Mwamba JPM, alitikisa Dunia, nayo Dunia ilitikisika. Mwamba aliwika na ssuti yake ilisikika haswaa.
Mwamba aliipenda Tanzania na Watanzania wote.
Mwamba alikuwa tishio kwa mabeberu, walarushwa, wezi na wazembe katika kazi za umma.
Ushujaa wa pekee aliotuonesha Mwamba ni pale alipojua kabisa kwamba Kiongozi yeyote wa Afrika kujaribu kutetea Rasilimali za Nchi yake ni sawa kabisa na kuvaa kitanzi shingoni mwake, lakini yeye hakurudi nyuma hata kidogo.
Kwa kifupi kabisa ni kwamba, JPM alipambana mpaka tone lake la mwisho bila kusalimu amri.
Ndo maana utakuta lile GENGE la mafisadi linajaribu kupambana naye, lakini unafika wakati wanashindwa, kwani Mungu hawapendi wanafiki.