Kwani huwa zinaingia kwa kuruhusiwa? Ukiona matangazo mengi ujue hawana uwezo wa kuzuia, hivyo wanatumia vitisho. Wakiwa na uwezo hawawezi hata kutamka, wanashambulia moja kwa moja. Unaona jinsi Israel anavyofanya huko Iran? Hatoi kauli yoyote, anazidi kushambulia tu kimya kimya.
Umeandika ujinga ukidhani kuwa kila mtu humu ni mjinga kama wewe.
Look bro, kama wewe huwa haufatilii habari ili kukwepa kuumia roho kutokana na mashambulizi makubwa yanayofanywa na Iran nchini Israel basi jua kuna tunaofuatilia kila kitu kuhusu Israel na Iran.
Waziri wa ulinzi wa Israel ndio mtu wa kwanza kwa kulia lia kwamba Iran inatumia cluster (mabomu ya kutawanyika)
na kusababisha vifo kwa raia (hapo anaficha vifo vya wanajeshi) na uharibifu mkubwa wa majengo na miundo mbinu. Juzi juzi baada ya Iran kushambulia eneo lao la Nuclear, Benjamin Netanyahu alilia kama mtoto mdogo na kudai kwamba aliwambia mapema Ulaya kwamba Iran ina makombora ya kuweza kufika Paris, London, Berlin nk.
Hivyo akaziomba nchi hizo ziungane na vita yao ili kupambana na Iran. Na hiyo kauli ya kuomba msaada haijaanza leo, imekuwa ikitolewa hata na Trump mwenyewe. Sasa kama una akili kamili unaweza ukajiuliza inakuaje mtu mwenye nguvu aomba msaada wa kupambana na yule asiekuwa na nguvu.
yani mtu mwenye nguvu kama Mike Tyson anaweza kweli kumuomba msaada Mayweather amsaidie kuja kupambana na Mandoga? Hiyo inaingia akili? Kwa kawaida siku zote mnyonge ndo huomba msaada wa kupambana na mwenye nguvu ndo maana leo ukisikia Mandonga kaomba msaada wa kupambana na Tyson hautoshangaa kutokana na nguvu alizonazo Tyson, ila ukisikia eti Tyson ndo kamuomba Mayweather msaidie kupambana na Mandonga wewe mwenyewe utakataa kwamba haiwezekani mwenye nguvu Tyson aombe msaada kwa ajili ya mnyonge Mandonga. Hivyo hivyo kwa Iran yenyewe ina uwezo wa kupambana peke yake na ndomaana inawachapa kimya kimya na sio iichape nchi moja. Bali inatembeza kichapo kwa Israel, Saudia, Kuwait, Bahrain, Dubai, Jordan, Marekani nk. Tena kila siku bila kusita wala kuchoka. Hebu pata picha kama Israel imeenda kuomba msaada kwa Marekani ili ije kumsaidia kupambana na Iran ndo ingeingia kwenye vita yenyewe na Iran bila msaada wa Marekani, halaf Iran ikapata msaada wa kijeshi kutoka Russia au China leo hii hali ingekuaje pale Tel Aviv?
Fikiria mpaka sasa hivi, Iran imesema kuwa majengo ya shughuli za kiraia yaliyovunjwa nchini Iran ni 82,000. Hiyo idadi haijumuishi infrastructure za kijeshi. Israel haipigi kelele, yenyewe ni kushambulia tu, ukiona wanatoa kauli basi ni kutoa taarifa ya maangamizi ambayo tayari wamefanya. Iran inatanguliza maneno, na mara nyingi yanaishia kuwa maneno. Sasa hivi mashambulizi dhidi ya Israel yanatoka zaidi kwa Hezbollah kuliko toka Iran.
Usijifanye umesahau kuwa sheria ya Israel hairuhusu raia kupiga picha au ku report taarifa za shambulio. Lakini pia hata vyombo vya habari haviruhusiwi kuandika habari ambazo hazijathibitishwa na serikali. Hali inayopelekea watu kukosa taarifa za kweli kutoka nchini humo. Hilo liko wazi na wew mwenyewe unalijua vizuri. Lkn kwa vile umeamua kuchagua upande, basi umeamua kujianika humu ili kula mtu ajue kuwa wewe ni muegemeaji unaeandika tu ilimradi uufurahishe moyo wako na kuwahadaa wachambuzi uchwara wenzako
NB: Watawala waijiwe na hekima, vita ikome, ili maisha ya watu yaokolewe. Hakuna vita iliyo na faida. Hata anayeshinda, lazima madhara ayapate.
Mwenye hekima mpaka hapo ni yule alievamiwa. Hivyo waliovamia kama wanataka hekima waache kushambulia ili wasishambuliwe.
Kama kufungua mlango tu wa streit of hormuz imekuwa changamoto kwao hadi kuomba msaada NATO, na nchi zingine ziwasaidie. Unafikiri wataweza vita na nchi ambayo ipo tayari kupambana na nchi zote za mashariki ya kati jumlisha Israel na Marekani tena bila kuchoka?