City Thunder OKC
JF-Expert Member
- May 4, 2025
- 6,655
- 13,097
Mkuu uongo unategemea na mapenzi yako yalipo, pale mapenzi yako yalipo ukisikia uongo utaona ni ukweli na pale ambapo hayapo ukisikia ukweli utahisi uongo.Kuna chungu cha uongo kuzidi Israel na washirika wake? Au we unafikiri kama kweli wangekuwa wanaweza kuingia wanavyotaka leo hii Iran ingekuwaje? Juzi tu katika yale maandamano yangefanikiwa kuitoa Serikali madarakani wangeingia na kupiga kila sehemu ya ile nchi ila ndiyo hivo mahesabu yalienda kombo.
Turudi kwenye mjadala. Unamaanisha kuwa israel haijaingia Iran na kushambulia? Sijakuelewa vizuri hadi sasa
Unasema wangeshambulia Iran ingekuwaje? Hivi unajua Iran ilipoteza vingapi kutokana na ile vita ya siku 12? Unajua kuwa kuwa fordow, Isfahan na natanz palikuwaje? Unajua ni mamia ya Askari wangapi walifariki?