Iran ni nchi ya maajabu sana

Iran ni nchi ya maajabu sana

6 Pack

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2022
Posts
2,819
Reaction score
5,996
Wakuu vipi, kwema.

Wakuu Iran ni mmoja kati ya nchi ambazo ziliwekewa vikwazo vikali na nchi za magharibi toka mnamo mwa miaka ya 70s huko hadi leo hii na siku zijazo.

Vikwazo hivyo ni vya kiuchumi, kijeshi nk, tena vimekuwa vikiongezwa siku hadi siku.

Tofauti na ilivyo kwa nchi nyingine kama vile Cuba, Venezuela nk zilizowekewa vikwazo pengine na marekan tu, au baadhi ya nchi za magharibi. vikwazo vya Iran vimewekwa na nchi za magharibi kama zote wakishirikiana na makampuni ya nchi hizo.

Lakini cha kushangaza Iran imeweza kuwa na uwezo hasa wa kijeshi sawa au pengine zaidi ya ule wa nchi ambazo hazijawahi kuwekewa vikwazo na nchi hizo.

Iran ni miongoni mwa nchi zenye eneo kubwa na watu wengi barani Asia, so pamoja na vikwazo vya kiuchumi walivyowekewa takriban miaka 50 na zaidi, lkn wameweza kuwa na mifumo mizuri ya kudhibiti hali ya umasikini nchini mwao, tofauti na nchi kama Venezuela ambazo vikwazo vya miaka miwili au mitatu vimesababisha mamilioni ya raia waishi maisha ya shida na ya umasikini kupita maelezo.

Pamoja na vikwazo vikali vya magharibi hasa kwa upande wa mambo ya ulinzi, lkn bado nchi hiyo imeweza kuonesha kuwa haipo chini au nyuma kijeshi hata siku moja. Wengi tuliona jinsi wa Iran walivyoziangamiza ndege zisizo na ruban zilizokuwa zinatumiwa na Marekan kupima upepo katika eneo lao, wengi tuliona jinsi Iran ilivyozilipua meli ambazo zilikuwa zinabeba wapelelezi mbali mbali wa magharibi karibu na eneo lake, wengi tuliona jinsi Iran ilivyoshambulia kambi kadhaa za Marekani kule Iraq na kusababisha maafa na uharibifu mkubwa katika kambi hizo baada ya Mmarekani kumuuwa mmoja wa maofisa wakubwa wa Iran kule Iraq, tena kabla ya kufanya mashambulizi hayo wa Iran walitoa taarifa mapema kuwa watalipiza kisasi kupitia kambi za wamarekan kule Iraq, so marekan ikajiandaa kuzuia shambulizi lkn mwisho wa siku shambulizi likashindikana kuzuilika na kuleta maafa kwa jeshi la nchi hiyo kubwa duniani.

Wengi tulishuhudia jinsi Iran ilivyotoa msaada wa silaha kwa kundi la hezbullah ambalo liliichachafya Israel inayopata msaada mkubwa wa fedha kutoka Marekani kwa ajili ya ulinzi wao. Hiyo ilikuwa mwaka 2006 hadi jumuiya ya kimataifa ikaingilia kati na kuomba ipatekane suluhu ya kudumu baina ya Israeli na hezbullah.

Wengi tulishuhudia jinsi Iran ilivyosimama na kumlinda Asad wa Syria katika vita vyake, hadi kupelekea mipango ya Marekani na nchi za magharibi kumng'oa imeshindikana.

Wengi tunashuhudia sasa jinsi silaha kidogo tu za ndege zisikuwa na rubani za Iran zinavyofanya uharibifu mkubwa, na kusababisha maafa makubwa na zaidi ya yale yaliokuwa yanafanywa na Russia kupitia silaha zake mwenyewe (Russia) huko Ukraine.
Mpaka Marekani na nchi zingine za magharibi zinapiga kelele, maana silaha zinazotumika sio zile za Russia ambazo zilikuwa zinampa jeuri raisi wa Ukraine kuona kwamba sasa vita vimekwisha.

Hata zile himars za Marekani sasa hivi zinaonekana hazifanyi kazi mbele ya maangamizi ya ndege hizi za Iran.

Sasa tujiulize, kama nchi iliyowekewa vikwazo na mataifa makubwa duniani kwa zaidi ya miaka 50 bado ina uwezo iliyo nao leo, sasa je kama isingewekewa vikwazo kwa miaka yote hiyo 50 leo ni nchi gani ambayo ingeitisha pale Asia na hata duniani kwa ujumla.

Hizo nilizosema hapa ni zile silaha ilizotoa kuwawezesha hao niliwataja washinde mapambano yao, hapo hatujazungumzia silaha zake mwenyewe alizoweka kwa lengo la kujilinda ambazo kwa sheria za kijeshi duniani huwa zinafanywa siri kubwa ili adui asizione.

Mpaka sasa Marekani na nchi za magharibi zinashindwa kujua ni njia gani nyingine ya kumdhibiti huyu mtemi, maana wamarekani waliwahi kumtumia msaudi mwaka jana, hapo hapo Iran hakuchelewesha akaangamiza mitungi yake mikubwa ya kuwekea mafuta mpaka saudia na dunia ikapiga kelele.

Hili taifa ni la maajabu sana, japo lina maadui wengi lililotengenezewa na nchi za magharibi na halipati msaada wa kifedha kutoka kwa nchi yoyote lkn bado linajiamini kupita maelezo.

Mti wenye matunda ndio hurushiwa mawe, namaanisha ukiona nchi za magharibi na vibaraka wao wanapambana kwa hali na mali dhidi ya uchumi na ulinzi wa kijeshi wa nchi moja, basi jua kwamba wamagharibi hao wameshagundua kwamba nchi hiyo ni hatari maradufu kwa mustakabali wa uchumi wao pamoja na ulinzi wao.
 
Yule jenerali wao aliuawa kinyama sana na drone ya us
Ya ile ilikuwa ni ambush, yan shambulizi la kushtukiza. Lkn Iran yenyewe ilitoa taarifa mapema kuwa itashambulia kambi za Marekani Iraq na kweli ilishambulia na kusababisha uharibifu

Imagine mtu anatoa taarifa kabisa kuwa anataka kushambulia kambi yenye vifaa bora ya Marekan na mwisho wa siku anashambulia na kufanikiwa kufanya uharibifu mkubwa.
 
ni nchi ambayo iliweka misingi imala ya UONGOZI
Asikwambie mtu DEMOCRASIA inadumaza

ukitaka nchi yako ifanikiwe na ipige HATUA achana na DEMOCRASIA
DEMOCRASIA ni mtego mbaya wa WESTERN
ili kuendelea kukutawala na kukididimiza
CHINA ingekuwa imefuata huo upuuzi isingefika pele ilipo same na IRAN pia

hata ULAYA na AMERICA iliichukua mamia ya miaka mpk kuja kuwa na SERA ya DEMOCRASIA baada kuwa imejengeka na wamekuwa IMARA

Ndio maana hatahapa NCHINI kwetu tunahitaji RAISI mwenye kariba ya HAYATI MAGUFURI Ili kusonga mbele
DEMOCRASIA kwangu mimi ni ADUI mkubwa kwa MATAIFA yanayoendelea kama hapa NCHIN kwetu
 
Unauhakika china hawana demokrasia au una jisemelesha humu jf.

#MaendeleoHayanaChama
 
Wakuu vipi, kwema.

Wakuu Iran ni mmoja kati ya nchi ambazo ziliwekewa vikwazo vikali na nchi za magharibi toka mnamo mwa miaka ya 70s huko hadi leo hii na siku zijazo.

Vikwazo hivyo ni vya kiuchumi, kijeshi nk, tena vimekuwa vikiongezwa siku hadi siku.

Tofauti na ilivyo kwa nchi nyingine kama vile Cuba, Venezuela nk zilizowekewa vikwazo pengine na marekan tu, au baadhi ya nchi za magharibi. vikwazo vya Iran vimewekwa na nchi za magharibi kama zote wakishirikiana na makampuni ya nchi hizo.

Lakini cha kushangaza Iran imeweza kuwa na uwezo hasa wa kijeshi sawa au pengine zaidi ya ule wa nchi ambazo hazijawahi kuwekewa vikwazo na nchi hizo.

Iran ni miongoni mwa nchi zenye eneo kubwa na watu wengi barani Asia, so pamoja na vikwazo vya kiuchumi walivyowekewa takriban miaka 50 na zaidi, lkn wameweza kuwa na mifumo mizuri ya kudhibiti hali ya umasikini nchini mwao, tofauti na nchi kama Venezuela ambazo vikwazo vya miaka miwili au mitatu vimesababisha mamilioni ya raia waishi maisha ya shida na ya umasikini kupita maelezo.

Pamoja na vikwazo vikali vya magharibi hasa kwa upande wa mambo ya ulinzi, lkn bado nchi hiyo imeweza kuonesha kuwa haipo chini au nyuma kijeshi hata siku moja. Wengi tuliona jinsi wa Iran walivyoziangamiza ndege zisizo na ruban zilizokuwa zinatumiwa na Marekan kupima upepo katika eneo lao, wengi tuliona jinsi Iran ilivyozilipua meli ambazo zilikuwa zinabeba wapelelezi mbali mbali wa magharibi karibu na eneo lake, wengi tuliona jinsi Iran ilivyoshambulia kambi kadhaa za Marekani kule Iraq na kusababisha maafa na uharibifu mkubwa katika kambi hizo baada ya Mmarekani kumuuwa mmoja wa maofisa wakubwa wa Iran kule Iraq, tena kabla ya kufanya mashambulizi hayo wa Iran walitoa taarifa mapema kuwa watalipiza kisasi kupitia kambi za wamarekan kule Iraq, so marekan ikajiandaa kuzuia shambulizi lkn mwisho wa siku shambulizi likashindikana kuzuilika na kuleta maafa kwa jeshi la nchi hiyo kubwa duniani.

Wengi tulishuhudia jinsi Iran ilivyotoa msaada wa silaha kwa kundi la hezbullah ambalo liliichachafya Israel inayopata msaada mkubwa wa fedha kutoka Marekani kwa ajili ya ulinzi wao. Hiyo ilikuwa mwaka 2006 hadi jumuiya ya kimataifa ikaingilia kati na kuomba ipatekane suluhu ya kudumu baina ya Israeli na hezbullah.

Wengi tulishuhudia jinsi Iran ilivyosimama na kumlinda Asad wa Syria katika vita vyake, hadi kupelekea mipango ya Marekani na nchi za magharibi kumng'oa imeshindikana.

Wengi tunashuhudia sasa jinsi silaha kidogo tu za ndege zisikuwa na rubani za Iran zinavyofanya uharibifu mkubwa, na kusababisha maafa makubwa na zaidi ya yale yaliokuwa yanafanywa na Russia kupitia silaha zake mwenyewe (Russia) huko Ukraine.
Mpaka Marekani na nchi zingine za magharibi zinapiga kelele, maana silaha zinazotumika sio zile za Russia ambazo zilikuwa zinampa jeuri raisi wa Ukraine kuona kwamba sasa vita vimekwisha.

Hata zile himars za Marekani sasa hivi zinaonekana hazifanyi kazi mbele ya maangamizi ya ndege hizi za Iran.

Sasa tujiulize, kama nchi iliyowekewa vikwazo na mataifa makubwa duniani kwa zaidi ya miaka 50 bado ina uwezo iliyo nao leo, sasa je kama isingewekewa vikwazo kwa miaka yote hiyo 50 leo ni nchi gani ambayo ingeitisha pale Asia na hata duniani kwa ujumla.

Hizo nilizosema hapa ni zile silaha ilizotoa kuwawezesha hao niliwataja washinde mapambano yao, hapo hatujazungumzia silaha zake mwenyewe alizoweka kwa lengo la kujilinda ambazo kwa sheria za kijeshi duniani huwa zinafanywa siri kubwa ili adui asizione.

Mpaka sasa Marekani na nchi za magharibi zinashindwa kujua ni njia gani nyingine ya kumdhibiti huyu mtemi, maana wamarekani waliwahi kumtumia msaudi mwaka jana, hapo hapo Iran hakuchelewesha akaangamiza mitungi yake mikubwa ya kuwekea mafuta mpaka saudia na dunia ikapiga kelele.

Hili taifa ni la maajabu sana, japo lina maadui wengi lililotengenezewa na nchi za magharibi na halipati msaada wa kifedha kutoka kwa nchi yoyote lkn bado linajiamini kupita maelezo.
Kumbe Israel wanapewa fedha za kujilinda na America?😎 Kweli wachovu
 
Back
Top Bottom