Iran kunazidi kufuka moshi, kamanda adungwa kisu na kufa kwenye maandamano

Kwa hiyo US waliongea na huyu dada alieuawa asifunike kichwa chake ili askari wamuue, then US hao hao wakawaambia askari wamuue huyo Dada ili maandamano yalipuke?.
Hii dhana ya kila migogoro US anahuska ina fanya kizazi chetu kiwe inferior.
 
Popoma
 
Wasiokuwa na Akili timamu watakuambia mgogoro huu imesababishwa na marekani
Wewe unayejitoa ufahamu ndio hauna utimamu wa akili. Hivi unakataa kabisa tena mchana kweupe kuwa Marekani hahusiki hapo?!

Marekani lazima ahusike na yeye ndie hutoa sapoti kwa vi' NGO uchwara ambavyo hutumika kuchochea uchafuzi wa kiitikadi kama huu kwa kisingizio cha utetezi wa haki za binadamu.

Hapo Kenya ana sapoti NGO's kibao cha kutetea uchoko. Hapa Tanzania pia ameweka mabavu. Yote hii ni kutengeneza base ya watu zaifu ambao atawatumia katika kudhoofisha sovereignty ya mataifa changa au yale yanayopiga hatua kwa kasi.

Ili taifa lolote liendelee linahitaji kuwa na msingi wake wa kimaadili na kiutamaduni wa tofauti ambao utatumika kujenga jamii ya aina yake itakayojisimamia kwa misingi yake hiyo kuweza kupiga hatua za kijamii, kisiasa, kiuchumi na teleology.

Sasa marekani yeye kwa misingi yake ya kibepari ni sumu kuona taifa lingine linaamka na kuja vizuri maana hii itamuathiri yeye miaka ijayo katika influence yake Duniani kama superpower nation. So anafanya kila awezalo kudhoofisha mataifa mengine kwa ndani.

Ona mfano hivi, Iran wanasheria zao kuhusu mavazi why huyu dada aamue kuyakiuka na anajua kuwa kuna hizo sheria. Hapo marekani ndio anapenda kuona hivi mataifa yasiyolingana nae kiitikadi yanapopata machafuko.

Hanatofauti na mwanamke ambaye ametumia ujana wake wote akifanya ukahaba, umalaya na udangaji sasa umri umeenda anaanza kuona hawezi tena kuwa na ndoa, familia wala mume sasa alitazama marafiki zake, ndugu, wadogo zake wapo ndoani anapatwa na husuda na maumivu plus gere. Anashinda kucha kutwa akitafuta namna za kuwafarakanisha na kuharibu ndoa zao ili na wao waharibikiwe na kuwa hovyo na maisha ya nje ya ndoa kama yeye.

Marekani pamoja na mazuri yake mengi ila ana UPUMBAVU mwingi sana anafanya na itakuja mgharimu mbeleni atapotezwa vibaya sana.
 
Hizi dini tunakoenda zitakuja kudharauliwa amini usiamini maana zingine zinasheria ngumu na za kinyanyasaji na wala si Mungu kaziweka ni watu walio shiba mihogo huko ndo waliziongeza kutoka kwenye mila zao sasa wanataka kila mtu azifuate
Naliona hilo, huo upuuzi wa kuminya haki za watu kwa mgongo wa dini unafikia kikomo muda si mrefu. Kwa Dunia hii iliyoelimika na kustaarabika hatuwezi kuendelea kushikilia haki za wengine na tukabaki salama.
 
Ukute wewe ndiyo huna akili timamu..Arab spring ilikua kazi ya marekani,ikakwama Iran na syria
Duuu!!!!
Ina maana huyu dada ametumwa na marekani? Kwasababu shida sio kuachia nywele zake wazi shida ni POLISI kumpiga Hadi kufa,kama asingekufa kusingekuwa na maandamano sometimes tunamfanya marekani kama MUNGU wa dunia hii yaani kila kitu yeye ndiyo muhusika
 
Kwani Arab spring ilianza vipi!?..mtu alijitia Moto Tunisia,marekani aka-capitalize
 
Ni utaahira uliotopea kutafuta mchawi Kwa changamoto zinazoziksbili nchi husika , kila kitu western ,Huu ni mtindio WA ubongo kabisa
 
source?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…