Ipo siku Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama atatoa Siri za nchi kwa maadui, Sabaya katufungua macho

Ipo siku Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama atatoa Siri za nchi kwa maadui, Sabaya katufungua macho

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Mkuu wa Wilaya Ni mwenyekiti wa ulinzi na Usalama, unapokuwa na DC anayeweza kumchafua au kutoa Siri za Rais na viongozi wa juu kwa public kisa tu amebanwa kwa makosa aliyoyatenda ipo siku au yawezekana hata Sasa baadhi ya Taarifa za nchi hazipo salama.

Most of DC na RC wamepewa hiyo kazi kwa sababu ya uanachama wa chama flani siyo kwa kuangalia qualties. Tuliaminishwa kwamba wanatunza Siri ila naamini tumeona kwa sabaya kwamba tuna umuhimu wakurudisha adhi ya DC na RC kwa watu wenye vifua vya kuhifadhi mambo. Na hii lazima TISS waweze kumshauri Rais na walipaswa kuona hii weakness toka zamani.

Tusipokubali kufanya kazi za Utumishi wa Umma tofauti na siasa tutauza nchi. Assume Sabaya alivyokuwa anatoa amri kwa polisi nao wanatekeleza, anabeba silaha hakuna Intel anayeingilia wote wamekaa kimya Leo hii kabanwa na kikesi kidogo tu kaanza kuwataja waliokuwa wamemfadhili. Tusipojirekebisha wakina Siro wakaendelea kuwa controlled na wanasiasa tutapoteana.
 
Tunza siri, nenda Jela waliokuwa wanakutuma ipo watakutoa na kukupa majukumu mengine ambayo pengine sio ya public.
Kutunza siri ndio msingi wa tawala za kidunia.
Kwanini ulimpeleka jela in the first place....siku nyingine Wajifunze kufanya vetting
 
Tunza siri, nenda Jela waliokuwa wanakutuma ipo watakutoa na kukupa majukumu mengine ambayo pengine sio ya public.
Kutunza siri ndio msingi wa tawala za kidunia.
Mimi siamini kama JPM alimtuma huyu dogo kwenda kufanya jinai,huyu anampakazia Magu kwa vile hayupo duniani kumjibu huu upumbavu wake. Na tukumbuke kuwa Sabaya alianza uhalifu siku nyingi hadi kufoji kitambulisho cha TISS ili kujipatia hela kwa njia za kitapeli.
 
Huko TISS kwenyewe wamejaa hao hao makada uchwara wa CCM. Bila Katiba Mpya nchi hii inaelekea shimoni kabisa. Lawama zote kwa JK ndiye katuachia huu msala wote
Kuna watu wanajifanya kutaka mabadiliko, ila katiba mpya hawataki kuisikia hata ikitamkwa tuu[emoji1787][emoji1787][emoji1787].ni unafiki ulio pitiliza
 
Tusubiri Katiba mpya ije hivi vyeo vifutwe na visiwepo, tanganyika mtakuwa na mfumo wa mangavana wa kuchaguliwa na wananchi na zanzibar hakutakuwa na dc wala rc wala hakutakuwa na mikoa wananchi watachagua madiwani kuwa viongozi wa serikali za mitaa ambao wataongoza shehia tu
 
Huyu jamaa kumbe mwepesi sana.sio mtu wa kazi kama alivyokua anajitunishaga mbele ya waandishi wa habari.Kesi kidogo tu kaanza kuongea yote hayo.huyu akibananishwa vizuri ataongea mambo mengi sana.
 
Mkuu wa Wilaya Ni mwenyekiti wa ulinzi na Usalama, unapokuwa na DC anayeweza kumchafua au kutoa Siri za Rais na viongozi wa juu kwa public kisa tu amebanwa kwa makosa aliyoyatenda ipo siku au yawezekana hata Sasa baadhi ya Taarifa za nchi hazipo salama.

Most of DC na RC wamepewa hiyo kazi kwa sababu ya uanachama wa chama flani siyo kwa kuangalia qualties. Tuliaminishwa kwamba wanatunza Siri ila naamini tumeona kwa sabaya kwamba tuna umuhimu wakurudisha adhi ya DC na RC kwa watu wenye vifua vya kuhifadhi mambo. Na hii lazima TISS waweze kumshauri Rais na walipaswa kuona hii weakness toka zamani. Tusipokubali kufanya kazi za Utumishi wa Umma tofauti na siasa tutauza nchi. Assume Sabaya alivyokuwa anatoa amri kwa polisi nao wanatekeleza, anabeba silaha hakuna Intel anayeingilia wote wamekaa kimya Leo hii kabanwa na kikesi kidogo tu kaanza kuwataja waliokuwa wamemfadhili. Tusipojirekebisha wakina Siro wakaendelea kuwa controlled na wanasiasa tutapoteana.
TISS wenyewe ni wanachama wa chama,shida ni kuchanganya maswala ya kitaalam na uchama,mabadiliko yaanzie juu
 
Kama vipi wangemlinda...Yaani mtu akafie jela kisa kutunza siri? Ulitaka ajitetee vipi na ameshtakiwa?
Kuna mission unatumwa kufanya lakini ukikamatwa waliokutuma hawausiki, na kuwataja ni kosa. Unachotakiwa kufanya ni kujitetea na wao watakuwa kwa nyuma, hata jele unaweza kwenda baada ya miaka 2 au 3 kesi inafufuliwa upya na unashinda, unapumzika kidogo then unarudi kwenye V8 kama kawa. Kama VP alikutuma, inamaana alikuamini unakomaa kiume hawezi kukusahau.
 
DC mstaafu pamoja na hiyo kesi inayomkabili aelezee kidogo sakata la risasi dhidi ya Tundu Lissu.
 
Back
Top Bottom