Sehemu fulani uko sahihi na sehemu nyingine umefikiri visivyo! Samia alivyomchagua P. Mpango katikati ya uongozi bila kuwepo uchaguzi mbele yake ni tofauti kabisa na Magufu aliyepaswa kuwa na mgombea mwenza ambae ataenda nae ktk uchaguzi. Kumbuka kumpata Samia kama mgombea mwenza kwa mara ya kwanza, Magufuli hakuwa mwenyekiti wa chama wala hakuwa Rais. Kifupi ni kwamba kwa mazingira yaliyopelekea kupatikana kwa Magufuli Kama mgombea wa urais kupitia CCM, JPM hakuwa na nguvu kwenye chama. Nguvu alikuwa nayo Kikwete kama Rais na mwenyekiti wa chama. Hivyo Uhuru wake wa kuchagua mgombea mwenza anaemtaka yeye haukuwepo, japo yeye ndiye aliyekuwa akiwajika kumtangaza. Kumbuka Lowassa alivyofyekelewa mbali pamoja na ushawishi aliokuwanao.Mgombea uraisi akishachaguliwa na kutangazwa anamteua mgombea mwenza.
Kama kweli huyo Magufuli alikuwa na hayo mnayoyaita maono angemkataa Samia kwakuwa alijua kikatiba ikitokea Raisi kafa basi makamu wake anaapishwa kuwa Raisi wa nchi (na ndicho kilichotokea).
Ni sawa na kusema Leo hii ikitokea Raisi kafa basi makamu wake Mpango anaapishwa kuwa Raisi. Akivurunda mtamtwisha lawama mama Samia au sivyo? Maana baada ya yeye kuapishwa kuwa Raisi akamteua Mpango kuwa makamu wake wa Raisi. "Kwa fikra yako wewe imajini Mpango awe Raisi wa nchi itakuwaje"!!?
Magufuli ndiye aliyesababisha wabunge wengi wa Bunge hili linalolalamikiwa na walio wengi kuwepo pale Bungeni. Leo hii Bunge linaonekana halifai nani alaumiwe kama sio yeye? Maana ni Bunge lake kwa utashi wake aliona ni sahihi kufanya vile alivyofanya.
Hii ndio legacy aliyotuachia Magufuli.
Unafiki na ulalamishi na uzandiki na wizi na uvivu wa kufanya kazi na kufikiri na lawama zisizo na msingi zimetutawala na zitatutesa hadi siku tukiamua kutumia akili zetu sawasawa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ktk uchaguzi wa mara ya pili, Magufuli hasingeweza kumchaguwa mgombea mwenza mpya ili kusilete mpasuko ndani ya chama wakati kuna uchaguzi mbele yao. Hesabu za siasa si nadharia kama unavyotaka wewe.
Unasema alijuwa kuwa akifa makamu atakuwa Raisi?!! Unachekesha, wewe binafsi unajua utakufa lini? Urithi kwa familia yako ulisha andaa? Mdogo wangu, kifo ni fumbo la Mungu, hakuna ajuae atakufa lini. Ndiyo maana ulipoongelea hilo la wabunge aliowapitishapitisha kiolela uku umati wa vijana ukimshangilia, alikuwa hana habari na kifo. Alidhani atachagua bunge litakalomsaidia kupitisha mambo yake ya hovyo bila kuulizwa wala kuhojiwa. Pili alikuwa na mpango bunge lake hilo butu libadilishe katiba ili liondoe ukomo wa kugombea kiti Cha urais baada ya mhula wa miaka kumi. Angejuwa ana kufa, hasingeyafanya hayo.