Kaka, kuna kitu kinaitwa nationalism au uzalendo. Hii humaanisha mtu anakuwa na upendo wa nchi yake kuliko nchi nyingine. Inapotokea raia wa nchi yake ameuawa katika nchi ya ugeni hupata huzuni isiyo kifani na hata huwa tayari kufanya lolote ile alipize kisasi cha jama yake (his countryman) kuuawa.
Mfano. Kama Serikali yetu ingetaka kulipiza kisasi cha kuuawa kwa Joshua Mollel, kama taarifa za kuuawa kwake ni sahihi, ingeingia vitani dhidi ya Hamas kwa sababu ya kumuua mtanzania na siyo kwa sababu Hamas wanaua raia wa nchi zingine. Hivyo sioni kosa kwa watanzania wenzangu kuumizwa na kitendo cha Joshua Mollel kuuawa.