwa juu chini zote zinamwakilisha mpinga kristo " k.f.r"

Mtume Muhammad alitabiri juu ya uwepo wa illuminati ambao pia umwabudu ibilisi(Lucifer), na jini liitwalo Dajjal, "mwana wa ibilisi" na wanasubiria kuja kwake kama ulivyo ujio wa messiah Yesu utakavyokuwa.
Umeelezea vizuri, baadhi ya mambo, ila mengine bado yana walakini. Umeenda mbali kufafanua chapa ya mpinga kristo, jambo ambalo ni la faida kwa wengine.

Ila Mnyama, Na vingine ambavyo mtoa uzi huu anataka kuvijua hujavigusia...kama ambavyo vimegusiwa kwenye waraka wa ufunuo wa yohana..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sehemu ya Pili: uchambuzi wa maandiko

Wakati wa ujio wa kristo, mpinga kristo ndiye kifaa kilichotumiwa na shetani kueneza uongo lakini kitakamatwa na kutupiliwa kwenye ziwa la moto. Sasa shetani naye atajikuta katika hatima hiyohiyo.
Shetani hapo kabla alikuwa ameshatupwa nje ya mbingu mpaka duniani (ufunuo 19:9+) rejelea baada ya ujio wa pili (ufunuo 20:2+) alitupwa katika hitimisho la ziwa la moto(mathayo 25:41) (ufunuo 12:41) (ufunuo 18:2)(Isaya 34:8-17) na wakorintho 15:24-28 na 15:24)

(Ufunuo 20:13) na (ufunuo 14:10-11) Hukumu ya dunia- maadui watatu wamekwisha pinduliwa na kufukuziwa mbali toka katika dunia ambayo walipania kuiharibu (ufunuo 11:18) hukumu ya mwanadamu yafuatia. Ufunuo 20:7-10 pia 19:20 pia ufunuo 20:1-3 kisha linganisha na ufunuo 16:13-14.

Vipi ni vitu muhimu vilivyogusiwa au kuzingatiwa katika ufunuo 20:9-10

I. Uamuzi wa mwisho ulifikiwa na kutolewa kuliokoa kanisa la kweli la Mungu dhidi ya ukatili na ubatili wa kishetani.

II. Ufunuo 20:9 Kushindwa rasmi kwa nguvu za shetani na jeshi lake lote.

III. Kufutiliwa mbali na kutokuwepo tena kwa maadui wa kanisa na Mungu (ufunuo 19:20) linganisho na 20:1-3) shetani sasa, kama adui wa mwisho atakumbwa na adhabu sawa na maadui wote waliokwenda kinyume na kanisa- katika namna mbalimbali za Kipagani, mohammedanism, popery na delusion.
Hawa wataharibiwa milele. Hapo ndipo dunia itakapotawaliwa na amani. Kanisa litapumzika, na ushindi mkuu utakuwa umepatikana.

IV. Ustawi na mwanzo mwema (ufunuo 20:9-10)(ufunuo 20:11-15) linganisha na somo toka (Luka 17:26-30) (Luka 18:8) (1thessalonike 5:2, -5:3:2) na (Petro 3:3-4)

Sehemu ya Tatu: Uchambuzi wa maandiko

UTATU USIYO MTAKATIFU

a) Mnyama- alianza kupokea nguvu na utawala wake kutokana kwa joka au shetani.

b) Nabii wa uongo au Mpinga kristo kulingana na wajibu wake usivyotofautiana sana na "Mnyama" ambaye ni mpinga kristo kupitia nguvu zake za ushawishi, ambaye kuja kwake ni matokeo ya kukamilisha kazi ya shetani, pamoja na ishara na miujiza ya uongo.

Utatu usiyo mtakatifu(unholy treanity) ni matokeo ya shetani kumwiga au kumwigiza Mungu ilikujifanya kana kwamba ndiye Mungu) ufunuo 12-13

Utatu mtakatifu= Baba, Mwana(Yesu kristo) na Roho Mtakatifu.

Na mpinzani wake yaani utatu usiyo mtakatifu ni Shetani(Mpinga Mungu), Mnyama(Mpinga Kristo) na Nabii wa Uongo(Mpinga Roho Mtakatifu)

Sifa za Roho mtakatifu; ni upendo,wema na ukweli. Na sifa za utatu usiyo mtakatifu udhihirisha kinyume chake yaani udanganyifu,chuki na maovu yasiyo na kipimo.

Ufunuo 12:3 "joka kuu jekundu" great red dragon 'yenye dhihirisho la wasifu wa mwenye hila na muuaji.'

Japo vifungu mbalimbali vya biblia umwelezea shetani katika namna tofauti, mfano joka au malaika wa mwanga, ameelezewa katika ufunuo 12:3 kama joka kuu jekundu mwenye vichwa saba na pembe kumi, na mataji saba katika vichwa vyake.
Rangi nyekundu ni ashirio la uasi na mauaji. Vichwa saba uwakilisha tawala ovu saba ambazo shetani ameziwezesha na anazitumia tokea mwanzo kuzuia na kudhibiti juhudi za Mwenyezi Mungu zisizae matunda. Miongoni mwa tawala hizo tano ni Misri, Assyria,Babiloni,Medo-persia na Ugiriki.

Ufunuo 12:4 kumbuka walitaka kumuua Yesu wakati wa kuzaliwa kwake na himaya ya sita yaani Rome ambayo bado ina-exist wakati wa unabii huu. Chini ya utawala wa kirumi mfalme herode aliua watoto wachanga wote. Ukiangalia katika kitabu cha Daniel ukurasa wa 2 mataji yale saba umaanisha moja kwa moja kuwa na nguvu juu ya dunia au kuitawala.

(Ufunuo 12) shetani na theluthi ya malaika zake walifukuzwa.
(Ufunuo 12:4) Malaika mkuu mikaeli na malaika wengine wakapigana vita na shetani na mapepo wake na shetani ataondoshwa kutoka mbinguni milele (ufunuo 12:7-9) pia soma (ufunuo 12:6,13-17), (mathayo 24:15-21)

MNYAMA au MPINGA KRISTO, anaelezewa katika ufunuo 13 na Daniel 7

Sifa na maana zake;

a) Anaelezewa akiibuka kutoka baharini "umaanisha watu wa mataifa"

b)Ana vichwa saba na pembe 10 "uashiria muunganiko wake na kutawaliwa na shetani"

c) Pembe 10 "serikali moja ya dunia ikifanana na himaya tano zilizopita za babiloni,medo-persia,ugiriki,Misiri na hata rumi.(ufunuo 13:2,Daniel 7:7,23)(ufunuo 13:3) Ataumizwa vibaya mnyama yule kwenye jeraha ila shetani atamponya(ufunuo 13:3- 17:8-14) baada ya tukio hili wataanza kumwabudu shetani na mpinga kristo (ufunuo 13:4-5) atamkufuru Mungu na kujitukuza, nakujikweza kama Mungu ili aabudiwe. Ufunuo 13:4-7; Mathayo 24:15) tukio hilo litafahamika kama abomination of devolution (kufuru kuu isiyo sameheka"

Mwisho ni NABII WA UONGO (ufunuo 13:11-18)
Sifa na maana zake;

a) Anaelezewa akichomoza katika nchi "utabiri unahusu ujio wa myahudi toka Israeli. Atajifanya mpole,mstaarabu na mtu mwema."

b) Pembe "uashiria kuwa atakuwa na nguvu" Yesu amekwisha onya (mathayo 7:15)

c) Uongea kama Joka "ataongea kwa ushawishi na kwa udanganyifu kuwafanya wanadamu wamwache Mungu na kugeukia ibada za kumwabudu mpinga kristo na shetani(ufunuo 13:11-12) atafanya ishara ya maajabu ikiwemo kushusha moto kutoka mbinguni (ufunuo 13:13) ataweka picha ya mpinga kristo iabudiwe, kuipa picha uhai, kutaka watu wote waisujudie na kuwahukumu wale wote wakataao kuiabudu.(ufunuo 13:14-15)
(Ufunuo 20:4) inathibitisha kuwa njia ya hukumu itakuwa ni kuwanyonga.

Nabii wa uongo pia atafanya kila mtu apokee chapa ya kudumu kama walivyofanyiwa watumwa nyakati za yohana, kuonesha kumuunga mkono Nabii wa uongo na kwenda kinyume na Mungu, ni wale tu wenye chapa hii watakao ruhusiwa kufanya biashara. Kukubali chapa hii umaanisha kupokea kifo cha milele(ufunuo 14:10) ukikubali siyo tu unakubali mfumo wa kiuchumi bali unaabudu na mfumo uliomkataa Yesu Kristo.

(ufunuo 13:18)inatufunulia namba ya mnyama ya kuwa ni 666

Na hakuna ajuaye kuwa maana kamili ya namba hii ni nini hasa.

Huu utatu usiyo mtakatifu utawayumbisha waamini na kudanganya walio wengi, matokeo yake ni kuwapelekea katika kifo cha milele. Lakini ufalme wa Mungu utadumu. Rejea (Daniel 7:21-22)
 
Acha urongo. Reference ipo wapi ya kusapoti hoja zako??

Alafu lucifer sio ibilisi. Usitupange..

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa nakubari ni uongo, lete wewe huo ukweli wako,.ila kwa msomaji wa biblia atakuwa amenielewa,.si vibaya ukasoma kitabu cha Daniel na ufunuo kimefananua vizuri tu, utaona nilichokoeleza.
 
Kivipi ebu itetee hoja yako kwa mifano au ufafanuzi kidogo
Sio warumi tu, iko hivi kuna tawala za dunia nyingi zimepita ikiwepo warumi, sasa kilichopo ni kwamba huyo mnyama ndio yuko nyuma ya hizo utawala, yaani ukifungua pazia nyuma ya mtawala wa dunia utamuona huyo mnyama,
Ndio maana katika kitabu cha Daniel, nabii Daniel alionyeshwa hizi tawala katika image ya wanyama ambao ndio uhaliasia wa wa tawala hizo tofauti ya mfalme nebkadreza ambaye yeye alionyeshwa sanamu ya mtu , Daniel alionyeshaa wanyama tofauti tofauti kila tawala kwa style za kutawala zilikuwa kinabadilika kwa kila tawala, sasa tuko katika utawala wa warumi ndio unaendelea kufika mwisho.
 
Sio warumi tu, iko hivi kuna tawala za dunia nyingi zimepita ikiwepo warumi, sasa kilichopo ni kwamba huyo mnyama ndio yuko nyuma ya hizo utawala, yaani ukifungua pazia nyuma ya mtawala wa dunia utamuona huyo mnyama,
Ndio maana katika kitabu cha Daniel, nabii Daniel alionyeshwa hizi tawala katika image ya wanyama ambao ndio uhaliasia wa wa tawala hizo tofauti ya mfalme nebkadreza ambaye yeye alionyeshwa sanamu ya mtu , Daniel alionyeshaa wanyama tofauti tofauti kila tawala kwa style za kutawala zilikuwa kinabadilika kwa kila tawala, sasa tuko katika utawala wa warumi ndio unaendelea kufika mwisho.
Je, umepitia pia nakukubaliana na fafanuzi nilizokusanya kutoka katika maandiko mbalimbali? Je, suala la dini zote tunazoabudu leo hii bila kujalisha madhehebu kumwabudu shetani kupitia mpinga kristo unalizungumziaje au nipe mtizamo wako.
 
Soma Biblia na uielewe kwa msaada wa Roho mtakatifu. Vinginevyo ni ngumu kuwatambua,japo ni rahisi kusema utawatambua kwa matendo yao. Binafsi nawajua vzr na hawanisumbui.
20230213_125746.jpg
 
Msaada jamani kwa mwenye uzoefu ama ufahamu wa kutosha naomba nisaidie kujibu hili swali.

Je nitamjuaje nabii wa uongo?

Natanguliza shukrani.
Nabii wa uwongo ni yule anaongea na kutenda mambo yaliyo tofauti na kitabu kitakatifu, kulingana na mwelekeo wake muislam/mkristo.

Kwahiyo fuata maandiko na sio mtu, hata padri/ shekh akiongea tofauti na maandiko usimfuate.
 
Aliye wa Mungu huzungumza habari za Mungu tu. Aliye muongo huzungumza mambo ya kidunia.

Imeisha hiyo.
 
Back
Top Bottom