6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 2,819
- 5,996
- Thread starter
- #281
Mkuu acha kupoteza muda wako kumjibu mtu asiejua alichoandika. Yeye hajui kwamba dunia ya leo kila nchi ina mapandikizi wa kila aina. Kuna wayahudi kibao Iran na pia kuna waajemi, waturuki na waarab kibao Israel.Jamii ya Iran ina wayahudi takribani laki 8. Kutokea mapandikizi kwao ni kitu cha kawaida.
Ni kama USSR, baada ya Stalin kuwa rais alikuta Shirika la kijasusi limejaa wayahudi ambao walikuwa wafuasi wa rais wa Leon Trotsky na Lenin. Aliwaondoa taratibu mpaka mambo yakawa shwari.
Kwa kesi ya Iran nayo ipo namna hiyo! Kuna waajemi wayahudi na kwa namna hiyo mambo ya kuvuja siri ni kitu kinachowezekana.
Hivyo kila nchi huwatumia watu wao katika nchi fulani (sio asili) kwa upelelezi. Yeye hakuona kilichotokea 7 October. Liliandaliwa chezo fulan na waisrael wenye asili ya uajemi na waarab kuwazubaisha Mosad na jeshi ili wazee wa kazi waingie kufanya yao.
Na kweli mission ilifanikiwa kwa 100%, maana wazee wa kazi waliingia wakafanya operation yao kimya kimya na kisha kuondoka na kundi la watu zaidi ya elfu 1 bila kushtukiwa.
Lakini kijana alieshiba makande na uji wa mtama hilo halijui.