Profit_Habari
New Member
- Oct 24, 2021
- 2
- 1
Huduma za pesa mtandao kupitia simu za mkononi ni eeneo ambalo katika sekta ya uchumi linatajwa kukua kwa kasi sana kwenye huduma za kifadha kwa njia ya mtandao.
Ripoti ya mwaka 2019 iliyotolewa na tasisi ya kimataifa ya GSMA Intelligence ilionyesha kuwa Tanzania ni mojawapo ya mataifa ya Afrika ambapo huduma za fedha kupitia simu zimekua kwa kasi.
Akaunti za pesa mtandao kupitia simu za mkononi zimeongezeka kutoka 17,639,349 Desemba 2015 hadi 25,864,318 Desemba 2019; ongezeko la asilimia 46.6.
Kukua huku kumewezesha watumiaji wengi kujumuika katika mfumo wa kifedha ama kwa kutuma au kupokea fedha, kufanya miamala mbalimbali kielektroniki kupitia simu za mkononi na pia kumepanua fursa za ujasiriamali.
Huduma hizo hutolewa na mitandao mbalimbali ya simu kupitia mawakala, lakini changamoto imekuwepo kwa baadhi ya maeneo huduma za kifedha za mtandao Fulani kukosekana hasa maeneo ya vijijini, mteja kulazimika kusafiri umbali Fulani ili kuifuata huduma hiyo jambo ambalo humgharimu fedha na muda.
Kwa sasa mfumo uliopo unawezesha mteja kutuma au kupokea pesa kutoka mitandao mingine na sio kutoa.
Wakati mwingine hulazimika kuwa na namba ya mtandao Fulani ili kwaajili ya huduma za kifedha za mtandao Fulani jambo ambalo ni gharama nyingine.
Tofauti na wananchi, pia Mawakala hulazimika kusajili laini za uwakala za mitandao yote inayotoa huduma za kutuma ua kupokea pesa kwa lengo kuhakikisha anawapata wateja wa mitandao yote.
Changamoto hizo zingeweza kumalizwa endapo pangekuwepo na huduma ya kutoa, fedha kupitia mfumo huo bila kujali aina ya mtandao unaotumia.
Mfumo huo ungeunganishwa na mifumo ya mitandao ya simu zote zilizopo nchini na itoe ruhusa kwa mtumiaji wa laini ya simu ya mtandao wowote kupata huduma ya kifedha ya uwekaji, utumaji au utoaji wakati wowote ilimradi tu awe na pesa kulingana na mahitaji yake.
Pia ingewarahisishia mawakala wanaotoa huduma za pesa katika mitandao ya simu kutolazika kuwa na laini za uwakala za mitandao yote inayohitajika, hivyo ingewapunguzia gharama.
Pangekuwepo na Mfumo huo wakala angepunguziwa muda na gharama za Kutafauta usajili wa kila laini kulingana na mtandao husika anaouhitaji.
“Kama ikishindikana mitandao ya simu inayotoa huduma za kifedha waboreshe huduma zao kwa kuruhusu huduma ya kutoa fedha kutoka mtandao mwingine kwa kupitia Mawakala”
Kwa mujibu wa taratibu za nchi Masuala ya fedha yanasimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania; lakini TCRA inahusika kama msimamizi wa sekta ya mawasiliano na mitandao, ambamo miamala ya kifedha inapitia kwa Pamoja wanaweza kulitazama hilo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Profit Mmanga
Email: prottemmanga@gmail.co

Attachments
Upvote
1