Nato ni nani wewe au US huwezi kushindana na Mtu yuko kwenye ardhi yake bila kupata support ya Saud Arabia na jiran zake. Saud Arabia hawezi kuhatarisha maisha yake kwa moto wa Iran. Kwa kutumia hizo carries ndio hawamuwezi kabisa Iran sababu atazizamisha zote
kobaz acha kujifariji. huyo iran unayemsifia, juzi alipiga simu kwa marekani kuomba pooo simu haikupokelewa, akakimbia mbio hadi Qatar kuwaomba waongee na Marekani manake yeye simu hazipokelewi. hawajaishia hapo, wametuma ujume India, kwamba kwasababi India ni rafisi wa Israel (wa india ni rafiki kwa mbali wa Iran kwasababu ya uadui wa india na pakistan) kwamba india iongee na israel ili wasiwapige. wameishia tu vitisho kwamba wakipigwa watapiga pakubwa. ila wanajilaumu kwa nini walirusha zile. why? kwa sababu Israel anachofanya ni kupanga zana za ulinzi kudaka mabom yaani amepewa muda wa kuweka mambo yake sawa alafu anapiga.
atapiga wapi? mpango wa kwanza ni kupiga kituo cha nuclear enrichment ambacho kwa miaka mingi mno Iran wamekuwa wakikijenga, kupiga kisiwa cha uzalishaji mafuta ambacho leo hii Iran wameonekana wakiondoa baadhi ya mitambo, na kupiga kituo cha kuzalisha umeme. maeneo hayo yakipigwa, iran imerudishwa nyuma miaka rundo kiuchumi na itashindwa kuendesha nchi. tangu juzi wananchi wa iran wamejaa ATM kuchukua pesa na kuzibadilisha kuwa dola ya kimarekani in anticipation ya kukimbia nchi iwe rahisi wakiwa wakimbizi, ATM hazina pesa huko iran. shughuli za kiuchumi haziendi kwa amani na uchumi unashuka, ndio maana kamaumesikiliza hotuba ya ayatolah leo amesema "adui anapigana nasi vita ya kiuchumi, kisaikolojia na kimwili". trauma wanayoishi nayo huko haina mfano na hasa kwasababu marekani ameiruhusu Israel kupiga jambo ambalo miezi ya nyuma hakufanya.
Marekani ina vituo vya kijeshi kuzunguka iran yote, saudia na nchi za kiarabu zinategemeana na Marekani sana, watampa anga. huwa wanadanganya kwamba hawatampa anga ili iran ajisahau halafu wanampa, kwasababu ni maadui wa iran washia. vita ikianza, jua UK, ufaransa, Ujerumani na nchi zingine zitaingia pia. UK kwa sasa wana zana za kutungua rocket za mionzi (razor) ambazo wanampango au inawezekana washazipeleka Israel.
kwa kifupi, tuombe Mungu Israel asipige vibaya, au hata akipiga iran ichuchumae kimyaa ili vita isiendelee kwasababu watakaoumia ni waafrica, maisha yatapanda sana. na kama haujui, kuna uwezekano mkubwa hata jordan na waarabu waliambiwa waziache tu hizo rocket karusha juzi zidondoke israel kwasababu marekani na israel walikuwa na bado wanatamani sana iran aingie kwenye vita kubwa ili waisambaratishe kabisa kabisa.
hifadhi huu uzi, kuna siku utaurudia kujikumbusha wakati iran itakuwa iraq ya sasa.