Iramba ni nyumbani kwa Mawaziri watatu lakini inazidi kudorora!

Iramba ni nyumbani kwa Mawaziri watatu lakini inazidi kudorora!

Kwa maana hiyo ana influence kubwa sana kwa jimbo letu kupiga hatua. Anaweza fanya tu kama Mwendazake alivyofanya Chato isipokuwa yeye sio lazima aanzishe mbuga ya wanyama au kujenga uwanja wa ndege. Kuna mengi anaweza kuyafanya na matokeo yake akaweka legacy - kwa sasa hana legacy yeyote!
Tatizo la wanyiramba, mnyiramba akipata pesa kidogo au kazi nzuri anahamia town kama wahaya na kusahau nyumbani, pia wanyiramba wengi ni wazembe wanapenda sn pombe za kienyeji(nturu kama sikosei), hivyo Mwigulu huwa anawanunulia pombe wanampitisha maisha yanaenda kirahisi sn.
 
We unasema Iramba vipi kada ya ualimu je.
Kada ya ualimu ndio utoa nusu ya viongozi wote kuanzia raisi, mawaziri hadi wabunge na wanazijua shida za walimu tena kwa kuziishi wakiwa walimu.
Lakini umewahi ona wamewakumbuka walimu? Hapana,hulka ya mswahili huwa akumbuki alipotoka hasa akishapata.
So sio ajabu kwa hao mawaziri
 
Unatakaje?
Yaani Mwigulu Nchemba, Dorothy Gwajima na Kitila Mkumbo waelekeze Iramba raslimali zote za wizara zao, kwa kuwa wewe na wao mnatokea huko!!?
Mawaziri hao watatu wanasimamia raslimali za taifa, hawatatenda kinyume na kiapo chao.
 
Uwaziri sio issue ,ivi mna wabunge wangapi watishe tu hao wabunge kuwa mwakani unajipanga kugombea basi utaona faida yake atakulipa hata mshahara ili usigombee nafasi hio na maendeleo pia mtayaona alimuradi atawanyamazisha na mtaridhika kabisa ,lakini waziri hao hawana faida.
 
Prof. Kitila Mkumbo kwa Mwaka 2025 nina uhakika hana lake Jimbo la Ubungo.

Mwaka 2020 aliingizwa kibabe na hangeshinda. Dr. Dorothy Gwajima - Mnyiramba wa Tarafa ya Shelui naye anaonesha kunogewa na siasa - hakika atagombea Jimbo la Iramba. Dr. Mwigulu Nchemba (Mamba Kinani) ameendelea kujiamini na kujijenga katika siasa za Kitaifa kwa sababu Jimboni hana tena mpinzani.

Wabunge wa kweli Iramba hawataki siasa wapo kimya - sio kuwa wana hofu lakini pia wamevaa utashi wa dhati ya mioyo yao. Hawataki mgawanyiko.

Sasa hawa wabunge ambao wote ni Mawaziri kuna maendeleo yeyote wanaweza kujivunia kuiletea Iramba? Prof. atasema ooooohhhh yeye ni wa Ubungo lakini tunajua moyo wake upo Iramba ila kiwiliwili ndiyo kipo Ubungo. Hakika imeshapita miezi saba sasa tangu hawa watu waingine uongozini lakini hamna chochote ambacho angalau kinaonesha nia njema waliyonayo kwa Iramba.

Dkt Mwigulu anataka ifike 2023 ndiyo aanza kuchacharika kuwahadaa wananchi. Prof. Kitila vipi mbona wakati hujawa Waziri Jimbo la Iramba ndiyo ilikuwa mahali pako pa kutalii?

Imekuwaje tangu upate ubunge wa kupachikwa na Mwendazake Ubungo na Uwaziri huo huku Iramba umepashit kabisa! Tukueleweje? Au ndiyo ulitaka tu kututumia kama ngazi? Hauna tofauti na Dkt Mwigulu!

Dr. Dorothy Gwajima nina uhakika ukipunguza mbwembwe kidogo tu 2025 unachukua hili Jimbo. Ninakufahamu vizuri na wewe ninajua unanifahamu vema ukisoma tu hapa utajua ni nani kaandika. Njoo mwka 2025 Iramba inakuhitaji - ili ufanikiwe anza mapema - kama ambavyo uliibadili Hospitali ya Wilaya yetu ikawa ya viwango wakati upo kama incharge hapa nina uhakika wewe una cha kujivunia Iramba kuliko hata Dkt. Mwigulu. Anza sasa - weka mipango murua na ufanyie kazi ili Jimbo hili liwe lako mwaka 2025 tuachane na hao wenzio wenye ndoto za URais kila kukicha.

Ninawashauri wote - kama mtaendelea kuwa kimya bila kuiongelea Iramba hakika mkianza mwaka 2023 tutajua fika mnaanza kujipendekeza ili mkubalike 2025. Sisi tunataka muanze sasa, mgombane sasa kwa kuoneana wivu huyu kaahidi hiki, yule kaahidi kile, huyu kaleta kile, yule kawaleta wadau wa maendeleo wale.

Anzeni kugombania nafasi mapema ili jimbo letu lichangamke! Acheni kuogopana nyie Wanyiramba!
Kila kukicha wanapambana kumwangusha Lissu. wana maana basi hao.
 
Tatizo la wanyiramba, mnyiramba akipata pesa kidogo au kazi nzuri anahamia town kama wahaya na kusahau nyumbani, pia wanyiramba wengi ni wazembe wanapenda sn pombe za kienyeji(nturu kama sikosei), hivyo Mwigulu huwa anawanunulia pombe wanampitisha maisha yanaenda kirahisi sn.
Huu ni uwongo wa mchana kweupe. Wanyiramba so wazembe ukilinganisha na Wanyamwezi na watu wa Tanga na Wazaramo!
 
Huu ndio Ujinga was Watanzania!
Ya Ngoswe mwachie Ngoswe

Sisi tunawatazama tu maana Waziri wa Fedha alikuwa na uwezo wa kuhakikisha Iramba (safari hii) madeni yote ya watumishi (hasa walimu) yanalipwa kwa kuyapa kipaumbele.

Mistake hii ikijirudia itakuwa ni second time Mwigulu kupata nafasi golini na kushindwa kufunga goli

We're just watching it very clearly and sensitively!!
 
Mkuu kuanzia Kilimanjaro mpaka Manyara umewahi kuona nyumba ya tembe?
Kilimanjaro zipo ingawa ni kwa uchache - nenda maeneo ya kule Chekereni na kwa mbele yake hata kuja huku Same mpaka Hedaru zipo nyingi tu za kumwaga. Manyara hata usiseme - manake hamna tofauti na Singida. Arusha nenda Longido na Simanjiro zipo za kumwaga tu. Usitufanye sisi hatuifahamu Tanzania.
 
Huu ndio Ujinga was Watanzania!
Ila hako ka slogan kako kana maana kweli. Mungu Wetu ndiye champion wa demokrasia kaumba hata Kiumbe Shetani ili ampinge yeye! Sisi ni akina nani hadi tukatae kupingwa?
 
mlamlalamikia nani kama mnaleta wabunge bogus. Gwajima utasema waziri sasa yule au comedian
Ila HAKI YA MUNGU TENA, Gwajima sio sisi tumemchagua ingawa pamoja na ucomedian wake anaweza 2025 akatufaa Zaidi kuliko G'wigulu!
 
Lyambalyani 😆..ktk kipindi Cha miezi 3 umeanzisha Thread humu kumhusu Mwigulu ,unazikumbuka na maudhui yake???Hebu zirejee tena urudi utuambie hapa wewe unasimamia Nini!
Ila Kama hujamaliza kuvuna nenda Kwanza shamba!🤒🤒
 
Hawa Ndio kwanza wamepewa vyeo na ni lazima bosi wao wamridhishe ili wawe sehemu ya anaowaamini.

Sidhani kama kwa sasa wanawazia majimbo, wana ilani ya kurasa 303 inawategemea wao. Huyo Mkumbo ndio mtafsiri halisi wa Tanzania ya viwanda.

Gwajima anapigwa vijembe kwamba haiwezi wizara akili yake ipo kazini. Mwigulu anajikita katika kuununua upendo wa Mzee JK na Rais sidhani kama anawazia jimbo kwa sasa.
 
Back
Top Bottom