Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Mataifa ya Uturuki na Iran yapo mbioni kutengeneza meli kubwa za kijeshi zitakazobeba droni kushambulia adui badala ya zile meli zilizozoeleka na zinazohofiwa ambazo huwa zinabeba ndege za kijeshi kama vile F-16 na F 35.
Tofauti na meli za kubebea ndege za kivita,meli hizo zao la ubunifu wa Uturuki na Iran zitakuwa zikiongozwa kutoka nchi kavu na kutokea ndani ya meli hizo.Droni kutoka meli hizo zitakuwa zinashambulia adui akiwa majini na nchi kavu na baadae kurudi kwenye kituo chao.
Wachunguzi wa kijeshi kutoka mataifa ya Ulaya na Marekani wamesema athari ya meli hizo kijeshi zinaweza kuwa kubwa kuliko hizi meli za sasa zilizozoeleka.
Marekani iliwahi kuinyima Uturuki vifaa na teknolojia ya kumalizia meli yake ya kivita iliyokusudiwa kubeba ndege za F 35.Hapo Uturuki ikaifanyia mabadiliko meli hiyo kuweza kubeba ndege waliyoibuni wenyewe pamoja na droni zao maarufu za Byraktar.