Aliyekuambia Waziri,au Mbunge analeta maendeleo jimboni,alikudanganya,
Waziri yoyote hawezi kujiamulia kwamba Mimi kijiji Changu lazima nipeleke umeme,zahanati,shule,Waalimu,balabala,hivi vitu ni sera,vinaamuliwa na baraza la mawaziri,na watendaji wa wizarani kwa kuangalia vipaumbele,na kugawa kila sehemu ya nchi ipate,Arusha,na Moshi hazikuendelea kwa vile mawaziri na wabunge wenye hasiri ya huko,"walipereka"maendeleo,wao wabunge na mawaziri hawakupereka Mali,walionyesha njia,vision na kutoa uongozi,wakawaweka wananchi pamoja,shule zikajengwa,kwa nguvu ya wananchi na wafadhili,biashara zikaanzishwa,wafanyabiashara wakapata usaidizi wa karibu kutoka kwa viongozi,na mambo yakatokea,
Mbeya,Kagera walifanya hivi pia.
Mkitegemea Hao viongozi wenu watakuja kujenga zahanati na shule,na huduma za maji kwa pesa yao ya mifukoni mtasubili mpaka Yesu Arudi