Ipi top 3 yako ya nyama tamu?

Ipi top 3 yako ya nyama tamu?

Kitimoto ni kiboko we bwana wewe acha kabisa. Hivi umeshawahi kusikia wapi kijiwe maalumu kwaajiri ya nyama aina moja tu. Yaani mdudu ukienda Bar au pub anajiko lake pekee yake.

Na anaweza kuwa na jiko lake pekee yake mtaani na akapata wateja balaa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
salam!!!
wale wazee wa misosi ipi top 3 yako ya nyama tamu
ya kwangu hiyapa

1. Kuku
Asee huyu ndege hadi leo binafsi naona nyama yake haina mpinzani yani hana mbadala yani nyama iwe mchemsho rosti choma au ya kukaanga nitamu zote nadhani sote tunafahamu jinsi supu ya kuku ilivyo tamu

2. Ng'ombe
Akitoka kuku anafata ng'ombe huyu myama nae yupo vizuri lakini huyu utamu wa nyama yake una depend na maufundi ya mpishi. laini na yeye nyama yake iwe mchemsho rosti choma au ya kukaanga nitamu zote

3 Kitimoto
kwangu huyu namba yake inashika namba 3 kwasababu tu nyama yake inanoga tu kwa rosti na kukaanga lakini mchemsho wake hahaha hapana asee

hiyo ndo top 3 yangu ya nyama tamu Je ya kwako ni ipi?

NB: Kuku anautamu wa asili tu yeye haitaji ata ufundi wa mpishi....
Samaki choma
Digidigi choma
Dondoo roast
 
1. Samaki alietoka majini akachomwa/banikwa na ugali wa mhogo
2. Kitimoto( ilitakiwa aanze basi tu)
3.Mbuzi choma.

Kuku na Ng'ombe nawapenda pia.

Japo nasikia ya binadamu ni noma,ukianza uachi - pengine inatumika zaidi sema hawa mazombi kuwaona kazi.
 
Back
Top Bottom