Mkuu
Gidbang , sababu ya CCM kutawala Tanzania milele, sio mfumo wa elimu au ugumu wa maisha, sababu pekee ni kuwa CCM sio tuu ni chama cha siasa, CCM ni chama dola!, ni dola!.
CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola!
P
HAPA Mayala umeongea ukweli mchungu! CCM Mimi nasema sio chama Cha siasa ni chama Dola CCM ni Dola na nimewahi kutoa mifano kadha wa kadha!
Hakishiki madarka KWA Sababu kinakubalika na wananchi au kimekidhi matarajio ya wananchi la hasha KWA Sababu kimejifungamanisha na dola "vanguard party" sio huo ushuzi alioandika mwashambwa Lucas!
CCM na dola ni kama Chanda na Pete! Nilinde nikulinde, ndio mana almost viongozi wote WA dola wamejifungamanisha na CCM, Wana hofu angalia viongozi wa taaisis za kidola wanaoteuliwa katika nafasi za kisiasa na au kugombea nafasi za sisasa Baada ya kustaafu!
Naungana na P kuwa CCM ni dola na dola ni CCM , ukiona upinzani umeshinda ni kwa Sababu tu ya hisani ya CCM au aibu ya wasimamizi!
Kumbuka kule HAI yule kamanda alimwambia FAM asilani unadhani utamshinda? Hiyo ni dhahiri kuwa CCM ni dola na dola ni CCM.
Nenda kwenye latina ya CCM usome muundo wa kamati ya siasa ya mkoa na wilaya, halafu uende nafasi ya mkuu wa mkoa katika kamati Hiyo halafu angalia wakuu wa mikoa ambao ni viongozi wa majeshi!
Kwahiyo kama alivyisema yule marehemu mama kule Zanzibar kuwa CCM haiwezi kuondolewa kwa makaratasi ni sahihi kutokana na hayo kuwa Kura haimui ushindi wa Ccm
Kama alivyosema Nape Nauye tutashinda hata kwa bao la mkono ni dhahiri kwamba ni ngumu kuitoa CCM kwa kutumia sanduku la Kura !
Wakati wa uchaguzi mdogo kule Kimara aliwahi kusema kada mmoja, wapigeni tu wapinzani kwa Sababu polisi ni wetu na mahakama ni zetu, ni wazi kwamba CCM imejifumgamanisha na dola ni ngumu kabisa kwa kupitia Kura ikapatikana mbadala wa chama tawala nakuunga mkono Mayala!
Kama alivyosema marehemu jiwe kuwa hawezi kukuteua akupe mshahra, nyumba na gari halafu umtangaze mpinzani kuwa ameshinda na BADO akuvumilie, ni dhahiri kwamba CCM haiwezi kukubali kushindwa hata kidogo na haitashindwa miaka mia moja sio kwamba inakubalika la hasha inasimama kwa mkono WA dola!
Dr Bashiru aliwahi kutamka mwenyewe kuwa ikiwa unashindwa kutumia dola kuwa madarakani au kutumia Hiyo advantage ya dola kuwa madarakani BASi una matatizo! (Sio nukuu halisi) huu ni ushahidi Tosha kuwa CCM unatumika dola kuingia madarakani na kutetain madaraka!
CCM Ina waadhibu wasioichagua kwa kuwanyima maendeleo ambayo ni hali Yao kama walipa Kodi na hili alifanya wazi wazi marehemu jiwe na kuwafananisha wapinzani na watoto wa kambo namagunzi! Lakini pia dola imetumika kuwatia nguvuni na hata kuwabambikia kesi ukiacha kuwaua wakosoaji au wapinzani wa Ccm Ili kuwatia hofu wengine na waiunge mkono CCM , Hivyo kwa nature ya Tanzania CCM itatawala hata milele ispipokua patokee kizazi jeuri kilichichoka na kufanya mapinduzi halisi ! Rejea watu wanaishinda kesi na rufaa Baada ya hata kuhukumiwa maisha . Au hamumkumbuki Afande kingai na amepewa zawadi ya cheo?
CCM inatumia Rushwa kwa jina la mlingula na takrima au shkrani kuwarubuni wananchi na hapo hapo inalindwa na vyombo cya dola ikiwemo takukuru, rejea sakata la ununuzi wa madiwani na Nassari akapeleka ushahidi mahakamani lakini mahakama na polisi wakaubatilisha haraka Ili kuilinda CCM.
CCM na bingwa wa reforms hasa anapopata pressure kutoka ndani na nje! Ni chama Cha matukio ya kuzima vugu vugu kwa kujibadili haraka jambo ambalo hufanya wapiga Kura wasahau mabaya yake yote.
Narudi CCM itakua madarakani sio Sababu ya kupendwa au kuhudumia vyema na wananchi ni kwa Sababu ni chama dola na dola ni CCM na imejifumgamanisha!
Kwako P