Wauaji mnajitokeza wazi. Na ninyi ninlazima mumwone muuaji mwenzenu kama shujaa wa karne.
Ila jambo moja mkumbuke, hamtaipata hiyo nafasi tena. Na kwa uhakika, kadiri siku zinavyoenda uovu wa shujaa wenu na wa kwenu utazidi kuwekwa wazi. Na siku zijazo, watu watatamani hata kaburi lipigwe pingu kama ilivyokuwa wakati wa mkoloni, marehemu akipatikana na hatia, anahukumiwa. Kama umehukumiwa kufungwa miaka 10, mnyororo utafungwa juu ya kaburi kwa miaka 10. Baada ya miaka 10, utafunguliwa kuashiria kuwa umemaliza kifungo.
Huyu hatakuwa tofauti na Stallin aliyeliliwa na mamilioni ya Warusi baada ya kufa. Miaka 13 baadaye, uovu wake uliwekwa wazi, watu wakakasirika, wakaiondoa maiti yake iliyokuwa karibu na maiti ya Lenin, na kwenda kuitupa kusikojulikana.
Itunze hii moyoni: siku zitakavyoenda, ndivyo uovu wa marehemu utakavyozidi kuwekwa wazi na kujulikana kwa wengi.